Agano la Kale 2022
Februari 7–13. Mwanzo 12–17; Ibrahimu1–2: “Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Uadilifu”


“Februari 7–13. Mwanzo 12–17; Ibrahimu1–2: ‘Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Uadilifu’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 7–13. “Mwanzo 12–17; Ibrahimu1–2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Ibrahimu na Sara

Mchoro wa Ibrahimu na Sara, na Dilleen Marsh

Februari 7–13

Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2

“Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Uadilifu”

Kumbuka kwamba sio lazima—au hata inawezekana—kuelezea kila kitu kwenye muhtasari huu. Acha Roho akuongoze kwenye kanuni na shughuli ambazo zitakuwa na maana zaidi kwa watoto unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Familia za watoto unaowafundisha zilialikwa kujifunza juu ya Ibrahimu na Sara wiki iliyopita. Wape watoto nafasi ya kushiriki kitu wanachokijua juu ya Ibrahamu au Sara.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Ibrahamu 1:18; 2:8

Yesu Kristo anaweza kuniongoza kwa mkono.

Ibrahimu alitaka kuwa mwenye haki japokuwa washiriki wa familia yake walikuwa waovu. Na Bwana akamwambia, “Nitakuongoza kwa mkono wangu” (Ibrahimu 1:18). Kama vile Mungu alivyoahidi kumsaidia Ibrahimu, anaweza kuwaongoza watoto unaowafundisha wanapotaka kuchagua haki.

Shughuli Yamkini

  • Soma kwa watoto Ibrahimu 1:18 na 2:8, na waalike watoto kusikiliza sehemu ya mwili ambayo inatajwa katika mistari yote miwili. Ingekuwaje kuona Yesu Kristo anatuongoza kwa mkono au kuruhusu mkono Wake utulinde? Shuhudia kwamba Yesu anatuongoza kupitia Roho Wake.

  • Tumia “Ibrahimu na Sara” (katika Hadithi za Agano la Kale) kuwasaidia watoto kuelewa kuwa watu wa karibu na Ibrahimu walikuwa wakifanya mambo mabaya, lakini Ibrahimu alitaka kufanya yaliyo mema na Bwana alimsaidia. Je, Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo hutusaidiaje tunapojaribu kuchagua haki? Imba wimbo unaohusiana na kanuni hii, kama vile “Teach Me to Walk in the Light” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 177).

  • Onyesha picha kadhaa za Mwokozi (ona Kitabu Cha Sanaa ya Injili, na. 38, 3940, na 41), na wasaidie watoto kuona vitu alivyofanya kwa mikono yake. Je, Tunaweza kufanya nini na mikono yetu ili kuwasaidia wengine?

Mwanzo 13:5–12

Ninaweza kuwa mleta amani.

Wakati wachungaji wa Ibrahimu na wachungaji wa Loti hawakukubaliana juu ya malisho yao, Ibrahimu alipendekeza suluhisho ambalo lilileta amani. Unaweza kutumia mfano huu kuhamasisha watoto kuwa waleta amani.

Shughuli Yamkini

  • Shiriki na watoto hadithi kutoka Mwanzo 13:5–12, na waalike waiigize. Acha watoto wachukue zamu kujifanya kuwa Ibrahimu, mpwa wake Loti, na wachungaji. Pendekeza njia ambazo wanaweza kufuata mfano wa Ibrahimu wa kuwa mtu anayetengeneza amani, kama vile kuchukua zamu na mwanasesere wakati wa kucheza na rafiki. Waalike waigize kwa zamu mifano hii.

  • Soma Mathayo 5:9, na elezea kwamba Yesu anataka sisi tuwe waleta amani. Wasaidie watoto wafikirie kile wanachoweza kufanya kuwa watengenezaji wa amani nyumbani au na marafiki. Waalike wachore picha zao wenyewe wakiwa waleta amani. Waombe watoto kushiriki jinsi wanavyohisi wanapokuwa waleta amani kama Yesu Kristo.

Mwanzo 15:1–6; 17:1–8; Ibrahimu 2:9–11

Ni muhimu kutunza ahadi zangu.

Kujifunza juu ya agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu na Sara kunaweza kusaidia watoto kuelewa maana ya kutimiza ahadi. Inaweza pia kuwasaidia kujiandaa kuweka na kutunza maagano.

Shughuli Yamkini

  • Waulize watoto kama wanajua ahadi au maagano ni nini. Waalike kushiriki uzoefu wakati wao walipotoa ahadi au mtu alifanya ahadi kwao. Ikiwa inasaidia, shiriki mifano yako mwenyewe. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Ibrahimu na Sara waliahidi kumtii Mungu. Chagua vifungu vichache kutoka Mwanzo 15:1–6; 17:1–8; Ibrahimu 2:9–11 kushiriki baraka ambazo Mungu aliwaahidi. Hii inaweza kujumuisha “Usiogope, Abramu: Mimi ni ngao yako, ” “Utakuwa baba wa mataifa mengi,” au “Familia zote za dunia zitabarikiwa.”

