Agano la Kale 2022
Januari 31–Februari 6. Mwanzo 6–11; Musa 8: “Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana”


“Januari 31–Februari 6. Mwanzo 6–11; Musa 8: ‘Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Januari 31–Februari 6. Mwanzo 6–11; Musa 8,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Nuhu, familia yake, wanyama, safina, na upinde wa mvua

Kielelezo cha Nuhu akitoka kwenye safina, na Sam Lawlor

Januari 31–Februari 6

Mwanzo 6–11; Musa 8

“Nuhu akapata neema machoni pa Bwana”

Muhtasari huu unasisitiza kanuni zinazopatikana katika Mwanzo 6–11 na Musa 8, lakini hizi sio kanuni pekee ambazo ungeweza kuzilenga unapofundisha. Amini misukumo ya Roho unayopata unapojifunza maandiko.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Fikiria kuwataka washiriki wa darasa kushiriki ujumbe wa kiroho kwa ajili ya wakati wetu kutokana na hadithi ya Nuhu au Mnara wa Babeli. Watie moyo kushiriki maandiko ambayo yanasaidia ujumbe huu.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mwanzo 6–8; Musa 8

Kuna usalama wa kiroho kwa kumfuata nabii wa Bwana.

  • Uovu katika siku za Nuhu unaweza kutukumbusha sisi juu ya uovu tunaouona unatuzunguka leo. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kufaidika kutokana na masomo ya hadithi ya Nuhu, ungeweza kuandika kwenye ubao Maonyo na Uthibitisho. Washiriki wa darasa wangeweza kuhakiki Mwanzo 6–8 au Musa 8:13–30 na kupata kitu fulani wanachohisi ni onyo muhimu kwa wakati wetu na kitu fulani wanachofikiria kinathibitisha (ona pia “Nyezo za Ziada”). Wangeweza kuandika kile wanachokipata chini ya kichwa cha habari kinachofaa ubaoni. Kwa nini hadithi ya Nuhu ni yenye thamani kwetu leo?

Mwanzo 9:8–17

Alama na ishara zinatusaidia kukumbuka maagano yetu na Bwana.

  • Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unapendekeza kusoma Mwanzo 9:8–17 na kutafakari jinsi ishara au alama zinavyoweza kutumika kama ukumbusho wa maagano yetu. Kuwasaidia washiriki wa darasa kushiriki mawazo yao, unaweza kuleta darasani kiasi kidogo cha vitu ambavyo vinatukumbusha kuhusu vitu muhimu—kama vile pete ya ndoa, bendera ya taifa, au kishikizo cha jina la mmisionari—na zifananishe na “ishara” ya upinde wa mvua. Nini Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 9:21–25 (katika kiambatanisho cha Biblia) inatufundisha kuhusu ishara? Jinsi gani Mungu anatumia ishara au alama kutusaidia kukumbuka maagano yetu?

Mwanzo 11:1–9

Njia pekee ya kufika mbinguni ni kwa kumfuata Yesu Kristo.

  • Maelezo ya watu wa Babeli kujenga mnara yanatoa utofauti wa kuvutia kwenye maelezo ya Henoko na watu wake kujenga Sayuni, ambayo washiriki wa darasa walijifunza wiki iliyopita. Makundi yote mawili ya watu yalikuwa yakijaribu kufika mbinguni lakini katika njia tofauti. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kuorodhesha ubaoni chochote wanachokumbuka kuhusu watu wa Sayuni (ona Musa 7:18–19, 53, 62–63, 69) na nini wanajifunza kutoka mwanzo 11:1–9 na Helamani 6:26–28 kuhusu watu wa Babeli. Ni Tofauti gani wanazozipata? Hii inakufundisha nini kuhusu juhudi zetu kurudi kwenye uwepo wa Mungu?

    mnara wa Babeli

    Kielelezo cha Mnara wa Babeli, na David Green

  • Jiji la kale la Babeli halipo tena, lakini kiburi na mambo ya kidunia lililoashiria yapo. Kuwasaidia washiriki wa darasa kutumia masomo kutoka Mnara wa Babeli kwenye maisha yao, anza kwa kuwataka kurejea Mwanzo 11:1–9. Kisha ungeweza kugawa vipande vya karatasi na watake washiriki wa darasa kuandika vitu watu wanavyovifanya ambavyo vinawavuta mbali na Mungu; kisha, kwenye vipande vingine vya karatasi, wangeweza kuandika vitu watu wanavyofanya ambavyo vinawavuta karibu zaidi kwa Mungu. Unaweza kufurahia kupanga kundi la kwanza la karatasi kwenye ubao katika umbo la mnara na kundi la pili katika umbo la hekalu. Mungu ametoa nini kutusaidia “kufika mbinguni”? (Mwanzo 11:4; ona pia Yohana 3:16). Mnaweza kuimba wimbo juu ya mada, kama vile “Nearer, My God ,to Thee” (Nyimbo za Kanisa, na. 100).

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Masomo kutoka kwa Nuhu.

Rais Henry B. Eyring alisema:

“Kushindwa kukubali ushauri wa kinabii hupunguza nguvu zetu za kukubali ushauri zaidi baadae. Muda muafaka wa kuweza kuamua kumsaidia Nuhu kujenga safina ulikuwa ni mara ya kwanza alipoomba. Kila muda alipoomba baada ya hapo, kila kushindwa kuitikia kungeweza kupunguza umakini kwa Roho. Na kwa hiyo kila muda ombi lake lingeonekana la kipumbavu zaidi, mpaka mvua ilipokuja. Na kisha ilikuwa wameshachelewa.

“Kila muda katika maisha yangu ambapo nimechagua kuchelewa kufuata ushauri wa kuvuvia au kuamua kwamba nilikuwa sihusiki, nilikuja kujua kuwamba nilijiweka katika njia ya kudhuru. Kila muda nilipousikiliza ushauri wa manabii, kuhisi ukithibitishwa katika sala, na halafu kuufuata, niligundua kuwa nilisogelea usalama” (“Finding Safety in Counsel,” Ensign Mei 1997, 25).

Kwa nini Mungu alituma Gharika?

Baadhi ya Watu wanastaajabu kuhusu haki ya Mungu katika kutuma gharika “kumfutilia mbali mwanadamu” (Mwanzo 6:7). Mzee Neal A. Maxwell ilieleza kwamba wakati wa Gharika Kuu, “uharibifu ulikuwa umefikia kiwango cha kuharibu uhuru wa kuchagua kwamba roho hazikuweza, katika haki, kuletwa hapa” (We Will Prove Them Herewith [1982], 58).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Ruhusu Muda kwa ajili ya kutafakari. Maswali mazuri yanahitaji kutafakari, kutafiti, na misukumo. Wape washiriki wa darasa dakika chache kutafakari swali kabla ya kuomba majibu. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 31–34.)