Agano la Kale 2022
Februari 14-20. Mwanzo 18–23: “Je, kuna Kitu Cho chote Kilicho Kigumu kwa Bwana?”


“Februari 14–20. Mwanzo 18–23: ‘Je, Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 14–20. Mwanzo 18-23,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Sara amembeba mtoto Isaka

Sara na Isaka, na Scott Snow

Februari 14–20

Mwanzo 18–23

“Je, Kuna Kitu Chochote Kilicho Kigumu Kwa Bwana?”

Soma na kutafakari Mwanzo 18–23, na uandike misukumo yako. Unaweza kutumia mawazo kutoka katika muhtasari huu ili kukusaidia ujifunze milango hii, na pia unaweza kuvutiwa kupekua ujumbe mwingine katika maandiko ambao Bwana anao maalumu kwa ajili yako.

Andika Misukumo Yako

Maisha ya Ibrahimu, yalijaa matukio yenye kuvunja moyo na ya kufurahisha, ni ushahidi wa ukweli kwamba Ibrahimu alijifunza katika ono—kwamba tuko duniani ili kujaribiwa, “ili kuona kama [sisi] tutafanya mambo yote ambayo Bwana Mungu [wetu] atatuamuru” (Ibrahimu 3:25). Je, Ibrahimu mwenyewe angethibitisha kuwa yeye ni mwaminifu? Je, angeendelea kuwa na imani katika ahadi ya Mungu ya kuwa na watoto wengi, hata wakati yeye na Sara katika umri wao wa uzee bado hawakuwa na watoto? Na mara Isaka alipozaliwa, je, Ibrahimu angastahimili lisilofikirika—amri ya kumtoa dhabihu mwana huyo wa pekee ambaye kupitia yeye Mungu aliahidi kutimiza agano lile? Ibrahimu alithibitisha yu mwaaminifu. Ibrahimu alimwamini Mungu, na Mungu alimwamini Ibrahimu. Katika Mwanzo 18–23, tunapata hadithi kutoka katika maisha ya Ibrahimu na wengine ambazo zinaweza kutushawishi sisi kufikiria kuhusu uwezo wetu wenyewe wa kuamini ahadi za Mungu, kuukimbia uovu na kamwe tusiangalie nyuma, na kumwamini Mungu pasipo kujali dhabihu tutakayoitoa.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mwanzo 18:9–14; 21:1–7

Bwana anatimiza ahadi Zake katika wakati Wake mwenyewe.

Bwanna amefanya ahadi tukufu kwa walio waaminifu, lakini nyakati zingine hali katika maisha yetu zinaweza kusababisha sisi kujiuliza jinsi gani ahadi hizo zinawezekana kutimia. Ibrahimu na Sara yawezekana nao walijisikia hivyo nyakati zingine. Je, unajifunza nini kutokana na uzoefu wao? Inaweza kuwa vyema kuanza kujifunza kwa kurejelea kile ambacho Bwana alimuahidi Ibrahimu katika Mwanzo 17:4, 15–22. Je, ni jinsi gani Ibrahimu na Sara waliipokea ahadi? (Ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 17:23 [katika Mwanzo 17:17, tanbihi b]; Mwanzo 18:9–12). Je, ni kwa jinsi gani Bwana alijibu ili kuwasaidia wao kuwa na imani kubwa zaidi katika ahadi Zake? (ona Mwanzo 18:14).

Je, wewe unapata nini katika mistari hii ambacho kinajenga imani yako? Je, ni matukio gani mengine—katika maisha yako au ya mtu mwingine—yameimarisha imani yako kwamba Bwana atatimiza ahadi Zake kwako katika wakati Wake na kwa njia Yake mwenyewe?

Ona pia Mafundisho na Maagano 88:68.

Mwanzo 19:12–29

Bwana anatuamuru tuukimbie uovu.

Je, ni masomo gani tunajifunza kuhusu kuukimbia uovu unaposoma kuhusu Lutu na familia yake? Kwa mfano, ni kitu gani kinachokuvutia kuhusu kile malaika walichosema na kufanya ili kumsaidia Lutu na familia yake kuepuka kuangamia? (Ona Mwanzo 19:12–17). Je, ni kwa jinsi gani Bwana anakusaidia wewe na familia yako kukimbia na kutafuta ulinzi kutokana na vishawishi viovu katika ulimwengu?

Kwa nyongeza kuhusu dhambi za Sodoma na Gomora, ona Ezekieli 16:49–50 na Yuda 1:7–8.

Ona pia Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 19:9-15 (katika Kiambatisho cha Biblia).

Picha
Kielelezo cha Loti na familia yake wakikimbia kutoka Sodoma na Gomora

Kuikimbia Sodoma na Gomora, na Julius Schnorr von Carolsfeld

Mwanzo 19:26

Je,ni kitu gani kibaya alichofanya mke wa Lutu?

