Agano la Kale 2022
Februari 21-27. Mwanzo 24–27: Agano Limefanywa Upya


“Februari 21-27. Mwanzo 24–27: Agano Limefanywa Upya,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 21-27. Mwanzo 24–27,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia: 2022

Picha
Rebeka

Kielelezo cha Rebeka na Dilleen Marsh

Februari 21-27

Mwanzo 24–27

Agano Limefanywa Upya

Unaposoma Mwanzo 24–27, kuwa makini na utambuzi wa kiroho unaopokea. Omba ili kujua jinsi gani kanuni unazopata zinahusika katika maisha yako.

Andika Misukumo Yako

Agano la Mungu na Ibrahimu linajumuisha ahadi kwamba kupitia Ibrahimu na watoto wake “familia zote za ulimwengu zitabarikiwa” (Ibrahimu 2:11). Hiyo siyo ahadi ambayo inaweza kutimia katika kizazi kimoja: katika njia nyingi, Biblia ni hadithi ya Mungu akiendelea kutimiza ahadi Zake. Na alianza kwa kufanya upya agano na familia ya Isaka na Rebeka. Kupitia uzoefu wao, sisi tunajifunza kitu kuhusu kuwa sehemu ya agano hilo. Mifano yao inatufundisha kuhusu ukarimu, uvumilivu, na kuamini katika baraka zilizoahidiwa na Mungu. Na tunajifunza kwamba inastahili kuacha “chakula chekundu” cho chote cha ulimwenguni (Mwanzo 25:30) ili kupata baraka za Mungu kwa ajili yetu na watoto wetu kwa vizazi vingi vijavyo.

Picha
ikoni ya kujifunza binafsi

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Binafsi Maandiko

Mwanzo 24

Ndoa ni muhimu kwa mpango wa milele wa Mungu.

Leo watu wengi wanafanya ndoa kipaumbele cha chini au hata kufikiria kama ni mzigo. Ibrahimu alikuwa na mtazamo tofauti—kwake yeye, ndoa ya mwanawe Isaka ilikuwa na umuhimu wa hali ya juu kabisa. Je, ni kwa nini unafikiri ilikuwa muhimu sana kwake? Unaposoma Mwanzo 24, fikiria kuhusu umuhimu wa ndoa katika mpango wa Mungu wa wokovu. Unaweza pia kusoma ujumbe wa Mzee D. Todd Christofferson “Kwa Nini Ndoa, Kwa Nini Familia” (Liahona, Mei 2015, 50–53) na fikiria kwa nini “familia iliyojengwa juu ya ndoa ya mwanamume na mwanamke inatoa mfumo ulio bora kwa ajili ya kufanikiwa kwa mpango wa Mungu” (ukurasa wa 52).

Maswali kama yafuatayo yanaweza kukusaidia kufikiria kanuni zingine muhimu katika mlango huu:

Mwanzo 24:1-14. Je, Ibrahimu na mtumishi wake walifanya nini ili kumshirikisha Bwana katika jitihada zao za kumtafuta mke kwa ajili ya Isaka?

Mwanzo 24:15–28, 55–60. Je, ni sifa gani unazipata katika Rebeka ambazo ungetaka kuiga?

Je, ni utambuzi gani mwingine unaoupata?

Ona pia Mafundisho na Maagano 131:1–4; “Familia: Tangazo kwa Ulimwengu,” ChurchofJesusChrist.org.

Mwanzo 25:29-34

Ninaweza kuchagua kati ya kutosheka kwa mara moja na mambo yenye thamani kubwa zaidi.

Katika utamaduni wa Ibrahimu, mtoto wa kiume aliye mkubwa zaidi katika familia kwa kawaida hupokea nafasi ya uongozi na heshima, inayoitwa haki ya uzaliwa wa kwanza. Mwana huyu alipokea urithi mkubwa zaidi kutoka kwa wazazi wake, sambamba na majukumu makubwa zaidi kwa ajili ya kutunza familia yote.

Unaposoma Mwanzo 25:29–34, fikiria ni kwa nini yawezekana Esau alikuwa tayari kutoa haki yake ya kuzaliwa kwa kubadilishana na chakula. Je, ni masomo gani unapata kwa ajili yako katika hadithi hii? Kwa mfano, kuna “chakula chekundu” chochote ambacho kinakuvuruga wewe uache baraka ambazo zina thamani zaidi kwako wewe? Je, unaafanya nini ili kufokasi juu ya baraka na kutoa shukrani kwa baraka hizi?

Ona pia Mathayo 6:19–33; 2 Nefi 9:51; M. Russell Ballard, “What Matters Most Is What Lasts Longest,” Liahona, Nov. 2005, 41–44.

Mwanzo 26:1-5

Agano la Ibrahimu lilifanywa upya kupitia kwa Isaka.

Agano ambalo Mungu alifanya na Ibrahimu lilikusudiwa kuendelea kupitia vizazi vingi, hivyo urithi wa Ibrahimu na Sara wa kushika maagano ungehitaji kutolewa kwa Isaka, Yakobo na walio waaminifu wengine wanawake na wanaume miongoni mwa watoto wao. Unaposoma Mwanzo 26:1–5, angalia baadhi ya baraka za agano ambazo Mungu alizitaja. Je, unajifunza nini kuhusu Mungu kutokana na mistari hii?

