“Oktoba 30–Novemba 5. Waebrania 1–6: ‘Yesu Kristo, ‘Sababu ya Wokovu wa Milele’’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano Jipya 2023 (2021)
“Oktoba 30–Novemba 5. Waebrania 1–6,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Oktoba 30–Novemba 5
Waebrania 1–6
Yesu Kristo, “Sababu ya Wokovu wa Milele”
Fikiria kushiriki na washiriki wa darasa lako baadhi ya misukumo ambayo umepokea kutoka kwa Roho Mtakatifu kuhusu Waebrania 1–6. Kwa kufanya hivyo unaweza kuwashawishi wao kutafuta misukumo yao wenyewe wakati wakijifunza maandiko.
Alika Kushiriki
Baadhi ya washiriki wa darasa ambao hawashiriki mara nyingi katika darasa, wanaweza kuhitaji mwaliko maalum na muda kidogo ili kujiandaa. Ungeweza kuwasiliana na wachache kati yao siku moja au mbili kabla na kuwaomba waje wakiwa wamejiandaa kushiriki mstari kutoka Waebrania 1–6 ambao ni wa maana kwao.
Fundisha Mafundisho
Yesu Kristo ni “sababu ya wokovu wa milele.”
-
Ni kwa namna gani unaweza kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki maandiko yenye maana kwao kuhusu Yesu Kristo ambayo waliyapata katika kujifunza kwako binafsi na katika familia wiki hii? Fikiria kutengeneza safu tano kwenye ubao zikiwakilisha sura tano za kwanza katika Waebrania. Waalike washiriki wa darasa kuandika katika safu husika virai kutoka kwenye sura hizi ambavyo viliwafundisha kuhusu Yesu Kristo na mstari ambapo kirai hicho kinapatikana. Ni kwa namna gani kujua vitu hivi kuhusu Mwokozi kunagusa imani yetu Kwake na utayari wa kumfuata Yeye?
Waebrania 2:9–18; 4:12–16; 5:7–8
Yesu Kristo aliteseka kwa yote ili kwamba Aweze kuelewa na kutusaidia sisi wakati tunapoteseka.
-
Waebrania 2:9–18; 4:12–16; 5:7–8 inaweza kuwasaidia watu wanaoangalia mateso ulimwenguni na kujiuliza kama Mungu anatambua au hata kama anajali. Labda washiriki wa darasa wangeweza kuchunguza mistari hii ili kupata kweli ambazo zingeweza kusaidia katika maswali kama hayo. Mistari hii inafundisha nini kuhusu jinsi Mwokozi anavyoitikia katika mateso ya binadamu? Inaweza pia kusaidia kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki mifano kutoka maandiko ambapo watu walisaidiwa na Yesu Kristo katika masumbuko yao (ona “Nyenzo za Ziada”) au onyesha video ya “Mountains to Climb” (ChurchofJesusChrist.org). Washiriki wa darasa wangeweza kujadili kitu wanachojifunza kuhusu jinsi Mwokozi anavyoweza kutusaidia wakati tunapokabiliwa na changamoto ngumu.
Baraka za Mungu zinapatikana kwa wote ambao “hawaifanyi mioyo [yao] kuwa migumu.”
-
Waebrania 3 na4 zina ombi kwa Watakatifu la kutoifanya mioyo yao kuwa migumu na kupelekea kukosa baraka ambazo Mungu alitaka kuwapa. Wakati wewe na darasa lako mkisoma Waebrania 3:7–4:2, jadilini njia ambazo uzoefu wa Waisraeli wa zamani ungeweza kutumika kwetu leo, kama zilivyotumika kwa Waebrania katika Kanisa la mwanzo (ona nyenzo za kujifunza kuhusu mistari hii katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia). Tunaweza kufanya nini ili kuiweka mioyo yetu iwe laini na yenye kuitikia mapenzi ya Bwana? (ona Methali 3:5–6; Alma 5:14–15; Etheri 4:15). Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi wao au watu wengine wanaowafahamu wamebarikiwa kwa sababu wamekuwa na mioyo laini na minyoofu.
Wale wanaohudumu katika ufalme wa Mungu lazima waitwe na Mungu.
-
Ujumbe katika Waebrania 5 kuhusu wenye ukuhani kuitwa na Mungu unaweza kutumika kwa wote ambao wanasimikwa kwenye mamlaka ya ukuhani ili kuhudumu katika miito ya Kanisa. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa lako kuelewa nini humaanishwa kwa “kuitwa na Mungu kama Haruni,” fikiria kuwaalika kurejea tukio la Haruni akipokea wito wake katika Kutoka 4:10–16, 27–31; 28:1. Ni tambuzi gani kutoka kwenye hadithi hii hutusaidia sisi kuelewa Waebrania 5:1–5? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi wao walivyopokea uthibitisho kwamba mtu fulani aliitwa na Mungu kutimiza wito maalumu—inajumuisha, pengine, wao wenyewe. Ni kwa namna gani uthibitisho huo unawasaidia wao kumkubali zaidi mtu huyo katika wito wake?
Nyenzo za Ziada
Mifano ya kimaandiko ya watu waliofarijiwa na Yesu Kristo.
-
Yohana 8:1–11: Bwana alimfariji mwanamke aliyehukumiwa kwa uzinzi.
-
Yohana 11:1–46: Bwana alimfariji Mariamu na Martha baada ya kifo cha kaka yao, Lazaro.
-
Enoshi 1:4–6: Bwana alisamehe dhambi za Enoshi na kuondoa hatia yake.
-
Mosia 21:5–15: Bwana alilainisha mioyo ya Walamani kwamba wakaanza kupunguza mizigo ya watu wa Limhi.
-
Mosia 24:14–15: Bwana aliwaimarisha watu wa Alma ili waweze kubeba mizigo yao.
-
Etheri 12:23–29: Maneno ya Bwana yalimfariji Moroni.
-
3 Nefi 17:6–7: Bwana aliwaponya Wanefi udhaifu wao.
-
Mafundisho na Maagano 121:7–10: Bwana alimfariji Joseph Smith (ona pia Mafundisho na Maagano 123:17).