“24. Mapendekezo ya Mmisionari na Huduma,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“24. Mapendekezo ya Mmisionari na huduma,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla.
24.
Mapendekezo ya Mmisionari na Huduma
24.0
Utangulizi
Katika nyakati za kale, Bwana alitoa mamlaka ya kuwakusanya Israeli miongoni mwa “mataifa yote, wakibatizwa katika jina la Baba, na Mwana, na la Roho Mtakatifu”.Mathayo 28:19; ona pia mstari wa 20) Bwana amerudia tena wito huo katika siku hizi za mwisho (ona Mafundisho na Maagano 39:11; 68:6–8; 112:28–30).
Kumtumikia Bwana kama mmisionari ni fursa takatifu. Inaleta baraka za milele kwa mtu huyo na wale anaowatumikia (ona Mafundisho na Maagano 18:14–16).
Bwana ameamuru kila mvulana mstahiki, na mwenye uwezo ajiandae kwa ajili ya na kutumikia misheni.
Bwana pia anamkaribisha kila msichana mwenye kustahili, na mwenye uwezo ajiandae kwa ajili ya kuhudumu misheni ikiwa wanatamani kufanya hivyo.
Wamisionari wazee pia wanahitajika na wanahimizwa kujitayarisha kuhudumu.
24.1
Wito wa Kuhudumu
Wamisionari wanamwakilisha Bwana na lazima waitwe kwa mamlaka sahihi (ona Mafundisho na Maagano 42:11; Makala za Imani 1:5). Wito wa kuhudumu misheni kwa kawaida unatolewa na Rais wa Kanisa. Kwa wamisionari wazee wanaohudumu, wito unatolewa na rais wa kigingi.
24.2
Majukumu ya Umisionari
Wito wa kuhudumu kama mmisionari unajumuisha majukumu maalumu. Majukumu haya hutofautiana sana.
24.2.1
Wamisionari Vijana Wanaofundisha
Wengi wa wamisionari vijana wanapangiwa kufundisha injili mbali na nyumbani. Teuzi hizi zinatolewa kwa ufunuo kwa Mitume. Wamisionari hawa wanahudumu chini ya maelekezo ya rais wa misheni.
24.2.2
Wamisionari Vijana watoa huduma
Baadhi ya wamisionari vijana wanapangiwa kuhudumia ndani ya Kanisa na kwa jamii wakati wakiishi nyumbani. Majukumu haya hutolewa kwa ufunuo kwa Mitume na yanatolewa kwa wateuliwa ambao hali zao zinakidhi misheni ya huduma(ona 24.3.3).
24.2.3
Wamisionari Wazee
Wamisionari wote wazee wanahimizwa kuwatafuta watu wa kuwafundisha na wawasaidie kujitayarisha kwa ajili ya ubatizo. Wamisionari wazee wanaweza pia kuteuliwa kusaidia:
-
Waumini na eneo na viongozi wenyeji.
-
Idara za Kanisa na vifaa.
-
Vikundi vya hisani.
Wamisionari wazee si lazima wafanye kazi masaa yanayofanana, wafanye shughuli zile zile, au wakamilishe matarajio yanayofanana na ya wamisionari vijana.
Majukumu kwa ajili ya wamisionari wazee yanatolewa kwa ufunuo kwa Mitume. Wateuliwa wanaweza kuonesha upendeleo kwenye jukumu lakini wanapaswa kuwa tayari kukubali jukumu lolote.
24.2.4
Wamisionari Wazee Watoa Huduma
Kwa nyongeza kwenye miito kwenye kata au kigingi cha nyumbani, waumini wanaweza kumhudumia Bwana kama Wamisionari Wazee watoa huduma. Wamisionari hawa wanatoa huduma ya thamani katika idara za Kanisa, majengo, na misheni (ona 24.7.1). Wanaishi majumbani mwao.
Wamisionari wazee watoa huduma wanaitwa na rais wa kigingi. Wanahudumu chini ya maelekezo yake. Kiasi cha muda wanaotumia kuhudumu kila wiki kinategemea na uwezo wao, fursa za kuhudumu katika eneo lao, na maelekezo kutoka Urais wa Eneo.
24.2.5
Muhtasari wa Majukumu ya Umisionari
Lifuatalo ni jedwali la muhtasari wa majukumu ya umisionari.
