Agano la Kale 2022
Februari 14–20. Mwanzo 18–23: “Je Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”


“Februari 14–20. Mwanzo 18–23: ‘Je Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 14–20. Mwanzo 18–23,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Sara akiwa amembeba mtoto Isaka

Sara na Isaka, na Scott Snow

Februari 14–20

Mwanzo 18–23

“Je, Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”

Unapojiandaa kufundisha, kumbuka kwamba washiriki wa darasa wanaweza kuwa walikuwa na uzoefu wao wenye maana wakati waliposoma Mwanzo 18–23. Unaweza kufanya nini cha kuwatia moyo kushiriki uzoefu huu na umaizi? Fikiria kuruhusu umaizi huo kushawishi majadiliano ya darasa.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Majaribu yetu na mateso mara nyingi huwa nyakati za ufafanuzi katika maisha yetu. Mwanzo 18–23 inaelezea nyakati kadhaa kama hizo katika maisha ya Ibrahimu na Lutu. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mstari walioupata wakati wa kujifunza kwao binafsi wiki hii ambao unaelezea wakati wa ufafanuzi unaowezekana kwa Ibrahimu. Kisha wangeweza kushiriki kile walichojifunza kutokana na hilo.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mwanzo 18:9–14; 21:1–7

Bwana anatimiza ahadi Zake kwa wakati wake Mwenyewe.

  • Maelezo kwenye mistari hii yanaweza kuwa ya kutia moyo kwa washiriki wa darasa wanaojiuliza kama ahadi za Mungu kwao zitatimizwa. Kwa kuanza majadiliano, inaweza kusaidia kuwaomba washiriki wa darasa kurejea upya na mtu mwingine katika darasa maelezo ya ahadi za Mungu kwa Ibrahimu na Sara kwenye mwanzo 17:4, 15–22; 18:9–14 na utimilifu wa ahadi hizo kwenye Mwanzo 21:1–7. Ni nini katika mistari hii kinaonekana kwa washiriki wa darasa? Ni kweli gani tunazipata kutokana na uzoefu wa Ibrahimu na Sara wa kushiriki na rafiki ambaye anakata tamaa kwamba Mungu atatimiza ahadi Zake? Maandiko gani mengine au uzoefu binafsi tunaweza kuushiriki? (ona, kwa mfano, Warumi 8:28; Waebrania 11; Mormoni 9:19–21; Mafundisho na Maagano 88:64). Ni uzoefu gani washiriki wa darasa wangeshiriki ambao kupitia huo ahadi za Mungu zilitimizwa katika maisha yao? Jinsi gani tunahimili imani yetu wakati baraka zilizoahidiwa zinaweza kutopokewa katika maisha haya? (ona Waebrania 11:8–13).

Mwanzo 7:15–26

Kama wafuasi wa Yesu Kristo, hatuna budi kuukimbia uovu na kutokuangalia nyuma.

  • Masomo gani unayohisi washiriki wa darasa wangeweza kujifunza kutokana na maelezo ya familia ya Lutu wakikimbia kutoka Sodoma na Gomorra? Somo moja linalowezekana limependekezwa katika kauli ya Mzee Jeffrey R. Holland katika “Nyenzo za Ziada.” Pengine ungeweza kulishiriki na darasa baada ya kufanyia muhutasari matukio yaliyoelezwa kwenye Mwanzo 19:15–26. Kwa njia zipi au katika hali gani wakati mwingine sisi “[huangalia] nyuma” (mstari wa 26) wakati tunatakiwa kuangalia mbele kwa imani katika Mwokozi? Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu ambao unaelezea kwa mfano umuhimu wa kutokuangalia nyuma. Ni nini Luka 9:62 inaongeza kwenye uelewa wetu wa wazo hili?

    Kielelezo cha Lutu na familia yake wakikimbia kutoka Sodoma na Gomorra

    Kukimbia kutoka Sodoma na Gomorra, na Julius Scknorr von Carolsfeld

Mwanzo 22:1–14

Utayari wa Ibrahimu kumtoa dhabihu Isaka ni mfano wa Mungu na Mwanae.

  • Maelezo ya Ibrahimu kumtoa mwanawe kama dhabihu yanaweza kutufundisha kuhusu dhabihu ya Baba wa Mbinguni ya Mwanae. Njia moja ya kuchunguza maelezo haya ni kupangia nusu ya darasa kutafakari Mwanzo 22:1–14 kutoka kwenye taswira za Ibrahimu na Mungu Baba, wakati nusu nyingine ikitafakari maelezo haya kutoka taswira ya Isaka na Yesu Kristo. Waombe washiriki wa darasa kushiriki umaizi wanaoupata. Kwa upekee, nini washiriki wa darasa wanajifunza ambacho kinaongeza shukrani zao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo? Kama sehemu ya majadiliano haya, ungeweza kuonesha picha ya Ibrahimu akimchukuwa Isaka Kutolewa Dhabihu (Kitabu cha sanaa za Injili, na. 9) au onesha video “Akedah (The Binding)” (ChurchofJesusChrist.org).

additional resources icon

Nyenzo za Ziada

“Imani siku zote imeelekezwa kuelekea badaaye.”

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Inawezekana kwamba mke wa Lutu aliangalia nyuma kwa uchungu kwa Bwana kwa kile alichokuwa Anamtaka kuacha nyuma. … Kwa hiyo si tu kwamba aliangalia nyuma; aliangalia nyuma kwa kutamani. Kwa kifupi, upendo wake kwa yaliyopita ulizidi kujiamini kwake kwa siku za baadaye. …

“… Ninawasihi nyinyi, msiwepo kwenye siku zilizopita tayari wala kutamani bure kwa ajili ya jana, hata kama jana hizo zilikuwa za kupendeza sana. Yaliyopita ni ya kujifunza lakini siyo ya kuyaishi. Tunatazama nyuma kudai makaa kutoka kwenye uzoefu unaowaka na si majivu. Na tunapookuwa tumejifunza kile tunachokihitaji na tumepata ubora ambao tumepata uzoefu wake, hivyo tunatazama mbele na kukumbuka kwamba imani siku zote imeelekezwa kuelekea badaaye. …

“… [Mke wa Lutu] hakuwa na imani. Alitilia mashaka uwezo wa Bwana kumpa yeye kitu kizuri zaidi kuliko alichokuwa nacho tayari. Inavyoonekana, alifikiri kwamba hakuna ambacho kingeweza kuwa kizuri kama kile alichokuwa anakiacha nyuma. …

“… kuishi maisha ya zamani, ikiwa ni pamoja na makosa yaliyopita, kwa kweli sio sahihi! Siyo injili ya Yesu Kristo” (“The Best Is Yet to Be,” Ensign, Jan. 2010, 24, 26–27).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ahidi baraka. Wakati unapowaalika wale unaowafundisha kutenda yale wanayojifunza, toa pia ushuda juu ya baraka ambazo Mungu amewaahidi wale wanaofanya hivyo. (Ona pia Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 35.)