Agano la Kale 2022
Februari 14–20. Mwanzo 18–23: “Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”


“Februari14–20. Mwanzo 18–23: “Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari14–20. Mwanzo 18–23,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Sara amembeba mtoto Isaka

Sara na Isaka, na Scott Snow

Februari14–20

Mwanzo18–23

“Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”

Unapotafuta kukidhi mahitaji ya watoto unaowafundisha, fikiria wazo kwa ajili ya watoto wakubwa na wadogo katika muhtasari huu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuwasaidia watoto kushiriki kile wanachojua tayari kuhusu Mwanzo 18–23, onyesha picha za tukio moja au zaidi kutoka kwenye sura hizi, na uwaombe watoto kushiriki kitu chochote wanachokumbuka juu ya hadithi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mwanzo 18:9–14; 21:1–7

Ninaweza kumuamini Mungu kutimiza ahadi Zake.

Hata hivyo Mungu alikuwa ameahidi kwamba Sara na Ibrahimu watapata mtoto wa kiume, kadiri walivyozeeka, ilionekana kuwa isingewezekana kwamba ahadi hiyo itakamilika. Unawezaje kutumia hadithi hii kusaidia watoto kuwa na imani kwamba Mungu atatimiza ahadi Zake kila wakati?

Shughuli Yamkini

  • Eleza muhtasari wa ahadi ya Mungu kwa Ibrahimu na Sara kwamba watapata mtoto na utimilifu wa ahadi hii (ona Mwanzo 17:15–19; 18:9–14; 21:1–7) Au waalike wenzi katika kata kuvaa kama Ibrahimu na Sara na kuelezea hadithi zao. Wasaidie watoto kuelewa kwamba Ibrahimu na Sara walikuwa wazee sana kuweza kupata watoto. Waulize swali kutoka Mwanzo 18:14, “Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?” Shuhudia kwamba Bwana anaweza kutimiza ahadi zake, hata kama zinaonekana kuwa ngumu.

  • Toa ahadi kwa watoto ambayo utaitimiza mwishoni mwa darasa (kwa mfano, kwamba utawaruhusu kupaka rangi). Muda wote wa darasa, wakumbushe kuhusu ahadi yako, na kisha utimize. Fafanua kuwa Bwana hutunza ahadi zake kila wakati.

  • Waulize watoto kushiriki wakati walilazimika kungojea kitu ambacho wanataka sana. Pamoja na watoto, imba wimbo ambao unathibitisha ahadi za Mungu, kama vile “Keep the Commandments” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 146–47). Wasaidie watoto kutambua vitu ambavyo Mungu ametuahidi ikiwa tutakuwa waaminifu.

  • Onyesha picha ya ubatizo au ya sakramenti (ona kitabu cha sanaa ya injili, na. 103, 104, 107108). Wasaidie watoto kujifunza kuhusu ahadi tunazofanya na Mungu, na kile Mungu anachotuahidi, pale tunapobatizwa na kuchukua sakramenti. (Ona pia True to the Faith, 23–25.)

Mwanzo 22:1–14

Ibrahimu alimtii Bwana.

Ilikuwa ngumu sana kwa Ibrahimu kufuata amri ya kumtoa sadaka mwanawe. Fikiria jinsi unavyoweza kutumia hadithi hii ipasavyo kuwahimiza watoto kumtii Mungu hata kama ni vigumu au hawajui kabisa sababu za amri Zake.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Ibrahimu na Isaka (ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia), na uitumie kuwaambia hadithi ya Ibrahimu na Isaka (ona pia “Ibrahimu na Isaka,” katika Hadithi za Agano la Kale). Onyesha picha ya Yesu Kristo, na ongea na watoto juu ya jinsi hadithi ya Abrahamu na Isaka inaweza kutukumbusha juu ya dhabihu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo waliyoifanya kwetu.

  • Cheza mchezo rahisi ambao unahitaji watoto kufuata uelekeo. Kwa mfano, uelekeo unaweza kuongoza kwenye picha ya Mwokozi iliyofichwa darasani. Ni vitu vipi ambavyo Baba wa Mbinguni ametutaka kufanya? Wasaidie watoto kuelewa kwamba kutii amri Zake kutatusaidia kurudi kuishi Naye na Yesu Kristo tena.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mwanzo 18:9–14; 21:1–7

Bwana hutimiza ahadi Zake, hata wakati inapoonekana kuwa haiwezekani.

Ibrahimu na Sara waliambiwa kwamba wangepata mwana, lakini ilionekana haiwezekani–Ibrahimu alikuwa na miaka 100, na Sara miaka 90 (ona Mwanzo 17:17). Mungu alitimiza ahadi yake, na hadithi hii inaweza kusaidia watoto unaowafundisha kuimarisha imani yao katika ahadi za Mungu kwao.