Mmisionari Kijana Anayefundisha |
Mmisionari Kijana Mtoa Huduma |
Mmisionari Mzee |
Mmisionari Mzee Mtoa Huduma | |
---|---|---|---|---|
Anaitwa na | Mmisionari Kijana Anayefundisha Rais wa Kanisa | Mmisionari Kijana Mtoa Huduma Rais wa Kanisa | Mmisionari Mzee Rais wa Kanisa | Mmisionari Mzee Mtoa Huduma Rais wa kigingi |
Anapangiwa na | Mmisionari Kijana Anayefundisha Mtume | Mmisionari Kijana Mtoa Huduma Mtume | Mmisionari Mzee Mtume | Mmisionari Mzee Mtoa Huduma Rais wa kigingi |
Anasimikwa na | Mmisionari Kijana Anayefundisha Rais wa kigingi | Mmisionari Kijana Mtoa Huduma Rais wa kigingi | Mmisionari Mzee Rais wa kigingi | Mmisionari Mzee Mtoa Huduma Rais wa Kigingi au mshauri |
Anaishi | Mmisionari Kijana Anayefundisha Mbali na nyumbani | Mmisionari Kijana Mtoa Huduma Nyumbani | Mmisionari Mzee Mbali na nyumbani au nyumbani | Mmisionari Mzee Mtoa Huduma Nyumbani |
Kiongozi wa Kanisa | Mmisionari Kijana Anayefundisha Rais wa misheni au rais wa eneo la kihistoria | Mmisionari Kijana Mtoa Huduma Rais wa kigingi | Mmisionari Mzee Misheni, hekalu, au rais wa eneo la kihistoria au Rais wa Eneo | Mmisionari Mzee Mtoa Huduma Rais wa kigingi |
Anaripoti kwa | Mmisionari Kijana Anayefundisha Rais wa misheni au rais wa eneo la kihistoria | Mmisionari Kijana Mtoa Huduma Viongozi wa huduma za misheni | Mmisionari Mzee Misheni, hekalu, au rais wa eneo la kihistoria,Rais wa Eneo; mkurugenzi wa kituo cha wageni, au idara ya Kanisa au meneja wa vifaa | Mmisionari Mzee Mtoa Huduma Meneja wa huduma za majukumu |
Mahitaji ya umri | Mmisionari Kijana Anayefundisha 18–25 (wanaume) | Mmisionari Kijana Mtoa Huduma 18–25 (wanaume) | Mmisionari Mzee 40 au zaidi kama ameoa/ameolewa au kama dada mseja | Mmisionari Mzee Mtoa Huduma 26 au zaidi |
24.3
Kujitayarisha na Kustahili Kuhudumu Misheni
Wamisionari watarajiwa wanahimizwa kuhudumu misheni kwa sababu ya upendo wao kwa Bwana na watoto Wake. Wanapaswa kuwa na uelewa wa maswali ya usaili wa mapendekezo ya kazi ya umisionari.
24.3.1
Kuongoka kwa Yesu Kristo
Wamisionari watarajiwa wanajitahidi kuimarisha uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake ya urejesho.
24.3.2
Kukidhi viwango vya Ustahili
Wamisionari watarajiwa wanajitahidi kuwa wenye kustahili wenza wa Roho. Hii inahitajika kwa ajili ya huduma ya umisionari yenye tija ( ona Mafundisho na Maagano 42:13–14).
24.3.2.1
Toba
Toba inahitaji kuonesha imani katika Kristo, kuwa na nia ya kweli, na kutii amri. Inajumuisha kuungama na kuacha dhambi. Kwa dhambi kubwa inahitaji kuungama kwa askofu au rais wa kigingi.
Mtu anayetubu anasamehewa na kufanywa msafi kupitia Upatanisho na neema ya Yesu Kristo. Bwana hakumbuki dhambi hiyo tena. (Ona Isaya 43:25; Yakobo 6:5; Alma 34:15–17; Helamani 5:10–11; Mafundisho na Maagano 58:42–43. Ona pia 32.1 katika kitabu hiki cha maelezo).
Mmisionari mteuliwa lazima awe ametubu dhambi kubwa kabla rais wa kigingi hajaweza kutuma mapendekezo yake (ona 32.6; ona pia 24.4.4). Mchakato wa toba unajumuisha muda wa kutosha kwa mtu kuonesha kupitia kuishi maisha ya haki kwamba amepokea roho ya Kristo kwa msamaha wa dhambi.
24.3.3
Afya ya Mwili, Akili, na Hisia
Kazi ya umisionari ni yenye changamoto Wamisionari vijana wanaofundisha lazima wawe wenye msimamo na uwezo wa kimwili, kiakili, na kihisia ili kufanyia kazi ratiba kamili ya umisionari.
