“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili : Agano Jipya 2023 (2022)
“Nyenzo za Ziada,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2023
Nyenzo za Ziada
Nyenzo hizi zinaweza kupatikana katika app ya Maktaba ya Injili kwenye ChurchofJesusChrist.org.
Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia
Unaweza kutohoa na kutumia shughuli yoyote kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia kwa ajili ya matumizi katika darasa lako la Shule ya Jumapili. Kama washiriki wa darasa wametumia shughuli hizi katika kujifunza kwao binafsi injili au kama familia, wahimize kushiriki na wengine uzoefu na utambuzi wao.
Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto
Muziki mtakatifu humwalika Roho, unatusaidia kuusikia upendo wa Mungu, hufundisha injili katika njia ya kukumbukwa. Katika nyongeza ya kutumia toleo lililopigwa chapa la Nyimbo za Kanisa na Kitabu cha Nyimbo za Watoto, unaweza kupata rekodi za sauti na video za nyimbo nyingi za kanisa na nyimbo za watoto kwenye music.ChurchofJesusChrist.org na katika app za Music na Gospel Media.
Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo
Vitabu vya Kiada vya Seminari na Chuo hutoa chimbuko la kihistoria na maoni ya kimafundisho kwa kanuni na hadithi zinazopatikana katika maandiko. Vinaweza pia kuchochea mawazo ya kufundisha kwa ajili ya madarasa ya Shule ya Jumapili.
Magazeti ya Kanisa
Magazeti ya Liahona na Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana yanatoa makala na tarifa zingine ambazo zinaweza kuongezea kanuni unazofundisha kutoka katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili.
Mada za Injili
Kwenye Mada za Injili (topics.ChurchofJesusChrist.org), unaweza kupata taarifa za msingi kuhusu mada mbali mbali za injili, sambamba na viunganisho kwenye nyenzo saidizi, kama vile mahubiri ya mkutano mkuu yanayoshabihiana, makala, maandiko na video. Unaweza pia kupata Insha za Mada za Injili, ambazo hutoa taarifa za kina kuhusu mambo ya kimafundisho na kihistoria, vilevile majibu ya maswali mbalimbali kuhusu Kanisa na mafundisho Yake.
Preach My Gospel
Mwongozo huu wa wamisionari hutoa muhtasari wa kanuni za msingi za injili.
Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana (kijitabu)
Nyenzo hii inatoa muhtasari wa viwango vya Kanisa ambavyo vinaweza kutusaidia kuishi injili na kufurahia wenza wa Roho. Unaweza kuirejelea mara kwa mara, hasa ikiwa unawafundisha vijana.
Video na Sanaa
Sanaa za kuchora, video, na vyombo vingine vya habari vinaweza kuwasaidia wale unaowafundisha kupata taswira ya mafundisho na hadithi zinazohusiana na maandiko. Tembelea Gospel Media katika GospelMedia.ChurchofJesusChrist.org ili kuvinjari mkusanyiko wa nyenzo za habari za Kanisa. Gospel Media pia inapatikana kama app ya simu ya mkononi. Picha nyingi ambazo unaweza kutumia katika darasa zinapatikana katika Kitabu cha Sanaa ya Injili.
Kufundisha katika Njia ya Mwokozi
Kufundisha katika Njia ya Mwokozi inaweza kukusaida kujifunza kuhusu, na kutumia kanuni za kufundisha kama Kristo. Kanuni hizi zinajadiliwa na kufanyiwa mazoezi katika mikutano ya baraza la mwalimu.