Agano la Kale 2022
Januari 31–Februari 6. Mwanzo 6–11; Musa 8: “Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana”


“Januari 31–Februari 6. Mwanzo 6–11; Musa 8: “Nuhu Akapata Neema Machoni pa Bwana,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: Agano la Kale 2022 (2021)

“Januari 31–Februari 6. Genesis 6–11; Moses 8,”” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Msingi: 2022

Picha
Nuhu, familia yake, wanyama, sanduku, na upinde wa mvua

Mchoroo wa Nuhu akitoka kwenye safina, na Sam Lawlor

Januari 31–Februari 6

Mwanzo 6–11; Musa 8

“Nuhu akapata neema machoni pa Bwana”

Kujifunza juu ya wanyama katika safina ya Nuhu na Mnara mrefu wa Babeli kunaweza kuwafurahisha watoto. Lakini kumbuka kwamba hadithi hizi zina lengo la kufundisha kweli za milele. Kwa maombi fikiria kweli ambazo Mungu anataka watoto wajifunze.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kabla ya kuanza kufundisha hadithi kutoka Mwanzo 6–11 na Musa 8 kwa watoto, wape nafasi ya kufundishana kile wanachojua juu ya Nuhu na safina au Mnara wa Babeli.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wadogo

Mwanzo 6:14–22; 7–8; Musa 8:16–30

Kumfuata nabii kutanibariki mimi na familia yangu.

Watoto wanapojifunza kumfuata nabii, watabarikiwa na kuwekwa salama kiroho, kama vile familia ya Nuhu ilivyokuwa salama kutokana na mafuriko.

Shughuli Yamkini

  • Kwa maneno yako mwenyewe, toa hadithi ya Nuhu na safina (ona “Nuhu na Familia Yake,” katika Hadithi Za Agano la Kale; ona pia “Follow the Prophet,” Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11, aya 3). Wasaidie watoto kuigiza sehemu za hadithi—kwa mfano, kwa kujifanya kutumia zana kujenga safina au kutembea kama wanyama wanaoingia ndani ya safina.

  • Wasomee watoto Musa 8:19–20, sisitiza kile Bwana alichomwagiza Nuhu afanye. Wasaidie watoto kuelewa kuwa Nuhu alikuwa nabii na kwamba familia yake iliokolewa kutoka kwenye Gharika kwa sababu walimfuata. Waulize watoto kama wanamjua nabii wetu wa sasa. Onyesha picha yake na wasaidie watoto kurudia jina lake.

  • Lete picha darasani au vitu vinavyowakilisha mafundisho ya nabii wa sasa, kama vile maandiko au picha ya hekalu. Acha watoto wachukue zamu ya kuchagua kitu na kuwaambia darasa wanajua nini kuhusu hicho. Waeleze vitu hvyo vinawakilisha nini. Watie moyo wachore picha ya wao wenyewe wakitii yale ambayo nabii amefundisha. Toa ushuhuda wako juu ya baraka za kumfuata nabii.

Mwanzo 9:15–16

Mungu atatimiza ahadi Zake kwetu.

Ni muhimu kwa watoto kujua kwamba Mungu hutunza ahadi Zake, haswa wanapokuwa wanajiandaa kufanya maagano pale wanapokuwa wamebatizwa.

Shughuli Yamkini

  • Waalike wanafunzi kuchora picha za upinde wa mvua. Wasomee Mwanzo 9:15–16, na waombe wasikilize neno kumbuka. Waalike kuinua picha zao za upinde wa mvua juu wanaposikia neno hilo. Fafanua kwamba upinde wa mvua ni ukumbusho wa ahadi ambazo Mungu amefanya kwetu.

  • Ongea na watoto juu ya ahadi kadhaa za Mungu—kwa mfano, kwamba tunaweza kurudi kwa Baba wa Mbinguni ikiwa tutamfuata Yesu Kristo au kwamba Mungu atatuma Roho Mtakatifu kutufariji. Toa ushuhuda wako kuwa Mungu hutunza ahadi Zake kila wakati.

  • Tumia picha kuwaambia watoto kuhusu maagano tunayofanya na Mungu, kama vile picha za mtoto akibatizwa, sakramenti, na hekalu (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 104, 108120).

Musa 11:1–9

Njia pekee ya kufika mbinguni ni kwa kumfuata Yesu Kristo.

Watu wa Babeli walidhani wanaweza kufika mbinguni kwa kujenga mnara badala ya kuishi kulingana na injili ya Yesu Kristo. Unawezaje kuwasaidia watoto kuelewa kuwa kumfuata Mwokozi ndiyo njia pekee ya kurudi kwa Baba yetu wa Mbinguni?

Shughuli Yamkini

  • Eleza hadithi ya Mnara wa Babeli kwa maneno yako mwenyewe, au soma hadithi inayopatikana katika “Mnara wa Babeli” (kutoka Hadithi za Agano la Kale). Wahimize watoto kukusaidia kwa kushiriki kile wanachojua juu ya hadithi.