24.3.4
Fedha
24.3.4.1
Kugharamia Wamisioari Vijana Wanaohudumu Mbali na Nyumbani
Wateuliwa vijana ambao wamejitayarisha kulingana na uwezo wao hawapaswi kucheleweshwa kuhudumumu kwa sababu ya kifedha. Wale wanaohitaji msaada wa kifedha ili kukamilisha ahadi ya mchango aliyoiweka wanaweza kuupokea kutoka kwa jamaa na marafiki.
Kama mahitaji yanaendelea kuwepo, askofu au rais wa kigingi anaweza kuomba waumini katika kata au kigingi kuchangia kwenye mfuko wa wamisionari wa kata.
Luba na matoleo ya mfungo visitumike.
Ahadi ya mchango wa kila mwezi. Wamisionari vijana wanaofundisha pamoja na familia zao wanachanga kiasi maalumu kila mwezi kusaidia kukamilisha gharama za programu za umisionari.
Michango inafanywa kwenye mfuko wa mmisionari wa Kata. Maaskofu wanahakikisha kwamba mifuko inachangiwa kila mwezi. Fedha inayozidi kiasi cha kila mwezi haipaswi kutolewa kabla ya mwezi husika. Fedha zilizochangwa kabla haziwezi kurudishwa kama mmisionari atarudi nyumbani kabla ya kumaliza muda wake.
Matumizi katika eneo. Kila mwezi, wamisionari vijana wanapokea fedha kutoka misheni kwa ajili ya chakula, usafiri, na matumizi mengine ya maisha. Fedha hizi ni takatifu. Wamisionari wanazitumia kwa malengo yanayohusiana na misheni pekee. Hazipaswi kutumika kwa matumizi binafsi, kuwekwa akiba, au kuwapelekea wanafamilia au watu wengine. Wamisionari wanarudisha misheni fedha zozote ambazo hawazihitaji.
Wamisionari wanatumia fedha binafsi ili kukidhi gharama zingine. Matumizi haya binafsi yanapaswa kuwa machache. (Ona Viwango vya Umisionari kwa Wafuasi wa Yesu Kristo, 4.8.)
24.3.4.2
Kugharamia Wamisioari Wazee Wanaohudumu Mbali na Nyumbani
Ahadi ya mchango wa kila mwezi. Wamisionari wazee wanaohudumu mbali na nyumbani wanachangia kwenye mfuko wa umisionari wa kata ya nyumbani kwao kila mwezi. Michango hii husaidia kukidhi gharama za nyumba na gari.
Maaskofu wanahakikisha kwamba mifuko inachangiwa kila mwezi. Fedha inayozidi kiasi cha kila mwezi haipaswi kutolewa kabla ya mwezi husika.
Gharama za Ziada. Kwa nyongeza kwenye ahadi za mchango wa kila mwezi, ambayo inasaidia kukidhi gaharama za nyumba na gari, wamisionari wazee lazima wagharamie kikamilifu gharama zingine zote, ikijumuisha chakula.
24.3.4.3
Kugharamia Wamisioari Wanaohudumu Nyumbani
Wamisionari wanaohudumu nyumbani wanawajibika kwa mahitaji yao yote ya kifedha.
24.3.4.4
Bima ya Afya na Matumizi
Wamisionari wote wanahimizwa kwa nguvu kutunza bima zao za afya zilizopo kama inawezekana, ikijumuisha wamisionari vijana wanaofundisha.
Wamisionari wanaohudumu nyumbani lazima walipie bima yao wenyewe ya afya na bima nyinginezo. Wamisionari wazee wanaohudumu mbali na nyumbani lazima pia walipie bima. Wamisionari wazee watakaohudumu nje ya nchi ya nyumbani kwao wanaweza kuwa na uwezo wa kupata bima kupitia Mpango wa Huduma za Afya kwa Wamisionari Wazee.
24.3.5
Wajibu wa Wanafamilia na Viongozi katika Kuwatayarisha Wamisionari
Wanafamilia, maaskofu, na viongozi wengine wananawasaidia vijana wajitayarishe kuhudumu misheni.
Wana familia na viongozi wanawahimiza waombaji wote wa umisionari kujifunza:
-
Kitabu cha Mormoni na maandiko mengine.
-
Hubiri Injili Yangu
-
Ulinzi kwa ajili ya kutumia Teknolojia.