Shughuli Yamkini

  • Andika kila neno kutoka sentensi ya kwanza ya Mwanzo 18:14 kwenye karatasi tofauti, na mpe kila mtoto moja. Kisha waombe darasa kuweka maneno kwa mpangilio sahihi. Soma Mwanzo 18:9–14; 21:1–7 pamoja na watoto kupata mfano mmoja kutoka kwenye maisha ya Sara na Ibrahimu wakati Bwana alifanya kitu ambacho kilionekana kuwa hakiwezekani. Je, Tunaweza kujifunza nini kutokana na uzoefu wa Sara na Ibrahimu ambao unaweza kutia moyo kutegemea ahadi za Mungu?

  • Onyesha picha za hadithi za maandiko ambamo Mungu alifanya kitu ambacho kilionekana kuwa kisichowezekana au kigumu (kwa mfano, ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 7, 8, 25, 26). Waombe watoto kushiriki kile wanachojua juu ya matukio yaliyoonyeshwa kwenye picha hizi, na uwasaidie kuona jinsi Bwana alitimiza ahadi Zake katika kila mfano. Shiriki jinsi Bwana alivyotunza ahadi zake maishani mwako au katika maisha ya watu unaowajua (kwa mifano kadhaa ya ahadi za Bwana, ona Malaki 3:10; Yohana 14:26–27; Mafundisho na Maagano 89:18–21). Waruhusu watoto washiriki kile wanachokijua.

Mwanzo 19:15–26

Naweza kukimbia uovu.

Simulizi ya Lutu na familia yake wakikimbia mji mwovu linaweza kuhamasisha watoto unaowafundisha kukimbia vishawishi vibaya katika maisha yao.

Picha
Mchoro wa Lutu na familia yake wakikimbia Sodoma na Gomora

Kukimbia Sodoma na Gomora, na Julius Schnorr von Carolsfeld

Shughuli Yamkini

  • Fupisha Mwanzo 19:15–26 na uelezee kwamba familia ya Lutu iliishi katika mji mwovu sana, na malaika wakawaonya waondoke. Someni pamoja mistari ya 15–17, 26, na uwasaidie watoto kufikiria inamaanisha nini kwao “kutoroka” mabaya na “kutazama nyuma” (mistari ya 17).

  • Onyesha picha ya Mwokozi, na uwaombe watoto wachukue hatua zaidi wanaposhiriki kitu kimoja wanachoweza kufanya kukimbia uovu na kuja karibu na Kristo.

  • Jadili hali ambazo rafiki anaweza kuwaalika watoto kufanya kitu ambacho wanajua si sawa. Je, tunawezaje “kukimbia” hali hizi? Je, tunaweza kusema nini kwa rafiki yetu?

Mwanzo 22:1–14

Baba wa mbinguni alimtuma Mwanae, ambaye alijitoa dhabihu kwa ajili yetu.

Unapofundisha juu ya utayari wa Ibrahimu wa kumtoa dhabihu Isaka, uwe mwangalifu na hisia za watoto. Tumia hadithi hii kusaidia watoto kuimarisha upendo wao na kuthamini dhabihu ya Mwokozi.

Shughuli Yamkini

  • Ili kuwasaidia watoto kujifunza hadithi katika Mwanzo 22:1–14, wasomee aya hizo, na waalike kuchora picha za kile unachosoma. Je, Kwa nini amri ya Bwana ya kumtoa dhabihu Isaka ingekuwa ngumu kwa Ibrahimu kuitunza? Tunajifunza nini kuhusu Ibrahimu kwenye hadithi hii?

  • Tumia picha za Ibrahimu na Isaka na ya Kusulibiwa (ona Kitabu Cha Sanaa ya Injili, na. 957) kulinganisha hadithi hii katika Mwanzo 22 na dhabihu ya Mwokozi (ona Mathayo 27:26–37). Je, Tunaweza kujifunza nini juu ya Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo kutoka kwa masimulizi ya Ibrahimu na Isaka na ya Kusulubiwa?

  • Onyesha video “For God So Loved the World” (ChurchofJesusChrist.org), au imba pamoja wimbo kuhusu dhabihu ya Mwokozi, kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35). Alika watoto wazungumze kuhusu dhabihu ya Yesu inavyoonyesha upendo wa Baba wa Mbinguni kwetu.

Picha
learning icon

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kushiriki na familia zao kuhusu wakati ambao Mungu aliwabariki walipotii mojawapo ya amri.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Himiza unyenyekevu. Kama inahitajika wakati wa darasa, unaweza kuwakumbusha watoto kuwa wanyenyekevu. Unaweza kufanya hivyo kwa kuimba kimya kimya au kutikisa wimbo au kwa kuonyesha picha ya Yesu.

Chapisha