Agano la Kale 2022
Februari 7–13. Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2: “Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki.”


“Februari 7–13. Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2: “Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 7–13. Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Ibrahimu na Sara

Kielelezo cha Ibrahimu na Sara na Dilleen Marsh

Februari 7–13

Mwanzo 12–17; Ibrahimu 1–2

“Kuwa Mfuasi Mkubwa wa Haki”

Nini Roho Mtakatifu amekufundisha wiki hii ulipokuwa unajifunza Mwanzo 12–17 na Ibrahimu 1–2? Kuwa na uhakika kuwapa washiriki wa darasa fursa kushiriki kile ambacho Roho Mtakatifu amewafundisha.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwapa washiriki wa darasa fursa za kushiriki kitu fulani walichojifunza kutoka Mwanzo 12–17 na Ibrahimu 1–2, wangeweza kila mmoja kuchagua mtu aliyetajwa katika sura hizi na kukamilisha sentensi kama zifuatazo: “Ibrahimu alinifundisha ” au “Sara alinifundisha .”

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mwanzo 15:1–6; 17:15–22; Ibrahimu 1: 1–19

Mungu atatubariki kwa ajili ya imani yetu na matamanio ya haki.

  • Uzoefu wa Ibrahimu na Sara uliorekodiwa katika Mwanzo 15; 17; Ibrahimu 1 unaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kudumisha imani ili matamanio yao ya haki yakamilishwe katika muda wa Bwana. Jinsi gani Unaweza kuanzisha majadiliano kuhusu kanuni hii? Wazo moja ni kuliomba darasa kutafuta mwanzo 15:1–6 na Ibrahimu 1:1–19 na kuelezea matamanio ya Ibrahimu na hali ngumu. Jinsi gani Ibrahimu na Sara walionesha imani yao katika nyakati za matatizo? (Ona Waebrania 11:8–13). Jinsi gani matamanio yao ya haki hatimaye yalikamilishwa? (Ona Mwanzo 17:15–22; 21:1–3; Mafundisho na Maagano 132:29; Ibrahimu 1:31). Jinsi gani tunaonesha imani yetu wakati matamanio yetu ya haki bado hayajakamilishwa kama tunavyotaka yawe? Labda washiriki wa darasa wangeweza kushiriki jinsi ambavyo Mwokozi amewasaidia katika hali kama hizo.

  • Baadhi ya washiriki wako wa darasa wanaweza kupokea msaada kidogo kutoka kwa familia zao pale wanapojitahidi kuishi injili—na wanaweza hata kukabiliana na upinzani. Tunajifunza nini kutokana na mfano wa Ibrahimu katika Ibrahimu 1:1–19 ambacho kinawezaa kuwasaidia wale wanaojitahidi kuishi kwa haki katika hali kama hizi?

  • Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kusoma Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:36–40 (katika kiambatanisho cha Biblia) na kushiriki kile wanachojifunza kuhusu imani na matamanio ya Ibrahimu. Wanaweza pia kushiriki jinsi walivyobarikiwa wakati walipotumia imani yao kulipa zaka.

Ibrahimu 2:6–11

Agano la Ibrahimu linatubariki sisi wote.

  • Kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa agano la Ibrahimu ni nini, unaweza kushiriki maelezo ya Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Ziada” (ona pia Mada za Injili, “Agano la Ibrahimu,” topics.ChurchofJesusChrist.org). Washiriki wa darasa wanaweza kuwa wamejifunza kuhusu agano la Ibrahimu kutoka Ibrahimu 2:6–11, kama ilivyopendekezwa katika muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kushiriki kile walichojifunza, au darasa lingeweza kujifunza mistari pamoja. Ni ahadi gani na majukumu tunayopokea kupitia agano la Ibrahimu? Video “Special Witness—President Nelson” inaweza kusaidia kujibu swali hili (ChurchofJesusChrist.org/media-library/video/2011-04-18-special-witness-president-nelson). Tunahitaji kufanya nini kupokea msaada Bwana alioahidi kwa ajili yetu? Jinsi gani tunaweza, kama uzao wa Ibrahimu, kubariki “familia zote za dunia”? (Ibrahimu 2:11).

Mwanzo 14:18–19; Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:25–40

“Melkizedeki alikuwa mtu wa imani.”

  • Kwa sababu ya Urejesho wa injili, waumini wengi wa Kanisa wana ufahamu wa Ukuhani wa Melkizedeki, lakini baadhi hawajui kuhusu mtu Melkizedeki. Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kujifunza zaidi kuhusu yeye, pengine ungeweza kuwaomba kufikiria kwamba walikuwa wameombwa kumtambulisha kwa mtu fulani ambaye hakumjua na tengeneza orodha ubaoni ya vitu watakavyosema. Wangeweza kuweka msingi wa vitu hivi kwenye kile wanachosoma katika Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 14:26–27, 33–38 (katika kiambatanisho cha Biblia); Alma 13:13–19; na Mafundisho na Maagano 107:1–4. Je, tunajifunza nini kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki kutokana na mistari hii?

    Melkizedeki akimbariki Ibrahimu

    Melkizedeki akimbariki Ibrahimu, na Walter Rane

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Baraka za agano la Ibrahimu.

Rais Russell M. Nelson alifundisha:

“Agano ambalo Mungu alilifanya na Ibrahimu na baadaye kuhakikishwa na Isaka na Yakobo ni la umuhimu kupita mpaka. … Bwana alitokea katika siku hizi za mwisho kufanya upya agano lile la Ibrahimu. … Pamoja na kufanywa upya huku, tumepokea, kama wale wa kale, ukuhani mtakatifu na injili ya milele. Tuna haki ya kupokea utimilifu wa injili, kufurahia baraka za ukuhani, na kustahili kwa baraka kubwa mno za Mungu—zile za uzima wa milele” (“Maagano;” Liahona, Nov. 2011, 87–88).

“Hatima ya baraka za agano la Ibrahimu hutunukiwa katika mahekalu matakatifu. Baraka hizi zinaturuhusu kuja mbele katika Ufufuko wa Kwanza na kurithi viti vya enzi, falme, uwezo, himaya za kifalme, na mamlaka, kwenye ‘kuinuliwa kwetu na utukufu katika vitu vyote’ [Mafundisho na Maagano 132:19]” (“Special Witnesses of Christ,” Ensign, Apr. 2001, 7).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Toa ushuhuda kila mara. Ushuhuda wako rahisi, wa kweli kuhusu ukweli wa kiroho unaweza kuwa na ushawishi wenye nguvu kwa wale unaowafundisha. Kwa mfano, ungeweza kushiriki ushuhuda wa kawaida kuhusu jinsi maagano yalivyobariki maisha yako.