Agano la Kale 2022
Februari 21–27. Mwanzo 24–27:Agano Lafanywa Upya


“Februari 21–27. Mwanzo 24-27; Agano Lafanywa Upya’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 21–27. Mwanzo 24–27,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Rebeka

Mchoroo wa Rebeka, na Dilleen Marsh

Februari 21–27

Mwanzo 24–27

Agano Lafanywa Upya

Unaposoma Mwanzo 24–27 na kujitayarisha kufundisha, fikiria juu ya watoto darasani mwako. Ni nini wanahitaji kujifunza? Ni ipi kati ya shughuli hizi ambayo itakuwa na maana kwao? Kulingana na mahitaji yao, unaweza kuchukua shughuli zozote zilizojumuishwa hapa au zile zinazopatikana katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia..

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Chini ya kiti cha kila mtoto, weka swali kuhusu tukio au kanuni katika Mwanzo 24–27. Acha watoto wajibu maswali ikiwa wanaweza, au waalike wasikilize majibu wakati wa somo.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mwanzo 24:10–21

Naweza Kuwa Mkarimu kwa wengine.

Mtumishi wa Ibrahimu alifurahishwa na fadhili nzuri ambayo Rebeka alimuonyesha kwa kumpa maji sio yeye tu bali pia na ngamia zake 10. Mfano wake unaweza kuwa ukumbusho kwa watoto daima kuwa na fadhili kwa wengine.

Picha
kisima cha zamani

Kisima katika Beer-sheba ya zamani, ambapo Ibrahimu na Isaka walichimba visima.

Shughuli Yamkini

  • Onyesha picha ya Rebeka katika ukurasa wa shughuli wa wiki hii. Toa maelezo katika picha unapofupisha hadithi kwenye Mwanzo 24:10–21, ambamo Rebeka alimwonyesha fadhili mtumishi wa Ibrahimu. Eleza kwamba maneno yake na kitendo chake cha fadhili ndio ishara kwamba Rebeka alikuwa mtu ambaye Mungu alitaka aolewe na Isaka mwana wa Ibrahimu . Waalike watoto kujifanya kama mtumishi anayefika na ngamia wake au Rebeka akichukua maji kwa ajili yao. Wape vifungu vya kusoma kutoka kwenye maandiko, kama vile “Acha … ninywe maji kidogo” (mstari wa 17) na “Nitachota maji kwa ajili ya ngamia zako pia” (mstari wa 19). Kwa nini ni muhimu kwetu kuwa wema kwa wengine?

  • Simulia hadithi kuhusu jinsi Mwokozi alivyoonyesha fadhili kwa mtu. Waalike baadhi ya watoto kushiriki uzoefu wao wenyewe wa kuonyesha fadhili.

  • Pendekeza hali kadhaa ambazo mtoto anaweza kuonyesha fadhili, kama vile kucheza na marafiki au kukutana na mtu mpya shuleni. Waulize watoto nini wanaweza kufanya ili kuwa na fadhili katika hali hizi.

  • Imba na watoto wimbo juu ya fadhili, kama vile“Kindness Begins with Me” au “I’m Trying to Be like Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto 145, 78–79). Waalike watoto wasikilize neno “fadhili” (au neno linalofanana) na wasimame wanaposikia. Tunawezaje kuonyeshaje fadhili kwa wengine? Ukurasa wa shughuli wa wiki hii unaweza kusaidia majadiliano haya.

Mwanzo 25:29–34

Ninaweza kuchagua vitu ambavyo ni muhimu sana.

Kwa sababu Esau alikuwa mtoto mkubwa katika familia yake, alitakiwa kupata majukumu na haki maalum, iitwayo haki ya mzaliwa wa kwanza. Siku moja wakati Esau alipokuwa na njaa, aliuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa mdogo wake, Yakobo, kwa chakula. Hadithi hii inaweza kuwafundisha watoto kwamba tunapaswa kuchagua vitu vya kudumu kuliko kuridhika kwa muda mfupi.

Shughuli Yamkini

  • Leta darasani vitu kadhaa ambavyo vinaweza kusaidia kuelezea hadithi ya Esau kuuza haki yake ya kuzaliwa, kama vile bakuli na picha ya mtu anayepata baraka ya ukuhani. Waalike watoto watumie vitu wanapokuambia kile wanachojua juu ya hadithi. “Yakobo and Esau” (katika Hadithi za Agano la Kale) inaweza kusaidia. Someni pamoja Mwanzo 25:34, na eleza kwamba mtu yeyote ambaye alikuwa na haki ya kuzaliwa atakuwa na upendeleo na majukumu maalum ya kutunza familia yote.

