Agano la Kale 2022
Mawazo ya Kuweka Akilini: Agano


“Mawazo ya Kuweka Akilini: Agano,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Mawazo ya Kuweka Akilini: Agano,” Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

ikoni ya mawazo

Mawazo ya Kuweka Akilini

Agano

Kote katika Agano la Kale, mara kwa mara utasoma neno agano. Leo kwa kawaida tunafikiria juu ya agano kama ahadi takatifu za Mungu, lakini katika ulimwengu wa kale, maagano yalikuwa pia ni sehemu muhimu ya maingiliano baina ya watu. Kwa ajili ya usalama na kupona kwao, watu walihitaji kuweza kuaminiana, na maagano yalikuwa ndiyo njia ya kupata kuaminiana huko.

Hivyo wakati Mungu aliponena na Nuhu, Ibrahimu, au Musa kuhusu maagano, Yeye alikuwa akiwaalika wao kuingia katika uhusiano wa kuaminiana na Yeye. Moja ya mifano bora ya agano katika Agano la Kale ni lile moja ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu na Sara—na kisha likafanywa upya na wazao wao Isaka na Yakobo (pia anaitwa Israeli). Mara nyingi tunaita hilo kama agano la Ibrahimu, ingawa katika Agano la Kale lilikuwa likijulikana tu kama “agano.” Utaona kwamba Agano la Kale kimsingi ni hadithi za watu ambao walijiona wenyewe kama warithi wa agano hili—watu wa agano.

Agano la Ibrahimu linaendelea kuwa muhimu leo, hususani kwa Watakatifu wa Siku za Mwisho. Kwa nini? Kwa sababu sisi pia ni watu wa agano, iwe au tusiwe wazawa halisi wa moja kwa moja wa Ibrahimu, Isaka, na Yakobo (ona Wagalatia 3:27–29). Kwa sababu hii, ni muhimu kuelewa agano la Ibrahimu ni nini na linatumikaje kwetu sisi leo.

Je, ni nani amejumuishwa katika agano la Ibrahimu?

Ibrahimu alitaka “kuwa mfuasi mkubwa wa haki” (Ibrahimu1:2), hivyo Mungu alimwalika katika uhusiano wa agano. Ibrahimu hakuwa wa kwanza kuwa na tamaa hii, na hakuwa wa kwanza kupokea agano. Yeye alitafuta “baraka za mababu” (Ibrahimu 1:2)—baraka ambazo zilitolewa kwa agano kwa Adamu na Hawa na baada ya hapo kwa wale walio zitafuta baraka hizo kwa bidii.

Agano la Mungu kwa Ibrahimu alimwahidi baraka za kupendeza: urithi wa nchi, watoto wengi, kupatikana kwa ibada za ukuhani, na jina ambalo litaheshimiwa na vizazi vingi vijavyo. Lakini mtazamo wa agano hili haukuwa tu juu ya baraka ambazo Ibrahimu na familia yake wangepokea bali pia baraka ambayo wao wangekuwa kwa watoto wote wa Mungu. “Nawe uwe baraka,” Mungu alitamka, “na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa” (Mwanzo 12:2–3).

Je, agano hili lilimpa Ibrahimu , Sara, na wazao wao hadhi ya upendeleo miongoni mwa watoto wa Mungu? Ni katika mtazamo tu kwamba ni heshima ya kuwabariki wengine. Familia ya Ibrahimu ilikuwa “ibebe huduma hii na Ukuhani kwa mataifa yote,” kutoa “baraka za injili, ambazo ni baraka za wokovu, hata za uzima wa milele” (Ibrahimu 2:9, 11).

Agano hili ndiyo baraka ambayo Ibrahimu alikuwa akitamani. Baada ya kupokea, Ibrahimu alijisemea moyoni mwake, “Mtumishi wako amekutafuta kwa dhati; sasa nimekupata” (Ibrahimu 2:12).

