Agano la Kale 2022
Januari 31–Februari 6. Mwanzo 6–11; Musa 8: “Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana”


“Januari 31–Februari 6. Mwanzo 6–11; Musa 8: ‘Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Januari 31–Februari 6. Mwanzo 6–11; Musa 8,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Nuhu, familia yake, wanyama, safina, na upinde wa mvua

Kielelezo cha Nuhu akiondoka kwenye safina, na Sam Lawlor

Januari 31–Februari 6

Mwanzo 6–11; Musa 8

“Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana”

Hadithi katika maandiko zinaweza mara nyingi kutufundisha masomo mengi ya kiroho. Unaposoma kuhusu Gharika Kuu na Mnara wa Babeli tafuta mwongozo wa kiungu kuhusu jinsi kumbukumbu hizi zinavyotumika kwako wewe.

Andika Misukumo Yako

Vizazi vya wasomaji wa Biblia wamekuwa wakishawishiwa na hadithi ya Nuhu na Gharika. Lakini sisi ambao tunaishi katika siku za mwisho tunayo sababu maalumu ya kuisikiliza kwa makini. Wakati Yesu alipofundisha jinsi tunavyopaswa kutazamia kwa ajili ya Ujio Wake wa Pili, Yeye alisema, “Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo pia kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Mtu” (Joseph Smith—Mathayo 1:41). Kwa nyongeza, vifungu vya maneno ambavyo vinaelezea siku ya Nuhu, kama “imeharibika” na “imejaa dhuluma,” vinaweza tu kuwa vinaelezea wakati wetu (Mwanzo 6:12–13; Musa 8:28). Hadithi ya Mnara wa Babeli pia yaonekana kutumika kwa siku yetu, na maelezo yake ya kiburi yakifuatiwa na ghasia na mgawanyiko miongoni mwa watoto wa Mungu.

Historia hizi ni za thamani si tu kwa sababu zinatuonyesha sisi kwamba uovu unajirudia wenyewe katika historia yote. Muhimu zaidi, zinatufundisha sisi kitu cha kufanya kuhusu hilo. Nuhu “akapata neema machoni pa Bwana” (Musa 8:27) licha ya uovu ulio mzunguka. Na familia za Yaredi na kaka yake walimgeukia Bwana na wakaongozwa mbali na uovu uliokuwa katika Babeli (ona Etheri 1:33–43). Kama tunajiuliza jinsi ya kujiweka wenyewe na familia zetu salama kipindi cha wakati wetu wa uharibifu na ghasia, hadithi hizi maarufu katika milango hii zinayo mengi ya kutufundisha.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mwanzo 6; Musa 8

Kuna usalama wa kiroho katika kumfuata nabii wa Bwana.

Shukrani kwa injili ya urejesho, tunajua mengi zaidi kuhusu Nuhu kuliko kile kinachopatikana katika Agano la Kale. Tafsiri yenye mwongozo wa kiungu ya Joseph Smith ya Mwanzo 6, inayopatikana katika Musa 8, inafunua kwamba Nuhu alikuwa mmoja wa manabii wakuu wa Mungu. Yeye alitawazwa na kutumwa kuhubiri injili ya Yesu Kristo, yeye alitembea na kuongea na Mungu, na aliteuliwa kuwaleta tena upya watoto wa Mungu juu ya dunia baada ya Gharika (ona pia Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith [2007], 104, 201). Je unajifunza nini kuhusu manabii kutokana na uzoefu wa Nuhu?

Wakati unaposoma kuhusu siku ya Nuhu, unaweza kugundua mifanano na siku yetu. Kwa mfano:

Je, manabii wanafundisha nini leo kuhusu injili ya Yesu Kristo ambacho kingeweza kukuweka wewe salama katika ulimwengu wa leo? Unaposoma kuhusu uzoefu wa Nuhu, ni kitu gani kinachokushawishi wewe kuwafuata manabii wa Bwana leo?

Ona pia Mosia 13:33; Mafundisho na Maagano 21:4–7.

Mwanzo 9:8–17

Ishara au alama zinatusaidia kukumbuka maagano yetu na Bwana.

Maagano ya injili yanaweza kuwakilishwa na ishara, alama, au “dalili” (Mwanzo 9:12). Kwa mfano, fikiria kuhusu jinsi gani mkate na maji ya sakramenti au maji ya ubatizo hutukumbusha ukweli mtakatifu unaohusiana na maagano yako. Kulingana na Mwanzo 9:8–17, je, upinde wa mvua unaweza kuleta nini katika mawazo yako? Je, Tafsiri ya Joseph Smith ya, Mwanzo 9:21–25 (katika kiambatisho cha Biblia) kinaongeza nini katika uelewa wako? Je, ni kwa nini Bwana anakutaka wewe umkumbuke Yeye na maagano uliyofanya?