    Picha
    mfano wa mnara wa Babeli

    Mchoro wa Mnara wa Babeli, na David Green

  • Acha watoto wajenge mnara kwa kutumia vibao au vitu vingine. Kisha waonyeshe watoto picha ya Mwokozi, na uwaulize ni ipi njia ya kurudi kwa Baba wa Mbinguni—kujenga mnara au kumfuata Yesu Kristo? Waalike watoto waeleze juu ya mambo wanayoweza kufanya ili kumfuata Mwokozi.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho: Watoto Wakubwa

Mwanzo 6:14–22; 7–8; Musa 8:16–30

Kumfuata nabii kutanibariki mimi na familia yangu.

Watoto wanakua katika ulimwengu wa kiovu, sawa katika njia kadhaa kwa ulimwengu wakati wa Nuhu. Uzoefu wa Nuhu unaweza kuwapa ujasiri kwamba wanaweza kupata usalama wa kiroho wanapomfuata nabii.

Shughuli Yamkini

  • Wasaidie watoto kuchagua mistari kutoka Mwanzo 6:14–22; 7–8 ambayo wanaweza kuonyesha kwenye mchoro. Tumia michoro yao kuwafundisha hadithi ya Nuhu. Waombe watoto washiriki kile walichojifunza kwenye hadithi.

  • Onyesha picha ya Nuhu (ona Kitabu cha Sanaa ya Injili, na. 7–8) na nabii wa sasa. Wasaidie watoto kufunua Musa 8:16, 19–20, 23–24 ili kutafuta vitu ambavyo Nuhu alifundisha ambavyo viongozi wetu wa Kanisa bado wanafundisha hivi leo. Je, tunabarikiwa vipi tunapotii mafundisho haya?

  • Shiriki kitu fulani ambacho nabii wa sasa amekifundisha hivi karibuni. Waulize watoto waandike kitu ambacho nabii amefundisha kwenye karatasi, na uwasaidie kupanga vipande katika umbo la safina. Je, mafundisho haya yanafananaje na safina ambayo Nuhu aliijenga?

Mwanzo 9:15–17

Tunatakiwa kukumbuka maagano yetu.

Wakati tunapobatizwa, tunaweka maagano na Mungu kutii Amri Zake. Katika Mwanzo 9:15–17, upinde wa mvua hutambuliwa kama ukumbusho wa agano la Mungu. Mistari hii inaweza kuhamasisha watoto kutafuta njia za kukumbuka maagano yao na Mungu.

Shughuli Yamkini

  • Waonyeshe watoto kitu ulichonacho ambacho kinakukumbusha jambo muhimu katika maisha yako, kama vile pete ya harusi, picha, au jarida. Acha watoto washiriki mifano yao wenyewe. Someni pamoja Mwanzo 9:15–17 (ona pia Joseph Smith Translation, Genesis 9:21–25 [katika kiambatanisho cha Bibilia]). Ni nini Baba wa Mbinguni anatutaka sisi tufikirie kuhusu pale tunapoona upinde wa mvua?

  • Wakumbushe watoto juu ya maagano waliyoweka wakati wanabatizwa na kwamba wanayafanya upya kila mara wanapochukua sakramenti (ona Mosia 18:8–10; Mafundisho na Maagano 20:77, 79). Acha watoto wachore au kutengeneza kitu cha kuwakumbusha juu ya maagano yao.

Mwanzo 11:1–9

Njia pekee ya kufika mbinguni ni kwa kumfuata Yesu Kristo.

Wakati watu leo​wanaweza kujaribu kujenga minara ili kufika mbinguni, wengi hujaribu kupata amani na furaha kwa kufuata njia zingine kuliko zile ambazo Yesu Kristo ameanzisha. Unawezaje kutumia hadithi ya Mnara wa Babeli kufundisha kanuni hii?

Shughuli Yamkini

  • Waombe watoto kushiriki kile wanachojua kuhusu hadithi ya Mnara wa Babeli (ona Mwanzo 11:1–9). Kulingana na Helamani 6:28, kwa nini watu wa Babeli walijenga mnara? Kwa nini kujenga mnara huu ilikuwa njia mbaya ya kufika mbinguni? Je, unatoa ushauri gani kwa watu wa Babeli?

  • Waalike watoto kutafuta dokezo kwenye 2Nefi 31:20–21 na Helamani 3:28 kutafuta njia sahihi ya kufika mbinguni. Toa ushuhuda wako juu ya Mkombozi Yesu Kristo.

Picha
ikoni ya kujifunza

Himiza Kujifunza Nyumbani

Waalike watoto kufikiria njia watakazofundisha familia zao kuhusu hadithi walizojifunza katika Msingi. Kwa mfano, wanaweza kutumia picha walizochora katika ukurasa wa shughuli wiki hii.

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Tafuta kuwaelewa watoto unaowafundisha. Unapofundisha watoto, zingatia maswali yao, maoni yao, na hadithi au kanuni zinazoonekana kuwa zenye maana kwao. Kujua mambo haya itakusaidia kuzingatia mahitaji yao.

Chapisha