Vitabu vya Maelekezo na Miito
14. Waumini Waseja


“14. Waumini Waseja,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“14. Waumini Waseja,“ Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
watu wakizungumza

14.

Waumini Waseja

14.0

Utangulizi

Wanaume na wanawake ambao hawajaoa au kuolewa au ambao wametalikiwa au wajane wanatengeneza sehemu muhimu ya waumini wa Kanisa. Ni muhimu kwa wote kupata tumaini kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo (ona Etheri 12:4). Kweli za milele zifuatazo zinaweza kusaidia kukuza matumaini kama hayo:

  • Maandiko na manabii wa siku za mwisho wanathibitisha kwamba kila mtu ambaye ni mwaminifu katika kuyashika maagano ya injili atakuwa na fursa ya kuinuliwa.

  • Muda kamili na namna ambavyo baraka za kuinuliwa zinatolewa siyo vyote vimekwisha kufunuliwa. Lakini hata hivyo zimehakikishwa (ona Mosia 2:41).

  • Subira juu ya Bwana inamaanisha utii endelevu na maendeleo ya kiroho kuelekea Kwake (ona Isaya 64:4).

  • Mungu hutoa uzima wa milele kwa watoto Wake wote. Wote wanaostahili kupata zawadi ya neema ya Mwokozi ya msamaha na kuishi amri Zake watapokea uzima wa milele. (Ona Mosia 26:30; Moroni 6:8.)

  • Ujasiri katika hakikisho hili umejikita kwenye imani katika Yesu Kristo. Kwa neema Yake, vitu vyote vinavyohusiana na maisha ya duniani vinawekwa sawa (ona Alma 7:11–13).

Bwana anawahitaji waumini wote ili kusaidia katika kazi ya wokovu katika kata, na vigingi vyao (ona 1 Wakorintho 12:12–27). Kadiri Roho atakavyoongoza, waumini waseja wanaitwa kwenye uongozi na nafasi za kufundisha.

Katika sura hii:

  • “Waumini waseja” ni waumini wote wa Kanisa walio watu wazima ambao kwa sasa hawajaoa au kuolewa.

  • “Vijana wakubwa waseja” ni wale wenye umri wa miaka 18–30

  • “Watu wazima waseja” ni wale wenye umri wa miaka 31 na zaidi.

14.1

Waumini Waseja katika Vitengo vya Kijiogrofia

14.1.1

Uongozi wa Kigingi

14.1.1.2

Kamati za Vijana Wakubwa Waseja na Watu Wazima Waseja katika Kigingi

Urais wa kigingi unaunda kamati ya vijana wakubwa waseja.

Urais wa kigingi unaweza pia kuunda kamati ya Watu wazima waseja.

Kamati zinatafuta kuwasaidia waumini kupitia urafiki na fursa za kushiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona 14.2).

14.1.2

Uongozi wa Kata

14.1.2.1

Uaskofu

Uaskofu ni ufunguo wa kuwashirikisha waumini waseja katika kazi ya wokovu na kuinuliwa. Wanafanya kazi na baraza la kata ili kutambua miito yenye maana na kupanga majukumu kwa ajili ya waumini waseja. Wanatambua na kujitahidi kusaidia kukidhi mahitaji ya wazazi wasio na wenza.

  • Mshiriki wa uaskofu anakutana na kila kijana mkubwa mseja angalau mara moja kwa mwaka.

  • Uaskofu unaweza kuanzisha kamati ya vijana wakubwa waseja katika kata.

14.1.2.2

Washiriki wa Urais wa Akidi ya Wazee na Muungano wa Usaidizi Waliopangiwa kwa Vijana Wakubwa Waseja

Marais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi wanaweza kila mmoja kumpangia mshiriki wa urais wao ili awasaidie vijana wakubwa waseja. Washiriki hawa wa urais wanajifunza juu ya uimara wa vijana wakubwa waseja na kusaidia kukidhi mahitaji yao.

Rais wa akidi ya wazee na rais wa Muungano wa Usaidizi wanaweza kuripoti juu ya juhudi hizi kwenye mkutano wa baraza la kata.

14.1.2.3

Viongozi wa Vijana Wakubwa Waseja

Katika kata yenye Vijana Wakubwa Waseja wengi, uaskofu unaweza kuita mwanamume kijana mseja na mwanamke kijana mseja kama viongozi wa vijana wakubwa waseja. Wajibu wao ni pamoja na:

  • Kuwasaidia vijana wakubwa waseja washiriki katika kazi ya wokovu na kuinuliwa (ona 14.2).

  • Kuhudumu katika kamati ya vijana wakubwa waseja katika kigingi.

  • Kuongoza kamati ya vijana wakubwa waseja katika kata kama itaanzishwa.

  • Kukutana mara kwa mara na urais wa akidi ya wazee na urais wa Muungano wa Usaidizi. Katika mikutano hii wanajadiliana uimara wa vijana wakubwa waseja na jinsi ya kusaidia kukidhi mahitaji yao. Pia wanafokasi juu ya uhudumiaji kwa vijana wakubwa waseja.

14.2

Kushiriki katika Kazi ya Wokovu na Kuinuliwa

14.2.1

Kuishi Injili ya Yesu Kristo

14.2.1.1

Jioni ya Nyumbani na Kujifunza Injili

Viongozi au waumini wanaotamani kushiriki wanaweza kutengeneza kundi moja au zaidi la jioni ya nyumbani kwa ajili ya watu wazima waseja na makundi mengine kwa ajili ya vijana wakubwa waseja.

14.2.1.3

Shughuli

Chini ya maelekezo ya viongozi wa kata au kigingi, vijana wakubwa waseja wanaweza kupanga na kushiriki kwenye shughuli mahususi kwa ajili yao. Mifano inaweza kujumuisha:

  • Kutembelea hekaluni.

  • Kazi ya historia ya familia.

  • Kushiriki Injili.

  • Huduma za Jamii.

  • Muziki na matukio ya kitamaduni.

  • Michezo.

Chini ya maelekezo ya viongozi wa kigingi, vijana wakubwa waseja wanaweza kupanga shughuli kama hizo kwenye ngazi ya kigingi.

Chapisha