“Machi 14–20. Mwanzo 42–50: ‘Mungu Aliyakusudia Kuwa Mema,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)
“Machi 14–20. Mwanzo 42–50,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022
Machi 14-20
Mwanzo 42–50
“Mungu Aliyakusudia Kuwa Mema”
Mzee David A. Bednar alisema, “Uelewa wa kiroho ambao nyinyi na mimi tumebarikiwa kuupata … kwa kawaida hauwezi kutolewa tu kwa mtu mwingine” (“Tafuta Kujifunza kwa Imani,” Ensign, Sept. 2007, 67). Utawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa kupata uelewa wa kiroho kwa ajili yao wenyewe?
Andika Misukumo Yako
Alika Kushiriki
Kuwapa washiriki wa darasa fursa ya kushiriki kitu fulani walichokipata chenye maana katika kujifunza binafsi maandiko au kifamilia, ungeweza kuuliza maswali kama haya mwanzoni mwa darasa: ni mstari gani katika sura hizi uliuelewa vizuri? Ni mstari gani ulijikuta ukiusoma zaidi ya mara moja? Ni mstari gani uliushiriki na mtu mwingine? Ni msitari gani ilikulielekeza kwenye majadiliano ya kiutambuzi na familia yako au marafiki?
Fundisha Mafundisho
Msamaha Huleta amani.
-
Kabla hujaanza majadiliano kuhusu nini uzoefu wa Yusufu unafundisha kuhusu msamaha, inaweza kusaidia kumpata mtu fulani kwa kifupi aelezee hadithi katika Mwanzo 37; 39–45. Kwa nini iliweza kuwa vigumu kwa Yusufu kuwasamehe kaka zake? Uzoefu gani au fikra ziliweza kumpa Yusufu nguvu kuwasamehe? (Ona, kwa mfano, mwanzo 45:1–15 au 50:15–21) Jinsi gani mfano wa Yusufu unatusaidia kuwa wenye kusamehe zaidi?
Video “Forgiveness: My Burden Was Made Light” (ChurchofJesusChrist.org) inatoa mfano mwingine unaotia moyo wa msamaha. Jinsi gani Mwokozi anatusaidia kusamehe wengine?
-
Baraka gani zilikuja kutokana na msamaha wa Yusufu kwa kaka zake? Inaweza kuwa ya kupendeza kufananisha mahusiano katika familia ya Yakobo mwanzoni mwa hadithi (ona, kwa mfano, Mwanzo 37:3–11) pamoja na hali yao mwishoni (ona Mwanzo 45:9–15; 50:15–21). Ni jukumu gani msamaha ulifanya katika mabadiliko ya familia ya Yusufu? Jinsi gani mambo yangeweza kuwa tofauti kama Yusufu asingekuwa radhi kusamehe? Unaweza kumwomba mshiriki wa darasa kupendekeza njia ambayo hadithi hii ingeweza kuzisaidia familia leo kushinda mabishano na wivu.
Mwanzo 45:5–11; Joseph Smith Translation (katika Kiambatanisho cha Biblia)
Kazi za Yusufu, Musa, na Joseph Smith zinashuhudia juu ya misheni ya Yesu Kristo.
-
Kwa nuru ya ziada ya injili ya urejesho, tunajua kwamba Yusufu, ambae aliokoa familia yake kwenye njaa, pia alitabiri juu ya baraka kuu ambazo siku moja zitakuja kupitia Musa na Joseph Smith. Na manabii wote hawa wanatuelekeza kwa Mkombozi Wetu Mkuu, Yesu Kristo. Kuwasaidia washiriki wa darasa kumwona Mwokozi katika huduma za manabii hawa watatu, ungeweza kuchora chati ubaoni sawa na ile inayopatikana katika “Nyenzo za Ziada.” Washiriki wa darasa wangeweza kufanya kazi pamoja kuijaza. Kisha wangeweza kuongeza safu zinazoelezea kazi ya Yusufu wa Misri, Musa, na Joseph Smith, wakitumia kile wanachosoma kutoka Mwanzo 45:5–11 na Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50:24–38 (katika kiabatanisho cha Biblia). Jinsi gani huduma za manabii hawa zunashuhudia juu ya, na kuelekeza kwenye misheni ya Mwokozi? (Kwa baadhi ya mifano ya mifanano kati ya maisha ya Yusufu wa Misri na maisha ya Mwokozi, ona Mwanzo 37:3 na Mathayo 3:17; Mwanzo 37;26–28 na Mathayo 26:14–16; Mwanzo 45:5–7 na Luka 4:18; na Mwanzo 47:12 na Yohana 6:35; ona pia Musa 6:63.)
Mungu anaweza kutusaidia kupata maana katika majaribu yetu.
-
Ingawa yawezekana haikuwa wazi alipokuwa akipitia majaribu yake makali, Yusufu hatimaye aliweza kuangalia nyuma kwenye shida zake Misri na kuona kwamba “Mungu aliyakusudia kuwa mema” (Mwanzo 50:20). Kama tungeweza kumtembelea Yusufu alipokuwa shimoni au gerezani, jinsi gani tungeweza kumfariji? Jinsi gani wazo lililoelezwa katika Mwanzo 50:19–21 litatusaidia katika nyakati za majaribu? Pengine washiriki wa darasa wataridhia kuzungumza kuhusu njia ambazo Mungu amewabariki hata kupitia uzoefu mgumu walioupata. Kwa mfano mmoja, ona video “Unto All the World: The Sam Family” (ChurchofJesusChrist.org). Ni nini Mafundisho na Maagano 122 inaoongeza kwenye uelewa wetu wa kanuni hii?
Nyenzo za Ziada
Maisha ya manabii yanashuhudia juu ya Yesu Kristo na misheni yake.
Maisha ya Yusufu wa Misri, Musa, na Joseph Smith yanaweza kutukumbusha juu ya Yesu Kristo. Washiriki wa darasa wangeweza kujaza chati hii na kisha kuongeza safu kwa ajili ya Yusufu wa Misri (ona Mwanzo 45:5–11), Musa (ona Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50:24, 29, 34–36 [katika kiambatanisho cha Biblia]), na Joseph Smith (ona Tafsiri ya Joseph Smith, Mwanzo 50:26–28, 30–33 [katika kiambatanisho cha Biblia]).
Yesu Kristo | |
---|---|
Nani alikombolewa? | |
Walikombolewa kutoka nini? | |
Nini kilifanyika kuwakomboa? |