Agano la Kale 2022
Novemba 21–27. Yona; Mika: “Yeye Hufurahia Rehema”


“Novemba 21–27. Yona; Mika: ‘Yeye Hufurahia Rehema,’” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: Agano la Kale 2022 (2021)

“Novemba 21–27. Yona; Mika,” Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Shule ya Jumapili: 2022

Mtu anatambaa ufukoni na nyangumi akiwa baharini  nyuma yake

Yona kwenye Ufukoni wa Ninawi, na Daniel A. Lewis

Novemba 21–27

Yona; Mika

“Yeye Hufurahia Rehema”

Uongofu wa kudumu unahitaji zaidi ya somo la kuvutia la Shule ya Jumapili wiki baada wiki. Wahimize washiriki wa darasa kutafuta uzoefu binafsi wa kiroho kote katika maisha yao.

Andika Misukumo Yako

ikoni ya kushiriki

Alika Kushiriki

Fikiria kuandika virai kama vifuatavyo ubaoni: Ukweli niliokumbushwa, Kitu kipya nilichojifunza, na Kitu ambacho ningependa kujifunza zaidi. Wape washiriki wa darasa muda kupitia kile walichojifunza katika Yona na Mika ambacho kinahusiana na mojawapo ya vifungu vya ubaoni.

ikoni ya kufundisha

Fundisha Mafundisho

Yona 1–4; Mika 7:18–19

Bwana ni mwenye rehema kwa wote wanaomgeukia Yeye.

Kukumbusha darasa lako rehema za Bwana kunaweza kuwasaidia wao kuhisi upendo Wake kwa ajili yao na kuwaongoza kutubu. Unaweza kualika darasa kusoma Mika 7:18–19 na kuorodhesha ubaoni baadhi ya matukio kutoka katika Yona 1–4 ambayo yanaonyesha Bwana anavyofurahia katika rehema. Ni uzoefu gani mwingine wa rehema za Bwana tunaweza kushiriki—kutoka katika maandiko au maisha yetu wenyewe?

Kupata uzoefu wa rehema za Bwana kunaweza kutuongoza kuwa wenye rehema zaidi. Hapa kuna wazo moja ambalo linaweza kuwasaidia washiriki wa darasa lako kujifunza kuhusu rehema kutoka katika kitabu cha Yona. Unaweza kuandika swali kama hili ubaoni: Ni nini rehema za Mungu, kama ilivyoonyeshwa katika Yona 1–4, kinaweza kunifundisha kuhusu kuwa na mwenye rehema zaidi? Kila mshiriki wa darasa anaweza kuchagua sura moja ya kurejelea na kutafuta majibu ya swali hili. Wape washiriki wa darasa muda wa kutafakari juu ya nafasi walizonazo za kubadilisha mitazamo ya kuhukumu na badala yake kuwa wenye rehema kwa wao wenyewe au wengine.

watu wawili wakizungumza kando ya mto

Tunaweza kushiriki injili pamoja na watoto wa Mungu.

Yona1; 3–4

Watoto wote wa Mungu wanahitaji kusikia injili.

  • Njia moja ya kupata masomo kutoka katika hadithi ya Yona ni kuilinganisha na matukio ya wamisionari katika Kitabu cha Mormoni. Fikiria kutengeneza safu mbili ubaoni zenye vichwa Yona na Alma na wana wa Mosia. Alika darasa kutofautisha mtazamo wa Yona kuhusu kuwafundisha watu wa Ninawi (ona Yona1; 3–4) na mtazamo wa wana wa Mosia kuhusu kuwafundisha Walamani (ona Mosia 28:1–5; Alma 17:23–25). Tunajifunza nini kutokana na zoezi hili kuhusu kushiriki injili na watoto wote wa Mungu?

  • Kama Yona, wengi wetu tunaweza kujisikia kusita kuwaalika wengine kumgeukia Bwana. Ni nini baadhi ya sababu zilizomfanya Yona atoroke wito wake wa kuwaonya watu wa Ninawi? Kwa nini wakati mwingine tunasita kushiriki injili? Washiriki wa darasa wanaweza kushiriki njia ambazo Bwana amewasaidia kushinda kusita kwao. Ushauri wa Henry B. Eyring katika “Nyenzo za Ziada” ungewasaidia washiriki wa darasa kutambua kanuni ambazo zinaweza kutia nguvu juhudi zetu za kushiriki injili.

Mika 6:6–8

“Bwana anataka nini kwako?

  • Mika 6:6–7 inataja vipengele kadhaa vya kanuni za ibada za Uyahudi ya kale. Lakini vitu fulani ni muhimu zaidi kwa Mungu kuliko kanuni za kuonyesha nje. Waalike washiriki wa darasa kutafuta vitu hivyo muhimu katika mstari wa 8. Labda washiriki wa darasa wangeweza kutambua virai muhimu na kujadili kitu ambacho kila kirai kinamaanisha. Kisha wanaweza kuchagua virai wavipendavyo, watafute maandiko yanayohusiana katika Mwongozo wa Maandiko au wimbo unaohusiana katika kitabu cha nyimbo, na kuelezea kile walichojifunza. Kwa nini kanuni hizi ni muhimu kwa Bwana?

ikoni ya nyenzo za ziada

Nyenzo za Ziada

Upendo, mfano, na ushuhuda.

Baada ya kujadili onyo la Yona kwa watu wa Ninawi, Rais Henry B. Eyring alisimulia tukio ambalo kwalo mama yake alimpatia onyo.

“Mimi bado nakumbuka mama yangu akiongea kwa sauti laini Jumamosi moja wakati wa alasiri ambapo, kama mvulana mdogo, nilimwomba ruhusa ya kufanya kitu nilichofikiri kilikuwa sahihi na cha kufaa na ambacho yeye alijua kilikuwa hatari. Mimi bado ninashangazwa na nguvu alizopewa, ninaamini kutoka kwa Bwana, kunigeuza kwa maneno machache tu. Ninavyoyakumbuka, yalikuwa: Eeh, nadhania wewe ungeweza fanya hivyo. Lakini chaguo ni lako.’ Onyo la pekee lilikuwa katika msisitizo alioweka kwa maneno ungeweza fanya na chaguo. Bado hiyo ilikuwa ya kutosha kwangu.

“Nguvu zake za kuonya kwa maneno machache tu zilichipua kutoka kwenye vitu vitatu mimi nilivyojua kumhusu yeye. Kwanza, nilijua ananipenda. Pili, nilijua yeye alikuwa tayari ameshafanya kile alichokuwa anataka mimi nifanye na kubarikiwa nacho. Na tatu, yeye alikuwa amewasilisha kwangu ushuhuda halisi kwamba chaguo ambalo mimi ningefanya lilikuwa muhimu kwamba Bwana angeniambia cha kufanya kama ningemwomba Yeye. Upendo, mfano, na ushuhuda: hivyo vilikuwa ndio funguo siku hiyo” (“Sauti ya Onyo,” Ensign, Nov. 1998,32).

Kuboresha Ufundishaji Wetu

Jiandae mwenyewe. Mafundisho ya injili yenye nguvu huanza kwa kujiandaa wenyewe. Kabla ya kuandaa somo lako, fokasi juu ya kuujaza moyo wako na Roho Mtakatifu kwa njia ya kujifunza na maombi yenye maana. (Ona Kufundisha Katika Njia ya Mwokozi, 12.)