Agano la Kale 2022
Novemba 14–20. Amosi; Obadia: “Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi”


“Novemba 14–20. Amosi; Obadia: ‘Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Novemba 14–20. Amosi; Obadia,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Picha
uso wa Yesu umeangazwa na mishumaa katika chumba kilicho na giza

Mkate wa Uzima, na Chris Young

Novemba 14–20

Amosi; Obadia

“Mtafuteni Bwana, Nanyi Mtaishi”

Unapojifunza Amosi na Obadia, karibisha misukumo kuhusu kile unachopaswa kuwafundisha washiriki wa darasa lako. Andika mawazo haya, na utafute fursa za kuyashiriki katika darasa lako la Jumapili.

Andika Misukumo Yako

Picha
ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Kama vile tu Amosi na Obadia walivyowaonya watu wa siku zao, maneno yao pia yanatoa onyo kwetu leo. Unaweza kuwaalika washiriki wa darasa kushiriki mafundisho kutoka kwa Amosi na Obadia ambayo yanafaa kwetu.

Picha
ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Amosi 3:7–8; 7:10–15

Bwana hufunua ukweli kupitia kwa manabii Wake.

  • Waalike washiriki wa darasa kushiriki ukweli kuhusu manabii ambao wao waliupata katika kujifunza kwao binafsi au kama familia kwa Amosi 3 and Amosi 7. Unaweza kuorodhesha majibu yao ubaoni. Ni ukweli gani mwingine kuhusu manabii tunaoujua? (Kwa mawazo zaidi, ona makala ya Mada za Injili, “Manabii,” [topics.ChurchofJesusChrist.org].) Wahimize washiriki wa darasa kadhaa kushiriki jinsi walivyopokea ushuhuda wao wa kazi muhimu ya manabii katika mpango wa Mungu.

  • Je, tunawezaje kumwelezea rafiki kwa nini ni muhimu kuwa na nabii katika siku yetu? Unaweza kuorodhesha ubaoni maswali ambayo mtu fulani ambaye si muumini wa Kanisa angeweza kuuliza kuhusu manabii. Je, tunawezaje kujibu baadhi ya maswali haya tukitumia Amosi 3:7–8 na 7:10–15?

  • Kama sehemu ya mjadala wenu kuhusu manabii, ungeweza kushiriki mojawapo ya video zifuatazo: “We Need Living Prophets” or “Words of the Prophets” (ChurchofJesusChrist.org). Je, ni kwa jinsi gani manabii wa siku za mwisho hutusaidia kusogea karibu na Yesu Kristo?

Amosi 5; 8:11–12

Ukengeufu ni kama njaa ya kusikia maneno ya Bwana.

  • Ili kuanza mazungumzo kuhusu njaa Amosi aliyoelezea katika Amosi 8:11–12, ungeweza kupata msaada kwa kifupi kupitia tena hali ya kiroho ya watu aliokuwa akiwahubiria. Je, ni kwa namna gani Waisraeli waligeuka kutoka kwa Bwana? (ona, kwa mfano, Amosi 2:6–8; 5:11–12). Kwa nini itakuwa msaada kujua kuhusu kuanguka kwao? Washiriki wa darasa wanaweza kisha kusoma Amosi 8:11–12 na kuzungumza kuhusu kwa nini “njaa” na “kiu” ni maneno mazuri ya kuelezea hali ya wale wanaogeuka kutoka kwa Bwana. Washiriki wa darasa wanaweza pia kupekua Amosi 5 kutafuta mistari ambayo inaweza kutusaidia kuepuka ukengeufu katika maisha yetu (ona, kwa mfano, mstari wa 4, 11–12, 14–15, 25–26).

  • Kuelewa njaa ya kiroho ambayo huandamana na ukengeufu hutusaidia kuelewa karamu ya kiroho tunayofurahia kwa sababu ya Urejesho. Ungeweza kuandika maswali machache kuhusu Ukengeufu na Urejesho ubaoni, kama vile Kwa nini kulikuwa na Ukengeufu? Ni athari gani Ukengeufu ulileta kwa watoto wa Mungu’? Ni athari gani Urejesho ulileta? Wahimize washiriki wa darasa kupata majibu ya maswali haya na mengine wakitumia nyenzo zifuatazo: “Ujumbe wa Urejesho wa Injili ya Yesu Kristo” katika sura ya 3 ya Hubiri Injili Yangu ([2019], 36–39); makala ya Mada za Injili “Ukengeufu” (topics.ChurchofJesusChrist.org); video “The Great Apostasy” (ChurchofJesusChrist.org); na dondoo katika “Nyenzo za Ziada.” Waalike washiriki wa darasa kuzungumza kuhusu kweli zilizorejeshwa katika siku yetu ambazo hasa ni muhimu kwao.

Picha
kikundi cha vijana wamesimama mbele ya hekalu

Tunaweza kuwa waokozi juu ya Mlima Sayuni kwa kufanya kazi ya hekaluni na historia ya familia.

Obadia 1:21.

“Waokozi watakwea juu ya Mlima Sayuni.”

  • Kwa nini kirai “waokozi … mlima Sayuni” (Obadia 1:21) ni maelezo mazuri kwetu wakati tunapofanya kazi ya hekaluni na historia ya familia. Ni kwa jinsi gani kazi tunayofanya kwa niaba ya mababu zetu katika hekalu inatusaidia kuhisi kuwa karibu na Mwokozi Yesu Kristo? Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki matukio ya hivi karibuni waliyopata wakati wakifanya kazi ya hekaluni na historia ya familia.

Picha
ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Masomo kutoka zamani.

Rais M. Russell Ballard alifundisha:

“Katika kipindi kifupi cha miaka kinachoshughulikia Agano Jipya, … watu waligeuka dhidi ya Kristo na Mitume Wake. Anguko lilikuwa kubwa sana hata tumekuja kulijua kama Ukengeufu Mkuu, ambao ulisababisha karne za kudorora kiroho na ujinga inayoitwa Miaka ya Giza.

… Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote, na Yeye anataka wao wote kuwa na baraka za injili katika maisha yao. Nuru ya kiroho haijapotea kwa sababu Mungu hugeuza mgongo Wake kwa watoto Wake. Badala yake, giza la kiroho hutokea wakati watoto Wake wanapogeuzia Yeye migongo yao kwa ujumla wao. Ni matokeo ya asili ya chaguzi mbaya zilizofanywa na watu binafsi, jumuiya, nchi na ustaraabu wote. Hii imethibitishwa tena na tena kote katika nyakati zote. Mojawapo ya masomo makuu ya mpangilio huu wa kihistoria ni kwamba chaguzi zetu, zote kama watu binafsi na kwa ujumla wote, huleta matokeo ya kiroho kwetu wenyewe na vizazi vyetu” (“Kujifunza Masomo ya Zamani,” Ensign au Liahona, Mei 2009, 32).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Kuwasaidia wanafunzi kumtambua Roho Mtakatifu. “Kama unavyoshawishiwa na Roho Mtakatifu, waulize wanafunzi wanajisikiaje na wanajisikia kushawishika kufanya nini. Wasaidie kuhusisha hisia zao za kiroho na ushawishi wa Roho Mtakatifu” (Kufundisha katika Njia ya Mwokozi, 11).

Chapisha