  • Ni ahadi gani rahisi ambazo watoto wanaweza kufanya na kutunza wakati wa darasa? Kwa mfano, waombe waahidi kukaa katika viti vyao kwa dakika chache au kuweka viti vyao mwishoni mwa darasa. Shiriki nao wakati ambao uliahidi na ukatimiza, na waalike washiriki uzoefu wowote ambao wamepata. Wasaidie kuelewa kwamba watafanya ahadi na Baba wa Mbingu watakapobatizwa na watakapoenda hekaluni.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Ibrahimu 1:12–17

Baba wa Mbinguni husikia na kujibu sala zangu.

Maisha ya Ibrahimu yalipokuwa hatarini, akamwita Mungu na akaokolewa. Watoto unaowafundisha wanaweza kuwa na uzoefu wao wenyewe wa sala wanaoweza kuushiriki.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha Malaika akimuokoa Ibrahimu (ChurchofJesusChrist.org), na waalike watoto kushiriki kile wanachojua juu ya hadithi inayoonyeshwa na picha hii, inayopatikana katika Ibrahimu 1:12, 15–17. Waombe watoto kusoma aya hizi na kushiriki vitu wanavyojifunza juu ya maombi.

  • Waombe watoto kushiriki uzoefu wa wakati Baba wa Mbinguni alijibu sala zao, na kushiriki moja ya uzoefu wako mwenyewe.

Mwanzo 13:5–12

Ninaweza kuwa mleta amani.

Sisi sote tunakabiliwa na hali ambazo zinatujaribu kuwa wenye kufadhaika na wenye ubishi. Fikiria jinsi hadithi ya Ibrahimu na Lutu ingeweza kuwasaidia watoto kuwa wamiliki wa amani katika hali kama hizi.

Shughuli Yamkini

  • Andika Wahusika Wakuu, Mpangilio, Tatizo, na Suluhisho kwenye ubao. Waalike watoto wasome Genesis 13:5–12 na watambue sehemu za hadithi zilizoorodheshwa kwenye ubao. Wasaidie watoto wafikirie hali wakati wanaweza kuwa waleta amani, kama vile wakati mtu anagombana au anajaribu kupigana. Halafu waalike wachukue jukumu la kuigiza jinsi wanavyoweza kuwa waleta amani katika hali hizo.

  • Wasaidie watoto kutafuta mada “Amani” na “Mleta amani” katika Mwongozo wa Maandiko (scriptures.ChurchofJesusChrist.org). Mualike kila mtoto kuchagua andiko juu ya amani na aweze kushiriki kile anachojifunza pamoja na darasa. Wasaidie kufikiria mifano kadhaa ya Mwokozi kuwa mtu wa kuleta amani, kama vile katika Luka 22:50–51. Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaweza kufuata mfano Wake?

    Lutu na Ibrahimu na mifugo

    Chaguo la Lutu, © Providence Collection/licensed from goodsalt.com

Mwanzo 17:1–8; Ibrahimu 2:8–11

Ninaweza kutii maagano ninayofanya na Baba wa Mbinguni.

Kuwafundisha watoto juu ya agano ambalo Mungu aliliweka pamoja na Ibrahimu na Sara kunaweza kuwasaidia kufikiria juu ya maagano yao wenyewe.

Shughuli Yamkini

  • Waaalike watoto kusoma Mwanzo 17:1–8 na Ibrahimu 2:8–11 na andika orodha mbili: kile Ibrahamu alichoombwa kufanya na yale ambayo Bwana alimwahidi kama akitimiza. Je, tunajifunza nini kuhusu Bwana kutoka kwenye mistari hii?

  • Onyesha picha ya mtu akibatizwa (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 103104). Waombe watoto kuorodhesha ahadi ambazo mtu hufanya wakati wa kubatizwa na ahadi ambazo Mungu humuahidi mtu huyo. Pendekeza kwamba watoto wasome katika Mosia 18:10; Mafundisho na Maagano 20:37, 77, 79 kwa msaada. Je, Tunaweza kufanya nini kuweka maagano ambayo tulifanya wakati wa Ubatizo?

ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Tuma ujumbe nyumbani kupitia watoto kuhimiza familia zao kutambua wakati watoto wanapokuwa waleta amani, kutunza ahadi, au kufanya kitu kingine ambacho umekizungumzia darasani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto ni wachangamfu. Wakati mwingine inaweza kuonekana kuwa nguvu nyingi za watoto huwatoa kwenye kujifunza, lakini unaweza kutumia nguvu zao kama sehemu ya kujifunzia. Waalike waigize hadithi au kufanya vitendo vinavyoambatana na maneno katika wimbo au andiko. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 25–26.)