Agano Jipya 2023
Novemba 6–12. Waebrania 7–13: “Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo”


“Novemba 6–12. Waebrania 7–13 ‘Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021.)

“Novemba 6–12. Waebrania 7–13,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023

Picha
Melkizedeki akimpa baraka Abramu

Melkizedeki Akimbariki Abramu, na Walter Rane Kipawa cha msanii

Novemba 6–12

Waebrania 7–13

“Kuhani Mkuu wa Mambo Mema Yatakayokuwapo”

Unaposoma Webrania 7–13, tafakari ni ujumbe gani wa Bwana ulikuwa kwa ajili ya Waebrania Watakatifu. Pia angalia jumbe Zake kwako na kwa watu unaowafundisha.

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kabla ya kuanza darasa, alika washiriki wachache kuja wakiwa wamejiandaa kushiriki mistari kutoka Waebrania 7–13 ambayo iliwasaidia “kusogea karibu na [Mungu] kwa moyo wa kweli katika utimilifu wa imani” (Waebrania 10;22).

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Waebrania 7–10

Ibada za kale na za sasa huelekeza kwa Yesu Kristo.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kupekua Waebrania 7 kwa ajili ya vifungu vya maneno ambayo yanafundisha kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki na vinashuhudia juu ya Yesu Kristo. Waalike washiriki wa darasa kuelezea kile walichokipata. Au ungeweza kutoa muda kwa darasa kurejelea sura ya 7 na kupata mistari ambayo inafundisha juu ya ukuhani huu na kushuhudia juu ya Mwokozi. Ni kwa jinsi gani Melkizedeki alikuwa kama Yesu Kristo? (Ona majina ya Melkizedeki katika mstari wa 1–2 Jinsi gani Ukuhani wa Melkizedeki unatusaidia sisi kuja kwa Kristo? Labda washiriki wa darasa wangeweza kutafuta majibu yamkini katika Mada za Injili, “Ukuhani wa Melkizedeki” (topics.ChurchofJesusChrist.org).

  • Japokuwa hatutoi dhabihu za wanyama, tunashiriki katika ibada leo ambazo, katika njia sawa na hiyo, zinaelekeza nafsi zetu kwa Kristo na kutoa “njia zilizoruhusiwa ambazo kupitia hizo baraka na nguvu za mbinguni zinaweza kutiririka na kufika katika maisha yetu binafsi” (David A. Bednar, “Daima Tunza Ondoleo la Dhambi Zako,” Liahona, Mei 2016, 60). Labda mngeweza kuchunguza kwa pamoja jinsi ibada za kale zilizoelezewa katika Waebrania 8–10 ziliashiria dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi. Kwa mfano, je, damu ya ngombe dume na mbuzi huwakilisha nini? (ona Waebrania 9:13–14). Kuhani mkuu anamwakilisha nani (ona Waebrania 9:24–26). Video ya “Dhabihu na Sakramenti” (ChurchofJesusChrist.org) ingeweza kusaidia. Ni kwa namna gani ibada za sasa zimetubariki na kusaidia kutuelekeza kwa Yesu Kristo? Tunaweza kufanya nini ili kuzifanya ibada hizi kuwa na maana zaidi na zenye kufokasi kwa Mwokozi?

Waebrania10:34–38; 11.

Imani huitaji kutumaini katika ahadi za Mungu.

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa mafundisho ya Paulo kuhusu imani, ungeweza kuanza kwa kuwaomba wafikirie kuhusu jinsi gani wanaweza kuielezea imani katika sentensi moja. Kisha, someni na kujadiliana kama darasa maana iliyotolewa na Paulo katika Waebrania 11:1. Kisha ungeweza kumpangia kila mtu kuchagua mmoja wa watu waliotajwa katika Waebrania 11 ili ajifunze kuhusu mtu huyo. Washiriki wa darasa wangeweza kutumia tanbihi au Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org) ili kurejelea uzoefu wa mtu huyo katika Agano la Kale na kisha kushiriki na darasa kile walichokipata. Ni kwa namna gani watu hawa walionyesha kwamba walihisi “uhakika wa mambo yatarajiwayo”? (Tafsiri ya Joseph Smith, Waebrania 11:1 [katika Waebrania 11:1, tanbihi b]). Washiriki wa darasa wanaweza kuwa tayari kushiriki mifano ya watu walio waaminifu. Ni wakati gani tulitumia imani katika ahadi ambazo bado hazijatimizwa?

  • Ushauri kwa Watakatifu wa Kiebrania ambao walikuwa wakishawishika “kurudi nyuma” kutoka kwenye imani yao unaweza kuwa wa thamani kwa washiriki wa darasa ambao yawezekana kuwa wanahangaika na shuhuda zao. Ungeweza pia kuwasaidia wale wanaojaribu kuwasaidia wapendwa wao walio katika mapambano ya imani. Ili kugundua ushauri huu, washiriki wa darasa wangeweza kusoma Waebrania 10:34–38 na maelezo ya Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.” Ni kwa nini wakati mwingine tunashawishika kutupilia mbali kujiamini kwetu (ona Waebrania 10:35) katika Bwana na injili Yake ? Je, tunaweza kufanya nini ili kujenga na kudumisha imani na kujiamini ili “kupokea ahadi za [Mungu]”? (Waebrania 10:36). Video za “Good Things to Come” na “An High Priest of Good Things to Come” (ChurchofJesusChrist.org) zingeweza kuwa nyongeza ya mjadala huu.

Picha
ikoni ya nyenzo

Nyenzo za Ziada

“Kwa hivyo usitupe kujiamini kwako.”

Akirejelea kwa Waebrania 10:32–39, Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Hakika ni vigumu—kabla hujajiunga na Kanisa, wakati unajaribu kujiunga na baada ya kuwa umejiunga. Hivyo ndivyo mara zote ilivyokuwa, Paulo alisema, lakini usirudi nyuma. Usihangaike na kurudi nyuma. Usipoteze kujiamini kwako. Usisahau ulivyohisi hapo awali. Usiache kuamini uzoefu uliowahi kuwa nao. …

Katika kila uamuzi muhimu kuna maonyo na mambo ya kufikiria, lakini mara kunapokuwa na mwangaza, kuwa makini na majaribu ya kukurudisha nyuma kutoka kwenye mambo mema. Kama ilikuwa sahihi ulipokuwa ukiliombea kuhusu hilo na kuamini na kuishi kwa hilo, basi ni sahihi hata sasa. Usikate tamaa wakati shinikizo linapokuwa kubwa. … Kabiliana na mashaka yako. Shinda woga wako. ‘Kwa hivyo, usitupe kujiamini kwako.’ Baki katika njia na uone uzuri wa maisha ukifunuliwa kwa ajili yako” (“Kwa hivyo Usitupe Ujasiri Wako,” Ensign, Machi. 2000, 8–9).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Nenda kwenye Maandiko kwanza. Maandiko yanapaswa kuwa chanzo cha msingi cha maandalizi na kujifunza kwako. Maneno ya manabii wa sasa yanaweza kujaliza maandiko kwenye vitabu vitakatifu (ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 17).

Chapisha