Agano Jipya 2023
Novemba 13–19. Yakobo: “Iweni Watendaji wa Neno na Si Wasikiaji tu”


“Novemba 13–19. Yakobo: ‘Iweni Watendaji wa Neno, Wala Si Wasikiaji Tu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2023)

“Novemba 13–19. Yakobo,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

kijana anasafisha ukuta

Novemba 13–19

Yakobo

“Iweni Watendaji wa Neno, Wala Si Wasikiaji Tu”

Kabla ya kusoma muhtasari huu, soma Waraka wa Yakobo na kuwa makini na ushawishi unaoupata. Je, ni kanuni gani unazipata ambazo zingebariki na kuwajenga washiriki wa darasa lako?

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Waalike washiriki wa darasa kushiriki mistari kutoka Yakobo ambayo imewapa msukumo wa kuwa “watendaji wa neno” (Yakobo 1:22). Kama si jambo la binafsi sana, wangeweza kushiriki kile wanachohisi wanahitaji kukifanyia kazi, kibinafsi au kama familia.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yakobo 1:5–6

Tunapoomba kwa imani, Mungu hutupatia kwa ukarimu.

  • Kanuni zinazofundishwa katika Yakobo 1:5–6 zilimuongoza Joseph Smith katika tukio lililomletea badiliko la maisha kiroho, na zinaweza kutubariki kila mmoja wetu katika njia fulani. Labda ungeweza kuandika maswali kama yafuatayo kwenye ubao na kuwaomba washiriki wa darasa kuyatafakari kimya kimya: ni ushawishi gani Yakobo 1:5–6 imekuwa nayo katika maisha yako? Je, uzoefu wa Joseph Smith kwenye mistari hii umekufundisha nini wewe kuhusu kutafuta hekima juu ya maswali yako mwenyewe? (ona Joseph Smith—Historia ya 1:10–17). Ni tukio gani limekufundisha wewe kwamba “ushuhuda wa Yakobo [ni] wa kweli”? ((Joseph Smith—Historia 1:26). Waalike washiriki wa darasa kushiriki mawazo waliyonayo baada ya kutafakari maswali haya.

  • Labda washiriki wa darasa wangeweza kuiweka Yakobo 1:5–6 katika maneno yao wenyewe. Ni kwa namna gani hii inawasaidia wao kuielewa mistari hii vizuri zaidi? Yawezekana ukataka kujadili pamoja kitu ambacho baadhi ya maneno kutoka kwenye mistari hii inamaanisha nini.

Yakobo 1:2–4; 5:7–11

Kama kwa uvumilivu tutasubiria, Bwana atatuongoza kwenye ukamilifu.

  • Ili kuanzisha mjadala juu ya mafundisho ya Yakobo kuhusu subira katika mistari hii, ungeweza kuwaalika washiriki wa darasa kusimulia juu ya tukio ambapo walitakiwa kuwa wavumilivu na walijifunza nini kutokana na tukio hilo. Kisha wangeweza kutafuta katika Yakobo 1:2–4; 5:7–11 kwa ajili ya kanuni ambazo zinahusiana na uzoefu wao. Wangeweza pia kupata kanuni za kutumia katika video “Continue in Patience” (ChurchofJesusChrist.org) au ujumbe wa Rais Dieter F. Uchtdorf “Endelea Katika Uvumilivu” (Liahoa, Mei 2010, 56–59). Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki kile walichojifunza kuhusu uvumilivu wakati walipokuja kuwajua Baba wa Mbinguni na Mwokozi. Je, ni kitu gani kimetusaidia sisi kukuza uvumilivu?

Yakobo 1:3–8, 21–25; 2:14–26

“Imani pasipo matendo imekufa.”

  • Njia mojawapo ya kujadili mafundisho ya Yakobo kuhusu imani na matendo ingeweza kuwa kwa kuligawanya darasa lako katika makundi mawili—moja kuchunguza kwa nini imani inahitaji matendo na lingine kwa nini matendo yanahitaji imani. Kufanya hivi, wangeweza kusoma Mathayo 7:21–23; Yakobo 1:6–8, 21–25; 2:14–26; and Joseph Smith—Historia ya 1:19. Kisha kila kundi lingeweza kuelezea walichokipata na kujadili kwa nini vyote imani na matendo ni muhimu.

    Ibrahimu akisali nje ya hema lake.

    “Ibrahimu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki” (Yakobo 2:23). Ibrahimu katika Uwanda wa Mamre, na Grant Romney Clawson

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari kwa kina zaidi kirai kikumbukwacho “Imani pasipo matendo imekufa” (Yakobo 2:26), ungeweza kuandika sentensi ifuatayo kwenye ubao: Imani bila matendo ni kama bila . Waalike washiriki wa darasa kufikiria njia za ubunifu ili kukamilisha sentensi, na waache waandike mawazo yao kwenye ubao. Tunaweza kufanya nini ili kuendelea daima kuifanyia kazi imani katika Yesu Kristo?

Yakobo 2:1–9

Kama wafuasi wa Yesu Kristo, hatuna budi kuwapenda watu wote, bila kujali hali zao.

  • Ili kuwahamasisha washiriki wa darasa kuonyesha upendo kama wa Kristo bila kujali hali za wengine au mwonekano wao wa nje, ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kupeana zamu kusoma mistari kutoka Yakobo1:9–11; 2:1–9; 5:1–6. Jadili maswali kama yafuatayo: Je, inamaanisha nini kuwa na “heshima kwa watu”? (Yakobo 2:9). Je, ni kwa nini wakati mwingine tunawatendea wale wenye fedha, umashuhuri, au uwezo tofauti na wale ambao hawana? Je, ni kwa namna gani tunaweza kuepuka kuwatendea wengine tofauti kulingana na hali walizo nazo? Ni kwa njia gani mfuasi wa kweli wa Mwokozi ni tajiri wa kweli kuliko wote? (ona JYakobo 2:5).

Yakobo 3

Maneno tunayoyatumia yana nguvu ya kuwaumiza wengine au kuwabariki.

  • Taswira madhubuti ambayo Yakobo aliitumia inaweza kutukumbusha na kutupa hamasa ya kutumia maneno—kwa kuongea na kuandika—ili kuwainua wengine. Fikiria kuwaalika washiriki wa darasa kupitia Yakobo 3, wakitafuta milinganisho Yakobo aliyotumia kuelezea jinsi gani maneno yanavyoweza kuumiza au kuwabariki wengine; baadhi ya washiriki wa darasa wanaweza kufurahia kuchora picha za kitu wanachopata. Je, ni kwa namna gani milinganisho hii inaelezea maelezo ya Yakobo katika sura hii? Kwa mfano, ni kwa namna gani maneno yetu yanaweza kuwa kama moto? Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao unaonyesha nguvu ambayo lugha inaweza kuwa nayo. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kutafakari ni kwa namna gani wanaweza kutumia ushauri wa Yakobo.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza mazingira yenye heshima. “Wasaidie washiriki wa darasa lako kuelewa kwamba kila mmoja wao ana mchango katika hali ya kiroho darasani. Wahimize wakusaidie kujenga mazingira ya uwazi, upendo, na heshima ili kwamba kila mtu ajisikie yuko salama kushiriki uzoefu, maswali na shuhuda zao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi15).