Agano la Kale 2022
Novemba 7–13. Hosea 1–6; 10–14; Yoeli: “Nitawapenda kwa Ukunjufu wa Moyo”


“Novemba 7–13. Hosea 1–6; 10–14; Yoeli: ‘Nitawapenda kwa Ukunjufu wa Moyo,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Novemba 7–13. Hosea 1–6; 10–14; Yoeli,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
bibi harusi na bwana Harusi kwenye viwanja vya hekalu

Novemba 7–13

Hosea 1–6; 10–14; Yoeli

“Nitawapenda kwa Ukunjufu wa Moyo”

Unapojifunza na kujiandaa wiki hii, fikiria ni upi kati ya ujumbe mzuri na wenye kuinua kutoka katika kitabu cha Hosea na Yoeli ungeweza kukidhi mahitaji ya wale unaowafundisha.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Ili kuwahimiza washiriki wa darasa kushiriki kile walichojifunza wiki hii, unaweza kuwaalika waandike ubaoni neno au kirai ambacho kimewavutia wakati wa kujifunza kwao. Kisha wanaweza kuelezea kwa nini neno au kirai hicho kina maana kwao. Maneno hayo na virai hivyo vinaweza kusaidia kuongoza mjadala wako wote.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Hosea 1– 3; 14

Bwana daima hutualika sisi turudi Kwake.

  • Ungeweza kuanza mjadala wa Hosea 1–3 kwa kuandika ndoa ubaoni na kuwaomba washiriki wa darasa kuorodhesha maneno ambayo wanayahusisha na ndoa. Ni kwa jinsi gani kufanya agano na Bwana ni kama kuingia katika ndoa? Ni kwa jinsi gani kuvunja agano hilo ni kama kutokuwa mwaminifu kwa mwenzi? (Ona Hosea 2:5–7, 13). Kisha darasa linaweza kuzungumza kuhusu jinsi uhusiano katika Hosea na Gomeri huashiria uhusiano kati ya Bwana na watu Wake. Ni nini Hosea 2:14–23 na Hosea 14 zinatufundisha sisi kuhusu upendo na rehema ya Bwana? Je, ni kwa jinsi gani sisi tunaonyesha upendo na uaminifu wetu Kwake?

  • Hosea 14 huelezea ahadi nyingi nzuri Bwana alizofanya kwa nyumba ya Israeli kama wangerudi Kwake. Labda washiriki wa darasa wanaweza kupekua sura hii wakitafuta ahadi hizi. Bwana alisema Yeye angefanya nini? Yawezekana kirai hiki “nawapenda kwa ukunjufu wa moyo” kina maana gani (mstari wa 4). Je, isitiari ya mmea katika mstari wa 5–8 inatufundisha nini kuhusu baraka za Bwana kwetu sisi, ikijumuisha baraka za toba?

    Picha
    mwanamke amekaa chini pamoja na mwanaume akimwekelea mkono kichwani

    Gomeri mwenye dhambi, ambaye huwakilisha Israeli, alipewa ukombozi na Bwana. Kielelezo na Deb Minnard, leseni kutoka kwa goodsalt.com

Hosea 6:6; Yoeli 2:12–13

Uchaji Mungu lazima usikike kwa ndani, hauonyeshwi nje pekee yake.

  • Hosea 6:6 na Yoeli 2:12–13 hurejelea dhabihu ya mnyama na kuchana nguo kama ishara ya majuto. Hali desturi kama hizo inawezekana kuwa si za kawaida leo, mistari hii inaweza kutuongoza kwenye mjadala kuhusu kitu kilicho muhimu zaidi kwa Bwana. Mnaweza kusoma pamoja Hosea 6:6 na kujadili yawezekana mstari huu unamaanisha nini. Alika baadhi ya washiriki wa darasa kusoma Mathayo 9:10–13 na wengine kusoma Mathayo 12:1–8. Kisha washiriki wa darasa wanaweza kufundishana jinsi matukio haya katika huduma ya Mwokozi yanatusaidia kuelewa kanuni inayofundishwa katika Hosea 6: 6. Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuishi kanuni hii katika siku yetu?

    Mnaweza pia kusoma kwa pamoja Yoeli 2:12–13 na mjadili inamaana gani kurarua mioyo yetu na si mavazi yetu tu. Tunajifunza nini kutoka kwenye mistari hii kuhusu kile inachomaanisha kuwa wanafunzi wa kweli Yesu Kristo?

Yoeli 2

“Nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili”

  • Ili kuanza mjadala wa Yoeli 2, unaweza kushiriki pamoja na darasa kile ambacho Moroni alisema kuhusu unabii huu wakati alipomtembelea Joseph Smith katika mwaka wa 1823 (ona Joseph Smith—Historia 1:41). Washiriki wa darasa wanaweza kuelezea jinsi wanavyohisi unabii katika Yoeli 2:28–32 unavyotimizwa katika siku yetu. Unaweza pia kujadili jinsi maneno ya Mzee David A. Bednar katika “Nyenzo za Ziada” yanavyohusiana na unabii wa Yoeli. Washiriki wa darasa wangeweza kujadili kile inachomaanisha kwao kuhisi mmiminiko wa Roho Mtakatifu katika maisha yao ya kila siku, Ni nini tunaweza kufanya kama tunahisi hatupokei mmiminiko kama huo? Je, ni kwa jinsi gani tunaweza kuwasaidia “wana [wetu] na mabinti [zetu] kuupokea? (mstari wa 28).

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

“Tunaweza kumtegemea Roho Mtakatifu kutuongoza.”

Mzee David A. Bednar alifundisha:

“Mara nyingi tunafanya iwe vigumu kupokea ufunuo binafsi. Kwa kusema hilo, ninamaanisha, ahadi ya agano ni kwamba tunapoheshimu maagano yetu, tunaweza daima kuwa na Roho Mtakatifu kama mwenzi wetu wa kudumu. Tunaongea juu yake na tunachukulia kama kusikia sauti ya Bwana kupitia Roho Wake ni tukio la nadra. … [Roho] anapaswa kuwa pamoja nasi nyakati zote. Sio kila sekunde, lakini kama mtu anajitahidi vizuri awezavyo—hauhitaji kuwa mkamilifu—lakini kama wewe na mimi tunajitahidi tuwezavyo na hatutendi dhambi nzito, basi tunaweza kutegemea Roho Mtakatifu kutuongoza.

“… Tunaonekana kuamini kwamba Roho Mtakatifu ni jambo la kidrama na kubwa na la ghafla, ilhali ni tulivu na dogo na huongezeka kidogo kidogo kwa muda. Hauhitajiki kutambua kwamba unapokea ufunuo ule muda ambapo unapokea ufunuo” (“Mzee David A. Bednar –Majadiliano” [jioni pamoja na Kiongozi Mkuu mwenye Mamlaka, Feb.7, 2020], broadcasts.ChurchofJesusChrist.org).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwa mwenye kukaribisha. Wanafunzi wanaweza kujua kwamba unawajali na unajali ukuaji wao wa kiroho. Njia moja ya kuwaonyesha hili ni kuwasalimu kwa moyo mkunjufu wanapowasili darasani. (Ona Kufundisha katika njia ya Mwokozi, 15.)

Chapisha