Mzee Jeffrey R. Holland alifundisha:

“Ni dhahiri kabisa, kilichokuwa kibaya kwa mke wa Lutu kilikuwa ni kwamba si tu alikuwa anaangalia nyuma; katika moyo wake alitaka kurudi nyuma. Ilionekana kwamba hata kabla yeye hajavuka mipaka ya mji ule, yeye tayari alikuwa anakikosa kile ambacho Sodoma na Gomora kilikuwa kikimpatia. … Hakuwa na imani. Alitilia mashaka uwezo wa Mungu wa kumpa yeye kilicho bora zaidi ya kile ambacho tayari alikuwa nacho. …

“Kwa [watu] wote wa kila kizazi, ninakuombeni, ‘Mkumbukeni mke wa Lutu’ [Luka 17:32]. Imani ni kwa ajili ya wakati ujao. Imani hujenga juu ya yaliyopita lakini kamwe haitamani kukaa hapo. Imani hutumaini kwamba Mungu ana mambo makuu ghalani kwa ajili ya kila mmoja wetu na kwamba hakika Kristo ni ‘kuhani mkuu wa mambo mema yajayo’ (Waebrania 9:11)” (“Yaliyo Bora Bado Hayajakuwa,” Ensign, Jan. 2010, 24, 27).

Mwanzo 22:1–19

Utayari wa Ibrahimu wa kumtoa dhabihu Isaka ni mfano wa Mungu na Mwanawe.

Sisi hatujui sababu zote za Mungu kumwamuru Ibrahimu kumtoa Isaka kama dhabihu; tunajua ilikuwa ni jaribio la imani yake kwa Mungu (ona Mwanzo 22:12–19). Unaposoma Mwanzo 22:1–19, unajifunza nini kutokana na kitendo hiki cha Ibrahimu?

Utayari wa Ibrahimu wa kumtoa dhabihu mwanawe kilikuwa “mfano wa Mungu na Mwanawe wa Pekee” (Yakobo 4:5). Unapotafakari mfanano huu kati ya jaribio la Ibrahimu na Mungu Baba kumtoa Mwanawe kama dhabihu kwa ajili yetu sisi, je, wewe unajisikiaje juu ya Baba yako wa Mbinguni?

Kuna mfanano pia kati ya Isaka na Mwokozi. Zingatia kusoma Mwanzo 22:1–19 tena, mkitafuta mifanano hiyo.

Ona pia “Akedah (The Binding)” (video), ChurchofJesusChrist.org.

Picha
family study icon

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mwanzo 18:14.Je, kuna hadithi katika maandiko, kutoka katika historia ya familia yako, au kutoka katika maisha yako mwenyewe unayoweza kusimulia ambayo imekufundisha kwamba hakuna kitu kigumu kwa Bwana?

Mwanzo 18:16–33.Je, tunajifunza nini kuhusu tabia za Ibrahimu kutoka kwenye mistari hii? Je, sisi tunawezaje kufuata mfano wake? (Ona pia Alma 10:22–23.)

Mwanzo 19:15–17.Mistari hii inaweza kusaidia washiriki wa familia yako kujitayarisha kwa ajili ya nyakati ambapo watahitajika kukimbia hali za uovu. Je, baadhi ya hali hizi zinaweza kuwa za aina gani? Kwa mfano, unaweza kuwa na majadiliano kuhusu vyombo vya habari visivyo sahihi au jaribio la kusengenya. Je, tunawezaje kukimbia kutoka kwenye hali kama hizo?

Mwanzo 21:9–20.Je, ni kitu gani kinaivutia familia yako kuhusu njia ambayo Mungu alimtendea Hajiri na Ishmaeli baada ya Sara na Ibrahimu kuwafukuza?

Mwanzo 22:1–14.Je, ni kwa jinsi gani unaweza kuisaidia familia yako kuona muunganiko kati ya hadithi ya Mungu kumwamuru Ibrahimu kumtoa dhabihu Isaka na ile dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi? Unaweza kuonyesha picha ya Ibrahimu na Isaka na ile ya Kusulubishwa (ona “Ibrahimu na Isaka,” katika Hadithi za Agano la Kale) wakati washiriki wa familia wakijadili mifanano wanayoiona kati ya matukio haya. Mngeweza pia kuimba wimbo kuhusu dhabihu ya Mwokozi, kama vile “He Sent His Son” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 34–35), na kutafuta vifungu vya maneno ambavyo vinaelezea dhabihu ya Mwokozi.

Je, sisi tumeagizwa kutoa dhabihu gani kama familia? Je, ni kwa jinsi gani dhabihu hizi zimetuleta karibu zaidi na Mungu?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “God Loved Us, So He Sent His Son,” Nyimbo za Kanisa , na. 187.

Kuboresha Kujifunza Binafsi

Msikilize Roho. Unapojifunza, kuwa makini na mawazo na hisia zako, hata kama zinaonekana havihusiani na kile unachokisoma. Mawazo hayo yanaweza kuwa ndiyo mambo hasa Mungu anayokutaka uyajue.

Picha
Ibrahimu na Isaka wanatembea

Kielelezo cha Ibrahimu na Isaka, na Jeff Ward

Chapisha