Hiyo ilikuwa maelfu ya miaka iliyopita, lakini agano hili limerejeshwa katika siku yetu (ona 1 Nefi 22:8–12). Na kwa sasa inatimizwa katika maisha ya watu wa Mungu. Kwa kweli, kutimia kwa agano kunaongezeka kasi katika siku hizi za mwisho wakati kazi ya Mungu inapoendelea, kubariki familia ulimwenguni kote. Na kila mmoja ambaye, kama Ibrahimu, anapotaka kuwa mfuasi mkubwa wa haki, kila mmoja anaye mtafuta Bwana kwa dhati, anaweza kuwa sehemu ya hili.

familia mbele ya hekalu

Je, Agano la Ibrahimu lina maana gani kwangu mimi?

Wewe ni mtoto wa ahadi. Ulifanya agano na Mungu wakati ulipobatizwa. Unafanya upya agano hilo kila unapokula sakramenti. Na unafanya maagano matakatifu hekaluni. Kwa pamoja, maagano haya yanakufanya wewe kuwa mshiriki katika agano la Ibrahimu, ambapo utimilifu wake unapatikana katika ibada za hekaluni. Kama Rais Russell M. Nelson alivyofundisha, “Hatimaye, katika hekalu takatifu, tunaweza kuja kuwa warithi wa pamoja wa baraka za familia ya milele, kama wakati mmoja ilivyo ahidiwa kwa Ibrahimu, Isaka, Yakobo na wazao wao.”1

Kupitia maagano na ibada hizi, sisi tunakuwa watu wa Mungu (ona Kutoka 6:7; Kumbukumbu la Torati 7:6; 26:18; Ezekieli 11:20). Tunakuwa tofauti na ulimwengu unaotuzunguka. Maagano yetu yanafanya iwezekane kwetu sisi kuwa wakweli, wafuasi waaminifu wa Yesu Kristo. “Maagano yetu,” Rais Nelson alielezea, “yanatufunga sisi Kwake na yanatupatia nguvu za kiungu.”2 Na Mungu anapobariki watu Wake kwa nguvu Zake, ni kwa mwaliko na matarajio kwamba nao watawabariki wengine—kwamba “watakuwa baraka” kwa “familia zote za dunia” (Ibrahimu 2:9, 11).

Huu ndio ufahamu wa thamani uliotolewa kwetu kwa sababu ya urejesho wa agano la Ibrahimu kupitia Nabii Joseph Smith. Hivyo basi unaposoma kuhusu maagano katika Agano la Kale, usifikiri tu kuhusu uhusiano baina ya Mungu na Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Fikiria pia kuhusu uhusiano Wake na wewe. Wakati unaposoma kuhusu ahadi ya watoto wasio na idadi (ona Mwanzo 28:14), usifikiri tu kuhusu mamilioni ambao leo wanamwita Ibrahimu baba yao. Fikiria pia kuhusu ahadi za Mungu kwako wewe juu ya familia ya milele na ongezeko la milele (ona Mafundisho na Maagano 131:1–4; 132:20–24). Wakati unaposoma kuhusu ahadi ya nchi ya urithi, usifikirie tu kuhusu nchi ya ahadi kwa Ibrahimu. Fikiria pia kuhusu hatima ya kiselestia kwa dunia yenyewe—urithi ulio ahidiwa kwa “wapole” ambao “wanamngojea Bwana” (Mathayo 5:5; Zaburi 37:9, 11; ona pia Mafundisho na Maagano 88:17–20). Na wakati unaposoma kuhusu ahadi kwamba watu wa Mungu wa agano watabariki “familia zote za dunia” (Ibrahimu 2:11), usifikirie tu kuhusu huduma ya Ibrahimu au manabii waliozaliwa kutokana na yeye. Fikiria pia kuhusu wewe unaweza kufanya nini—kama mfuasi wa agano wa Yesu Kristo—kuwa baraka kwa familia zinazokuzunguka.