Agano la Kale 2022
Februari 7-13. Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2: “Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki”


“Februari 7-13. Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2: ‘Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 7-13. Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Ibrahimu na Sara

Kielelezo cha Ibrahimu na Sara, na Dilleen Marsh

Februari 7-13

Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2

“Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki”

Unaposoma kuhusu Abramu na Sarai (baadae waliitwa Ibrahimu na Sara) na familia zao, tafakari jinsi mifano yao inavyokuvutia wewe. Andika mawazo yako kuhusu kile unachoweza kufanya “ili kuwa mfuasi mkubwa wa haki” (Ibrahimu 1:2).

Andika Misukumo Yako

Kwa sababu ya agano Mungu alilofanya na yeye, Ibrahimu amekuwa akiitwa “baba wa walio waaminifu” (Mafundisho na Maagano 138:41) na “Rafiki wa Mungu” (Yakobo 2:23). Mamilioni leo wanamheshimu kama babu yao halisi, na wengine wameasiliwa katika familia yake kupitia uongofu katika injili ya Yesu Kristo. Ingawa Ibrahimu mwenyewe amekuja kutoka katika familia iliyokuwa na matatizo—baba yake, ambaye aliitelekeza ibada ya kweli ya Mungu, alijaribu kumtoa Ibrahimu kuwa dhabihu kwa miungu wa uongo. Bila kujali hili, tamaa ya Ibrahimu ni “kuwa mfuasi mkubwa wa haki” (Ibrahimu 1:2), na historia ya maisha yake inaonyesha kwamba Mungu aliheshimu tamaa yake. Maisha ya Ibrahimu yanasimama kama ushuhuda kwamba bila kujali historia ya familia ya mtu ilivyokuwa, hatima yake inaweza kujazwa na matumaini.

Picha
Learn More image
Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Ibrahimu 1:1–19

Mungu atanibariki mimi kwa ajili ya imani yangu na tamaa yangu ya haki.

Kama wengi wetu, Ibrahimu aliishi katika mazingira ya uovu, bado yeye alitamani kuwa mwenye haki. Rais Dallin H. Oaks alifundisha umuhimu wa kuwa na tamaa za haki: “muhimu kama ilivyo hili ni kuacha kila tamaa ya dhambi, uzima wa milele unahitaji zaidi. Ili kufikia hatima yetu ya milele, tutatamani na kufanyia kazi viwango vinavyohitajika ili kuwa viumbe wa milele. … Kama hili linaonekana kuwa gumu sana—na hakika siyo rahisi kwa kila mmoja wetu—basi tunapaswa kuanza na tamaa ya viwango vya aina hiyo na tumwombe mpendwa Baba wa Mbinguni kwa ajili ya msaada wa hisia zetu hizi [ona Moroni 7:48]” (“Tamaa,” Liahona, Mei 2011, 44–45). Unaposoma Ibrahimu 1:1–19, zingatia jinsi gani mistari hii inaonyesha kile Rais Oaks amefundisha. Maswali kama haya yangeweza kusaidia:

  • Je, Ibrahimu alitamani nini na kutafuta nini? Je, alifanya nini ili kuonyesha imani yake?

  • Je, wewe tamaa zako ni zipi? Je, kuna kitu cho chote unachohisi unapaswa kufanya ili kutakasa tamaa zako?

  • Je, ni changamoto gani Ibrahimu alikabiliana nazo kwa sababu ya tamaa zake za haki? Je, ni kwa jinsi gani Mungu alimsaidia?

  • Je, ni ujumbe gani mistari hii unao kwa ajili ya wale ambao washiriki wa familia zao hawatamani haki?

Ona pia Mathayo 7:7; “Deliverance of Abraham” (video), ChurchofJesusChrist.org; “Educate Your Desires, Elder Andersen Counsels” (ChurchofJesusChrist.org).

Ibrahimu 2:10–11

Je, ni nani amejumuishwa katika agano la Ibrahimu?

Wakati Bwana alipofanya agano na Ibrahimu, Yeye aliahidi kwamba agano hili lingeendelea katika watoto wa Ibrahimu, au “uzao,” na kwamba “kadiri wengi watakavyoipokea injili hii wata … hesabiwa uzao wako” (Ibbrahimu 2:10–11). Hii ina maana kwamba ahadi za agano la Ibrahimu zinatumika kwa waumini wa Kanisa leo, iwe ni wazawa halisi wa Ibrahimu au wameasilliwa katika familia yake kupitia ubatizo na uongofu katika injili ya Yesu Kristo (ona Wagalatia 3:26–29; Mafundisho na Maagano 132:30–32). Kuhesabika kama uzao wa Ibrahimu, mtu lazima atii sheria na ibada za injili.