Mwanzo 26:18–25, 32–33

Yesu Kristo ni kisima cha maji ya uzima.

Unaweza kuona kwamba kisima na chemchemi na vyanzo vingine vya maji vinashika nafasi muhimu katika hadithi nyingi za Agano la Kale. Hii siyo ya kushangaza, kwa sababu nyingi ya hadithi hizi zilitokea katika sehemu kame sana. Unaposoma katika Mwanzo 26 kuhusu kisima cha Isaka, je, maji yanaweza kuwa alama ya nini katika maandiko. Je, ni utambuzi gani unaopata kuhusu visima vya kiroho vya “maji ya uzima”? (ona Yohana 4:10–15). Je, ni kwa jinsi gani wewe unachimba visima vya kiroho katika maisha yako? Je, ni kwa jinsi gani Mwokozi ni kama maji ya uzima kwako wewe? Kumbuka kwamba Wafilisti “walizuia” visima (ona Mwanzo 26:18). Je kuna kitu chochote katika maisha yako ambacho kinazuia visima vyako vya maji ya uzima?

Picha
kisima cha zamani

Kisima katika Ber-sheba ya kale, mahali ambapo Ibrahimu na Isaka walichimba visima.

Mwanzo 27

Je, Rebeka na Yakobo walikosea kumdanganya Isaka?

Sisi hatujui sababu walizotumia Rebeka na Yakobo kumwendea ili kupata baraka kwa ajili ya Yakobo. Inasaidia kukumbuka kwamba Agano la Kale kama tulilo nalo leo halijakamilika (ona Musa 1:23, 41). Hapo yawezekana kuna taarifa inakosekana kutoka kwenye kumbukumbu za mwanzoni ambayo ingeelezea kile kinachoonekana cha kutatiza kwetu. Hata hivyo, tunajua kwamba yalikuwa mapenzi ya Mungu kwa Yakobo kupokea baraka kutoka kwa Isaka kwa sababu Rebeka alipata ufunuo kwamba ilimpasaYakobo kumtawala Esau (ona Mwwanzo 25:23). Baada ya Isaka kutambua kuwa amembariki Yakobo badala ya Esau, alithibitisha kwamba Yakobo “atabarikiwa” (Mwanzo 27:33)—akimaanisha kwamba mapenzi ya Mungu yametimia.

Picha
ikoni ya kujifunza kama familia

Mawazo kwa ajili ya Kujifunza Maandiko kama Familia na Jioni ya Nyumbani

Mwanzo 24:2–4, 32–48.Ibrahimu akimwagiza mtumishi aliyeaminika kumtafuta mke kwa ajili ya Isaka, na mtumishi yule akaagana na Ibrahimu kwamba angefanya hivyo. Je, ni kwa jinsi gani mtumishi yule alionyesha uaminifu katika kushika agano lake? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kufuata mfano wake?

Mwanzo 24:15–28, 55–60.Familia yako inaweza kuangalia katika mistari hii kwa ajili ya kuona sifa ambazo zilimfanya Rebeka kuwa mwenza mstahiki wa Isaka Wahimize wanafamilia kuchagua moja ya sifa hizi ambayo wanaonelea kuwa wanapaswa kuikuza.

Mwanzo 25:19–3427.Ili kurejelea hadithi ya jinsi haki ya uzaliwa wa kwanza na baraka ya Esau ilivyokuja kwa Yakobo, ungeweza kuandika sentensi kutoka “Yakobo na Esau” (katika Hadithi za Agano la Kale) kwenye vipande tofauti vya karatasi. Washiriki wa familia wangeweza kufanya kazi pamoja ya kuweka sentensi katika mpangilio sahihi.

Unapojadili kuhusu Esau kuuza haki yake ya uzaliwa wa kwanza, mnaweza pia kuongelea kuhusu kitu cha muhimu zaidi kwa familia yenu, kama vile uhusiano wenu na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Pengine washiriki wa familia wangeweza kupata vitu au picha ambazo zinawakilisha kitu wanachofikiri kuwa kina thamani ya milele. Acha waelezee ni kwa nini wao wamechagua vitu hivyo.

Mwanzo 26:3–5.Ili kuisaidia familia yako kuelewa agano la Ibrahimu, ungeweza kuwaalika kutafuta ahadi zilizoelezwa katika mistari hii. Kwa nini ni muhimu kwetu sisi kujua kuhusu ahadi hizi leo? (ona “Mawazo ya Kuweka Akilini: Agano,” katika nyenzo hii).

Mwanzo 26:18–25, 32–33.Kwa nini visima ni muhimu? Ni kwa njia gani Yesu Kristo ni kama kisima cha maji?

Kwa mawazo zaidi kwa ajili ya kuwafundisha watoto, ona muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa ajili ya Msingi.

Wimbo uliopendekezwa: “Choose the Right,” Nyimbo za Kanisa, na. 239.

Kuboresha Kujifunza binafsi

Kariri andiko. Mzee Richard G. Scott alifundisha, “Andiko takatifu lililokaririwa linakuwa rafiki mvumilivu ambaye hadhoofishwi na muda kupita” (“The Power of Scripture,” Ensign au Liahona, Nov. 2011,6).

Picha
Esau na Yakobo

Esau Anauza Haki Yake ya Uzaliwa wa Kwanza kwa Yakobo, na Glen S. Hopkinson

Chapisha