  • Onyesha watoto picha mbili: moja ya kitu cha thamani kubwa ya kiroho (kama hekalu) na moja ya kitu ambacho huleta tu furaha ya muda mfupi (kama mchezo, mwanasesere, au pipi). Waombe wachague ni kipi kitakachotusaidia kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni. Rudia hili kwa kutumia picha zingine.

  • Imbeni wimbo kuhusu kufanya maamuzi sahihi, kama vile “Choose the Right Way” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 160–61) na watoto. Shuhudia kwamba tumebarikiwa na tunafurahi wakati tunapochagua haki.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mwanzo 24:1–28

Nitabarikiwa ninapotenda kwa imani na kuonyesha fadhili kwa wengine.

Mtumishi wa Ibrahimu alionyesha imani kwa kuamini mwongozo wa Mungu wa kutafuta mke kwa ajili ya Isaka. Rebeka alionyesha fadhili jinsi alivyomtendea mtumishi wa Ibrahimu. Unawezaje kuwasaidia watoto unaowafundisha kufuata mifano ya mtumishi wa Ibrahimu na Rebeka?

Shughuli Yamkini

  • Someni Mwanzo 24:1–28 pamoja, na uwasaidie watoto kutambua mifano ya imani na fadhili (tazama, kwa mfano, mistari ya 12–14 na 17–20). Je, mtumishi wa Ibrahimu na Rebeka walibarikiwaje kwa kuonyesha imani na fadhili? Andika ubaoni tunaweza kuonyesha imani kwa… na Tunaweza kuonyesha wema kwa… , na waombe watoto kupendekeza njia za kukamilisha sentensi hizi.

  • Kwenye karatasi, andika vitu ambavyo mtumishi wa Ibrahimu alisema au alifanya na mambo ambayo Rebeka alisema au alifanya katika Mwanzo 24:1–28. Waalike watoto kwa kila mmoja kuchagua kipande cha karatasi na kwa pamoja kubashiri ni nani aliyesema au alifanya vitu hivi (wanaweza kurejelea kwenye maandiko ikiwa wanahitaji msaada). Hadithi hii inatufundisha nini kuhusu fadhili? Inatufundisha nini sisi kuhusu imani? Mifano mingine ya fadhili na imani inapatikana katika Mwanzo 24:29–33, 58–61.

  • Waalike watoto wafikirie tendo la fadhili ambalo wameliona. Waalike kuandika na kushiriki pamoja na darasa au familia zao nyumbani. Tunajisikiaje mtu akiwa mwema kwetu?

Mwanzo 25:21–34

Nitathamini vitu vya milele badala ya vitu vya kidunia.

Esau alichagua kuuza kitu cha thamani kubwa, haki yake ya kuzaliwa, kwa kitu cha chini, mkate na bakuli la supu. Unaposoma aya hizi, fikiria jinsi unavyoweza kusaidia watoto kutayarisha vitu ambavyo ni vya milele.

Shughuli Yamkini

  • Soma pamoja hadithi ya Yakobo na Esau katika Mwanzo 25:21–34. Unaposoma, mualike kila mtoto kuchagua kitu cha kuchora kutoka kwenye hadithi. Halafu waalike watumie picha zao kuelezea hadithi hiyo kwa maneno yao wenyewe. Ikiwa wanahitaji msaada kuelewa ni haki gani ya mzaliwa wa kwanza, wahimize wasome “Haki ya Mzaliwa wa Kwanza” kwenye Mwongozo kwenye Maandiko (ChurchofJesusChrist.org). Waalike watoto wafikirie kwamba Esau aliomba ushauri wetu kuhusu kuuza haki yake ya mzaliwa wa kwanza kwa ajili ya dengu; tungemwambia nini?

  • Elezea juu ya wakati ambapo ilibidi utoe sadaka kitu kizuri kwa kitu kingine cha thamani kubwa zaidi. Au onyesha video “Continue in Patience” (ChurchofJesusChrist.org). Hadithi yako au hadithi ya kwenye video inahusiana vipi na chaguo ambalo Esau alifanya katika Mwanzo 25:29–34? Wasaidie watoto wafikirie baraka ambazo Baba wa Mbinguni anataka kuwapa (kama ushuhuda wenye nguvu, baraka za hekaluni, au uzima wa milele pamoja naye). Watie moyo wafikirie vitu watakavyokuwa tayari kujitolea ili kupata baraka hizi muhimu.

Picha
learning icon

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto wafikirie lengo ambalo wanaweza kujiwekea kuhusu kanuni ambazo wamejifunza katika Msingi leo. Kwa mfano, wanaweza kuweka lengo la kuwa na fadhili kwa wengine nyumbani.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Watoto wanapenda kushiriki kile wanachojifunza. Ingawa ni wadogo, watoto wanaweza kuwaimarisha wanafamilia wao. Wahimize watoto kushiriki na familia zao kitu walichojifunza katika darasa la Msingi. (Ona Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 30.)

Chapisha