Ona pia Gerrit W. Gong, “Daima Wamkumbuke,” Liahona, Mei 2016, 108–11.

Mwanzo 11:1–9

Njia pekee ya kufika mbinguni ni kwa kumfuata Yesu Kristo.

Babeli ya zamani, au Babilonia, imetumika tangu zamani kama alama ya uovu na kiulimwengu (ona Ufunuo 18:1–10; Mafundisho na Maagano 133:14). Unapojifunza Mwanzo 11:1–9, tafakari utambuzi uliotolewa na nabii Mormoni, ambaye aliandika kwamba ilikuwa ni Shetani “ambaye aliweka ndani ya mioyo ya watu kujenga mnara mrefu wa kutosha ili wapate kufika mbinguni” (Helamani 6:28; ona pia mstari wa 26–27). Je ni maonyo gani hadithi ya Mnara wa Babeli yanayo kwa ajili yako wewe?

Ona pia Zaburi 127:1.

Picha
mnara wa Babeli

Kielelezo cha Mnara wa Babeli na David Green

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mwanzo 6–8.Je, ni kwa jinsi gani unaweza kutumia hadithi ya safina ya Nuhu ili kuifundisha familia yako jinsi gani kumfuata nabii kunaweza kutuweka salama kiroho? (ona “Noah and His Family,” katika Hadithi za Agano la Kale). Pengine familia yako ingefanya kazi pamoja ya kujenga kiboti rahisi cha bandia kwa kutumia karatasi au mbao. Unaposoma Mwanzo 6–7, ungeweza kulinganisha usalama unaotolewa na boti na usalama tunaopata katika kumfuata nabii. Unaweza kujadili ushauri wa hivi karibuni kutoka kwa nabii na uandike maneno yake ya ushauri juu ya boti lako.

Je, Mungu ametupa kitu gani kingine ambacho tunaweza kukilinganisha na safina ambayo iliokoa familia ya Nuhu? Nyenzo hizi zinapendekeza baadhi ya majibu, ingawa kuna mengine mengi: 2 Nefii 9:7–13; Mafundisho na Maagano 115:5–6; na ujumbe wa Rais Russell M. Nelson “Kuwa Mtakatifu wa Siku za Mwisho wa Mfano” (Liahona, Nov. 2018, 113–14).

Musa 8:17.Je, inamaanisha nini kwa Roho wa Bwana “kujishughulisha na sisi? (ona 1 Nefi 7:14; Mafundisho na Maagano 1:33). Je, ni lini tuliona Roho akijishughulisha na sisi?

Mwanzo 9:8–17.Watoto wadogo pengine wangefurahia kuchora au kupaka rangi upinde wa mvua wakati ukizungumza kuhusu kile upinde huu unawakilisha (ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 9:21–25 [katika kiambatisho cha Biblia]). Ungeweza pia kujadili mambo ambayo yanatusaidia kukumbuka maagano yetu, kama vile sakramenti, ambayo inatusaidia kukumbuka agano letu la ubatizo la kumfuata Yesu Kristo (ona Mafundisho na Maagano 20:75–79).

Mwanzo 11:1–9.Yaweza kuwa vyema kusoma Etheri 1:33–43 wakati familia inajifunza Mwanzo 11 na inajifunza kuhusu Mnara wa Babeli. Je, tunajifunza nini kutoka katika familia za Yaredi na kaka yake ambacho kinaweza kusaidia familia yetu kupata usalama wa kiroho licha ya uovu katika ulimwengu? Je, ni masomo gani ya ziada tunayojifunza kutoka kwa Nuhu na familia yake wakati wakikabiliana na changamoto zinazofanana? (ona Musa 8:13, 16–30).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto,, 110–11 (mstari wa 3).

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Shiriki mawazo yako. Wakati unapoeleza kile unachojifunza kutoka kwenye maandiko, siyo tu unabariki wengine bali pia unakuza uelewa wako mwenyewe. Je, unajisikia kushawishika kueleza nini kutoka kwenye maandiko kwa familia yako, marafiki, au kwa washiriki wa kata?

Picha
Safina ya Nuhu

Picha ya kuchora ya safina ya Nuhu, na Adam Klint Day

Chapisha