Agano la Kale 2022
Februari 28–Machi 6. Mwanzo 28–33: “Kweli Bwana yupo Mahali Hapa”


“Februari 28–Machi 6. Mwanzo 28–33: ‘Kweli Bwana yupo Mahali Hapa,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Februari 28–Machi 6. Mwanzo 28–33,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
Hekalu la Tijuana Mexico

Februari 28–Machi 6

Mwanzo 28–33

“Kweli Bwana yupo Mahali Hapa”

Unapojiandaa kufundisha, kwa sala fikiria kanuni zipi katika Mwanzo 28–33 zitasaidia sana kwa washiriki wa darasa lako. Mawazo yafuatayo yamekusudia kuongeza kwenye mafunzo yako binafsi na mwongozo wa kiungu.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Moja ya baraka ya kukusanyika katika darasa la Shule ya Jumapili ni kwamba waumini wanaweza kusaidiana kupata maana katika maandiko. Watie moyo washiriki wa darasa kushirikiana na yule waliyekaa karibu naye kile Roho Mtakatifu alichowafundisha walipojifunza maandiko wiki hii. Wachache wangeweza kualikwa kushiriki pamoja na darasa kile walichojadiliana. Hii inaweza kutengeneza mahala pazuri pa kuanzia kwa ajili ya majadiliano ya darasa.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Mwanzo 28:10–22

Ndani ya Hekalu tunafanya maagano na Mungu.

  • Unawezaje kuwasaidia washiriki wa darasa lako kupata maana ya uzoefu wa Yakobo huko Betheli, kama ilivyoelezwa katika Mwanzo 28:10–22? Wanaweza kuanza kwa kurejea Mwanzo 27:41–45; 28:1–5 na kufikiria maisha ya Yakobo wakati ule. Jinsi gani Yakobo alikuwa akijisikia? Washiriki wa darasa kisha wangeweza kuchunguza Mwanzo 28:10–22. Jinsi gani uzoefu huu ulimbariki Yakobo? Jinsi gani aliweza kufarijiwa? Jinsi gani uzoefu wa Yakobo unaweza kututia moyo tunapoabudu ndani ya hekalu? Darasa lingeweza pia kuimba, kusoma, au kusikiliza “Nearer My,God to Thee, “ambayo ina msingi kwenye mistari hii (Nyimbo za Kanisa, na. 100). Wangeweza kushiriki virai kutoka kwenye wimbo au kutoka Mwanzo 28:10–22 ambavyo vingewakumbusha juu ya uzoefu waliokuwa nao kwa kujaribu kusogea karibu zaidi kwa mwokozi.

  • Ngazi Yakobo aliyoiona katika ndoto yake mara nyingi imekuwa ikifananishwa na maagano ya hekaluni. Pengine ungeweza kuwaonesha au kuchora picha ya ngazi na hekalu. Washiriki wa darasa wangeweza kurejea Mwanzo 28:10–22 na kuzungumza kuhusu kile ambacho ngazi katika ndoto ya Yakobo inatufundisha kuhusu hekalu. Nini kingine tunachokipata katika mistari hii ambacho kinatukumbusha juu ya baraka tunazopokea kwa sababu ya maagano yetu ya hekaluni? (Ona “About the Temple Endowment” na “About a Temple Sealing” [temples.ChurchofJesusChrist.org].)

  • Ili kuwasaidia washiriki wa darasa kutafakari ahadi za agano la Ibrahimu ambalo Bwana alilifanya upya na Yakobo, ungeweza kuwaomba wasome Mwanzo 28:10–15 na kuzungumza kuhusu jinsi tunavyoweza kupokea baraka hizi leo (ona pia Mwanzo 12:2–3). Wangeweza pia kusoma maelezo ya Rais Russell M. Nelson katika “Nyenzo za Ziada,” wakitafuta baraka ambazo zinakuja kutokana na kufanya na kushika maagano. Jinsi gani Yakobo alibarikiwa kwa kupokea ahadi zinazopatikana katika Mwanzo 28:10–15? Ni mahusiano gani tunayoyaona kati ya matukio katika mistari hii na matukio katika Mwanzo 29 na 30 (Yakobo akioa na kuzaliwa kwa watoto wake)? Ni kwa jinsi gani Bwana anatubariki tunapofanya na kushika maagano matakatifu?

Picha
Yakobo na Esau wakikumbatiana

Kielelezo cha Yakobo na Esau wakikumbatiana, na Robert T. Barrett

Mwanzo 32–33

Mwokozi anaweza kutusaidia kushinda kutokuelewana katika familia zetu.

  • Mwanzo 32–33 inaweza kuwatia moyo washiriki wa darasa wanaotaka kupata uponyaji katika mahusiano ya familia zao. Inaweza kuwa ya kusaidia kumwomba mshiriki wa darasa kwa kifupi kufanya muhutasari wa matukio yaliyoandikwa katika Mwanzo 27. Muhtasari wa wiki hii katika Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia unajumuisha maswali ya kutafakari wakati wa kujifunza Mwanzo 32–33. Pengine washiriki wa darasa wangeweza kuchagua moja ya maswali haya na kutafuta majibu katika sura hizi. Wanaweza pia kuwa radhi kushiriki uzoefu waliowahi kuwa nao kwa kuimarisha mahusiano ya kulazimishwa katika familia zao. Watie moyo kuzungumza kuhusu jinsi Baba wa Mbinguni alivyowasaidia.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Sisi ni watoto wa agano.

Rais Russell M. Nelson alifundisha:

“Wakati wa ubatizo tunaweka agano kumtumikia Bwana na kutii amri Zake. Tunaposhiriki sakramenti, tunafanya upya agano hilo na kutangaza utayari wetu kujichukulia juu yetu jina la Yesu Kristo. Kwa hiyo tumeasiliwa kama wana na mabinti zake na tunajulikana kama kaka na dada. Yeye ni Baba wa maisha yetu mapya. Hatimaye, katika hekalu takatifu, tunaweza kuwa warithi wa pamoja kwa baraka za familia ya milele, kama mwanzo ilivyoahidiwa kwa Ibrahimu, Isaka, Yakobo na uzao wao. Kwa hiyo, ndoa za selestia ni agano la kuinuliwa.

“Tunapotambua kwamba sisi ni wana wa agano, tunajua sisi ni nani na kile Mungu anachotarajia kutoka kwetu. Sheria yake imeandikwa katika mioyo yetu. Yeye ni Mungu wetu na sisi ni watu Wake. Wana wa agano wenye msimamo wanabaki imara, hata katika mateso. Wakati fundisho hilo likipandwa ndani ya mioyo yetu, hata maumivu ya kifo yanafanywa kuwa nafuu na nguvu yetu ya kiroho inaimarishwa” (“maagano,” Liahona, Nov. 2011, 88).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Wasaidie wanaojifunza kufanyia kazi ushawishi. “Uongofu wa kweli unajumuisha zaidi ya kuhisi Roho tu akithibitisha ukweli katika nafsi zetu; ni lazima pia tuufanyie kazi ukweli huo. Zaidi ya kuwasaidia wanaojifunza kuhisi na kumtambua Roho, wasaidie kutenda juu ya ushawishi wanaoupokea” (Kufundisha katika njia ya mwokozi 10).

Chapisha