Mwanzo 12:1–3; 13:15–16; 15:1–6; 17:1–8, 15–22; Mwanzo 2:8–11

Agano la Ibrahimu linanibariki mimi na familia yangu.

Kwa sababu waummini wote wa Kanisa wamejumuishwa katika agano la Ibrahimu, ungeweza kutumia muda fulani ili kutafakari ni kwa nini agano hili lina umuhimu katika maisha yako. Andika mawazo yako kuhusu maswali yafuatayo:

Je, ni kwa jinsi gani ahadi zinazopatikana katika Ibrahimu 2:8–11 zinanibariki mimi na familia yangu? (Ona pia Mwanzo 12:1–3; 13:15–16).

Je, ninajifunza nini kuhusu agano la Ibrahimu kutoka Mwanzo 15:1–6; 17:1–8, 15–22?

Je, ninajisikia kuvutiwa kufanya nini ili kusaidia kutimiza ahadi kwamba “familia zote za duniani zitabarikiwa”? (Ibrahimu 2:11).

Ungeweza kuzingatia kwamba baadhi ya baraka za kidunia zilizoahidiwa kwa Ibrahimu na Sara, kama vile nchi ya ahadi na kuwa wazazi wa watoto wengi, zina mfano wa milele. Hizi zinajumuisha urithi katika ufalme wa selestia (ona Mafundisho na Maagano 132:29) na ndoa ya milele pamoja na kupata watoto milele (ona Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:20–24, 28–32). Ni “hekaluni,” Rais Russell M. Nelson alifundisha, kwamba “tunapokea baraka za msingi, kama uzao wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo” (“The Gathering of Scattered Israel,” Liahona, Nov. 2006, 80).

Ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 15:9–12; 17:3–12 (katika kiambatisho cha Biblia); Kamusi ya Biblia, “Ibrahimu, agano la”; “Mawazo ya Kuweka Akilini: Agano,” katika nyenzo hii.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko Kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mwanzo 13:5–12.Je, Ibrahimu alifanya nini ili kutengeneza amani katika familia yake? Pengine washiriki wa familia yako wangeweza kufanyia mazoezi ya kuwa wapatanishi kama Ibrahimu kwa kuigiza mchezo wa jinsi ya kutatua mizozo ambayo ina uwezekano wa kuibuka katika familia yenu.

Mwanzo 13:16; 15:2–6; 17:15–19.Je ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia familia yako kuelewa ahadi za Bwana katika mistari hii—kwamba ingawa Ibrahimu na Sara walikuwa bado hawajapata watoto, watoto wao wangekuwa wengi kama mavumbi ya nchi, nyota katika anga, au mchanga wa ufukwe wa bahari? (Ona pia Mwanzo 22:17). Pengine ungeweza kuwaonyesha washiriki wa familia chombo chenye mchanga, waangalie nyota, au tumia picha zinazoambatana na muhtasari huu. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuamini katika ahadi za Mungu hata wakati ambapo inaonekana haiwezekani?

Mwanzo 14:18–20.Je, tunajifunza nini kuhusu Melkizedeki kutoka Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:25–40? (katika kiambatisho cha Biblia; ona pia Alma 13:13–19). Je, ni kwa jinsi gani tunaweza “[kukuza] haki” kama Melkizedeki alivyofanya? (mstari wa 36). Je, ni kitu gani kingine kinatuvutia kuhusu huduma ya Melkizedeki?

Picha
Melkizedeki akimbariki Abramu

Melkizedeki Anambariki Abramu, na Walter Rane

Mwanzo 16.Kusoma kuhusu Hajiri kungeweza kuwa fursa ya kujadili jinsi Bwana anavyotusaidia sisi wakati tunapojisikia kukosewa. Unaweza kuelezea kwamba “Ishmaeli” maana yake “Mungu anasikia.” Je, ni lini tulijisikia kuwa Bwana amesikia na ametusaidia wakati tulipoona tumekosewa? (ona Mwanzo 16:11).

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “I Love to See the Temple,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 148.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa mwenye kupatikana na kufikika. “Baadhi ya nyakati nzuri zaidi za kufundisha huanza kama swali au wasiwasi katika moyo wa mshiriki wa familia. Acha washiriki wa familia yako wajue kupitia maneno yako na vitendo kwamba una hamu ya kuwasikiliza. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi,16.)

Picha
Sara anaangalia anga lililo jaa nyota

Mungu aliahidi kwamba watoto wa Ibrahimu na Sara idadi yao ingekuwa “kama nyota za mbinguni” (Mwanzo 22:17). Kutafakari Ahadi za Mungu, na Courtney Matz.

Chapisha