Wanafamilia na viongozi wawanawasaidia wateuliwa wote waweke msimamo katika kufuata viwango vya umisionari Wanawahimiza wateuliwa wajifunze kitabu cha maelezo cha viwango vya umisionari ambavyo vinahusiana na majukumu yao yamkini:
-
Kwa ajili ya wamisionari vijana wanaofundisha; Viwango vya Mmisionari kwa Wafuasi wa Yesu Kristo
24.4
Kuwapendekeza wamisionari
24.4.1
Uchunguzi wa Afya
Wateuliwa wote wanatakiwa kufanyiwa uchunguzi wa afya na wataalamu ili kuona utayari wao kiafya.
24.4.2
Usaili na Fomu za Mapendekezo
Askofu na rais wa kigingi wanaendesha kwa ufanisi usaili wenye kuchunguza kiroho na wenye kuinua kwa kila mteuliwa. Wanatumia maswali ya usaili ya mapendekezo ya umisionari.
Askofu na rais wa kigingi.pia wanapitia upya taarifa kuhusu viwango vya ustahili na utayari wa afya katika Mfumo wa Mapendekezo ya Umisionari Mtandaoni. Askofu na rais wa kigingi hawaongezi viwango vyovyote vya ustahil. Wala hawabadili maswali ya usaili.
Kama askofu na rais wa kigingi wana mashaka kuhusu mteuliwa kukidhi viwango vya ustahili au kuhusu utayari wa afya, wanashauriana wote wawili na pamoja na mhusika mwenyewe. Kwa ruhusa ya wateuliwa vijana, wanaweza pia kushauriana na wazazi wake. Askofu na rais wa kigingi hawapeleki mapendekezo mpaka mtu awe ametubu dhambi yake kubwa (ona 24.3.2.1). Kutegemea na afya ya mtu ya mwili, akili, au hisia, wanaweza kujadiliana uwezekano wa kuteuliwa kama mmisionari wa huduma.
Katika hali za dharura wakati askofu au rais wa kigingi hawapatikani, anaweza kumruhusu mmoja wa washauri wake aendenshe usaili huu.
Katika wilaya, rais wa misheni au mshauri aliyepewa jukumu anasaili na kupendekeza wateuliwa wa umisionari. Marais wa wilaya hawaendeshi usaili huu.
24.4.4
Wale Wasioweza Kuhudumu kama Wamisionari wa Muda Wote
Wakati mwingine muumini anayetamani kuhudumu anaweza asiitwe kama mmisionari wa muda wote. Hii inawezekana kutokana na changamoto za kiafya, kutokufanikisha viwango vya ustahili, maswala ya kisheria au hali zingine. Rais wa kigingi anaweza kumtoa kwenye huduma ya umisionari wa muda wote.
24.5
Baada ya Kupokea Wito wa Misheni
Wamisionari wapya walioitwa wanahimizwa kusoma au kusoma tena Kitabu cha Mormoni kabla ya kuanza misheni zao. Wanafuata ushauri wa Mfalme Benjamini “jichungeni wenyewe, na mawazo yenu, na maneno yenu, na matendo yenu“ (Mosia 4:30).
24.5.1
Endaumenti ya Hekaluni na Huduma za Hekaluni
Kama wamisionari wapya walioitwa hawajapokea ibada ya endaumenti ya hekaluni wanapaswa kufanya hivyo kabla ya kuanza huduma ya umisionari pale inapowezekana (ona Mafundisho na Maagano 43:15–16; 105:33). Hii inajumuisha wamisionari wa huduma kama ni sahihi kwa hali zao.
Wamisionari wapya walioitwa hivi karibuni ambao wamepata endaumenti wanaweza kuhudumu kama wafanyakazi wa ibada za hekaluni kabla hawajaanza huduma ya umisionari ikiwa inafaa (ona 25.5
24.5.2
Mikutano ya Sakramenti
Uaskofu unawaalika wamisionari wapya walioitwa wazungumze katika mkutano wa sakramenti kabla ya kuanza misheni yao. Huu ni mkutano wa kawaida wa sakramenti. Fokasi inapaswa kuwa kwenye sakramenti na Mwokozi.
24.5.3
Kuwasimika Wamisionari
Rais wa kigingi cha nyumbani anamsimika kila mmisionari karibu kabisa na tarehe yake ya kuanza misheni. Katika hali ya dharura wakati askofu au rais wa kigingi hawapatikani, anaweza kumruhusu mmoja wa washauri wake awasimike wamisionari.
Rais wa misheni au mmoja wa washauri wake anawasimika wamisionari ambao wameitwa kutoka katika wilaya za misheni yake. Rais wa willaya hawasimiki wamisionari.
