Agano la Kale 2022
Machi 7–13. Mwanzo 37–41: “Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu”


“Machi 7–13. Mwanzo 37–41: ‘Bwana Alikuwa pamoja na Yusufu,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Machi 7–13. Mwanzo 37–41,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
Yusufu wa Misri gerezani

Kielelezo cha Yusufu wa Misri gerezani, na Jeff Ward

Machi 7–13

Mwanzo 37–41

“Bwana alikuwa pamoja na Yusufu”

Haikusudiwi kwamba ufundishe shughuli zote katika muhutasari huu. Unapojiandaa kufundisha, omba kwamba Roho akusaidie kujua ni shughuli gani (kama zipo) katika muhutasari huu zitakidhi vyema mahitaji ya darasa lako.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kuwatia moyo washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza katika kujifunza kwao binafsi na kifamilia, ungeweza kuwaomba kutafuta kirai katika Mwanzo 37–41 ambacho kinaelezea somo au kanuni wanayohisi ni muhimu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Kutoka 37:1–28; 39; 40:1–19; 41:9–45

“Bwana alikuwa pamoja na Yusufu” katika shida zake.

  • Kama Yusufu, washiriki wa darasa lako wanaweza kuwa wanakabiliana na majaribu. Kulisaidia darasa kupata mwongozo wa kiungu katika mfano wa Yusufu, ungeweza kuwagawa katika makundi matatu na kuliomba kila kundi kurejea upya moja ya vifungu vya maandiko vifuatavyo: Mwanzo 39: 40:1–19; au 41:9–45. Kila kundi kisha lingeweza kushiriki njia ambazo Bwana alikuwa na Yusufu katika changamoto zake. Kama inafaa, washiriki wa darasa wangeweza kushiriki uzoefu wakati Bwana alipokuwa pamoja nao wakati wa majaribu magumu. Jinsi gani tunaweza kujifunza kuona vyema uwepo wa Bwana katika maisha yetu?

  • Somo hili linalofundishwa kwa vielelezo linaweza kueleza jinsi tunavyoweza kuinuka juu ya shida: weka kitu chepesi, kama vile mpira wa plastiki, chini ya chombo kilichojazwa nusu yake kwa mchele mkavu au maharage. Mwombe mtu fulani atikise chombo polepole mpaka mpira uinuke mpaka juu. Jinsi gani Yusufu alikuwa kama mpira? Washiriki wa darasa wangeweza kushiriki mifano ya Bwana kumsaidia Yusufu kuinuka juu ya shida kutoka Mwanzo 37:5–11; 39; 40:1–19; 41:9–45. Wangeweza pia kushiriki nyakati Bwana alipowasaidia katika njia sawa na hizo.

  • Ungeweza kuwaomba washiriki wa darasa kuimba au kusoma maneno ya wimbo kuhusu kufanya chaguzi za haki, kama vile “Do What Is Right” (nyimbo za Kanisa, na. 237). Kisha washiriki wa darasa wangeweza kupata utambuzi au virai katika Mwanzo 37:1–28; 39; 40:1–19; 41:9–45 ambavyo vinaelezea jumbe za wimbo. Jinsi gani Yusufu alibarikiwa, licha ya shida zake, wakati alipofanya kile kilicho chema? Lini Bwana ametubariki katika nyakati za shida kwa kufanya jambo jema?

Mwanzo 37:5–11; 40; 41:1–38

Kama tuna imani, Bwana atatuongoza na kututia moyo.

  • Ingawa sio kila mtu anapokea ufunuo binafsi kupitia ndoto, kuna vitu tunaweza kujifunza kuhusu ufunuo kutokana na uzoefu wa Yusufu, watumishi wa Farao, na Farao. Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kurejea upya Mwanzo 37:5–11; 40:5–8; 41:14–25, 37–38 na kushiriki kila kitu walichojifunza kuhusu ufunuo. ungeweza pia kuwaomba kushiriki kile ambacho kimewasaidia kujiandaa kupokea, kuelewa, na kufanyia kazi ufunuo.

    Picha
    Yusufu gerezani akitafsiri ndoto

    Yusufu akitafsiri Ndoto za Mnyweshaji na Mwoka mikate, na François Gérard

Mwanzo 39:1–20

Kwa msaada wa Bwana, tunaweza kukimbia majaribu.

  • Unaweza kuwaomba washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza kuhusu kuepuka majaribu wakati wanaposoma Mwanzo 39 wiki hii. Yusufu alifanya nini kushinda majaribu? (Ona mistari 7–12). Video “Leave the Party” na “Dare to Stand Alone” (ChurchofJesusChrist.org) zinatoa mifano ya watu walioepuka majaribu. Fikiria kuwaomba washiriki wa darasa kutengeneza orodha ya vitu tunavyoweza kufanya ili kuvuta uwezo wa Bwana wakati tunapokabiliana na majaribu. (Washiriki wa darasa wangeweza kupata mawazo katika Mathayo 4:1–11 au katika maandiko yaliyoorodheshwa chini ya “Tempt, Temptation” katika Mwongozo kwenye Maandiko [scriptures.ChurchofJesusChrist.org].)

  • Jinsi gani unaweza kutumia mfano wa Yusufu kuwasaidia washiriki wa darasa kuepuka jaribu la kufanya dhambi ya uasherati? Kwa kuongezea kwenye kurejea upya Mwanzo 39:1–20, washiriki wa darasa wangeweza kuangalia video “Chastity: What are the Limits?” (ChurchofJesusChrist.org) au kurejea upya “Sexual Purity” (katika Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana (2011), 35–37). Wangeweza kushiriki kile wanachojifunza kuhusu kuepuka mawazo, maneno, na matendo ambayo yanaelekeza kwenye dhambi ya uasherati. Kurejea upya “Toba” (katika Kwa ajili ya Nguvu kwa Vijana, 28–29) kunaweza kuwasaidia washiriki wa darasa kuelewa fursa ambayo Yesu Kristo anatoa kwetu ya kutubu.

Mwanzo 41:15–57

Tunapaswa kujiandaa kwa ajili ya uwezekano wa taabu.

  • Ungeweza kumwomba mshiriki mmoja wa darasa kuelezea ndoto za Farao (ona Mwanzo 41:15–24) na mwingine kushiriki tafsiri za Yusufu (ona mistari 25–32). Yusufu alishauri kufanya nini? ((Ona mistari 33–36, 47–49). Ni mafunzo gani maelezo haya yanayo kwa ajili ya wakati wetu? (Ona ushauri wa Rais Gordon B. Hinckley katika “Nyenzo za Zaida”).

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Jiandae kwa ajili ya nyakati za matatizo.

Rais Gordon B. Hinckley alisema: “Ninawasihi nyinyi muwe wenye staha katika matumizi yenu; mjiwekee nidhamu wenyewe katika manunuzi yenu ili kuepuka madeni kadiri iwezekanavyo. Lipa deni haraka kadiri uwezavyo. … Kuwa na akiba, hata kama itakuwa ndogo” (“To the Boys and to the Men, Ensign, Nov. 1998, 54).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kusikiliza ni kitendo cha upendo. Muombe Baba wa Mbinguni akusaidie kuelewa kile washiriki wa darasa lako wanachosema. Unapotoa usikivu wa makini kwa jumbe zao zinazozungumzwa na zisizozungumzwa, utakuja kuelewa vyema mahitaji yao” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 34).

Chapisha