Kaka ambaye atahudumu mbali na nyumbani atakuwa amekwisha kupokea Ukuhani wa Melkizedeki kabla ya kusimikwa kama mmisionari. Kaka ambaye atahudumu kama mmisionari wa kutoa huduma anapaswa kuwa na Ukuhani wa Melkizedeki kama ni sahihi kwa hali yake.
24.6
Huduma Mbali na Nyumbani
24.6.2
Katika Eneo
24.6.2.5
Maombi ya Kuwasaidia Wengine Kifedha au Kimasomo au Uhamiaji
Wamisionari na familia zao hawapaswi kutoa msaada wa kifedha kwa ajili ya wale wanaoishi kule ambapo wamisionari wanahudumu, ikijumuisha msaada wa kifedha kwa ajili ya kusoma shule. Wala wamisionari na familia zao hawapaswi kufadhili watu wanaotaka kuhamia nchi zingine (ona 38.8.19
24.6.2.8
Kumbukumbu za Uumini na Zaka
Kata ya nyumbani ya mmisionari inabakiza kumbukumbu ya uumini. Kata ya nyumbani pia inaweka kumbukumbu ya hali yake ya zaka. Wamisionari hawalipi zaka kutokana na fedha ya msaada wanayopokea kutoka misheni. Hata hivyo wanalipa zaka kama wana kipato chochote binafsi.
24.6.3
Kurudi Nyumbani kutoka Misheni
24.6.3.1
Kurudi Nyumbani kama Ilivyopangwa Hapo Mwanzo
Wamisionari na washiriki wa familia zao hawapaswi kuomba kuachiwa mapema au nyongeza ya siku za huduma kwa matakwa yao.
Wamisionari vijana wanapaswa kusafiri kwenda moja kwa moja nyumbani baada ya misheni zao. Usafiri wowote kwenda mahala tofauti na nyumbani unatakiwa kuidhinishwa tu kama mmisionari amefuatana na angalau mmoja wa wazazi au mlezi.
Wamisionari hawapumzishwi mpaka wanaporipoti kwa rais wao wa kigingi. Wanafuata viwango vya umisionari hadi wakati watakapopumzishwa.
24.6.3.2
Kurudi Nyumbani Mapema
Baadhi ya wamisionari wanapumzishwa mapema kwa ajili ya afya, ustahili, au sababu zingine. Maaskofu na marais wa kigingi wanatoa msaada maalumu kwa wamisionari hawa waliorudi. Viongozi wanawasaidia wafanye yanayotakiwa ili kuwa na afya au kurudi kwenye huduma kama inawezekana.
24.7
Misheni za Huduma
24.7.1
Kutambua Fursa kwa ajili ya Wamisionari wa Huduma
Askofu, rais wa kigingi, na mmisionari wa huduma wanashauriana pamoja kutambua fursa za kuhudumu. Kwa ajili ya wamisionari vijana, kiongozi wa misheni ya huduma na wazazi wa mmisionari au walezi wanashiriki katika majadiliamo.
24.8
Baada ya Huduma ya Umisionari
24.8.2
Usaili wa Kumpumzisha Mmisionari
Rais wa kigingi huwapumzisha wamisionari na kuendesha usaili wa kupumzishwa. Katika wilaya, kwa kawaida rais wa misheni au mshauri aliyepewa jukumu anawapumzisha wamisionari.
Miongozo ifuatayo kwa ajili ya usaili huu inaweza kuwa ya msaada.
-
Watie moyo waendelee kama wafuasi wa maisha yote wa Yesu Kristo.
-
Wanawashauri wajenge juu ya tabia nzuri walizozikuza kama wamisionari
-
Wanawahimiza wafikiri na wajitayarishe kwa ajili ya siku za baadae, ikijumuisha elimu, na ajira kwa ajili ya wamisionari vijana.
-
Wanawahimiza waishi siku zote kwa kustahili kibali cha hekaluni.
24.8.4
Miito
Viongozi bila kupoteza muda wawapangie wamisionari waliopumzishwa hivi karibuni kazi za kuhudumu na miito Hii inajumuisha kifikiriwa kama wafanyakazi wa ibada za hekaluni kama inafaa (ona 25.5).
24.9
Nyezo kwa ajili ya Mapendekezo ya Mmisionari na Huduma
24.9.2
Tovuti
-
MissionaryRecommendations.ChurchofJesusChrist.org (inapatikana kwa viongozi wa eneo husikana wamisionari wateuliwa pekee)