“25. Kazi ya Hekaluni na Historia ya Familia katika Kata na Kigingi,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2013).
“25. 25. Kazi ya Hekalu na Historia ya Familia katika Kata na Kigingi,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla
25.
25. Kazi ya Hekaluni na Historia ya Familia katika Kata na Kigingi
25.0
Utangulizi
Kazi ya hekaluni na historia ya familia ni njia kwa ajili ya kuziweka pamoja na kuziunganisha familia kwa ajili ya milele (ona Mathayo 16:19). Kazi hii inajumuisha:
-
Kufanya maagano wakati tunapopokea ibada zetu wenyewe za hekaluni (ona Isaya 55:3; Mafundisho na Maagano 84:19-23).
-
Kuwagundua mababu zetu waliofariki na kufanya ibada kwa niaba yao katika hekalu ili nao waweze kufanya maagano na Mungu (ona Malaki 4:5–6; 1Wakorintho 15:29; Mafundisho na Maagano 128:15–18).
-
Kwenda hekaluni mara kwa mara, pale inapowezekana, ili kumwabudu Mungu na kufanya ibada kwa ajili ya watoto Wake (ona Luka 24:52–53; Mafundisho na Maagano 109:13–14
Taarifa zaidi zinapatikana kwenye “Mahekalu” na “Historia ya Familia” (Mada za Injili, topics.ChurchofJesusChrist.org).
25.1
Ushiriki wa Muumini na Kiongozi katika Kazi ya Hekaluni na Historia ya Familia
Waumini wa Kanisa wana fursa na wajibu wa kusaidia kuziunganisha familia zao kwa ajili ya milele. Wanajitayarisha wenyewe kufanya maagano pale wanapopokea ibada za hekaluni, na wanapojitahidi kuyashika maagano hayo.
Waumini wa Kanisa wanahimizwa kuwatambua jamaa zao waliofariki ambao hawajapokea ibada za hekaluni. Waumini kisha wanafanya ibada kwa niaba ya jamaa hao (ona Mafundisho na Maagano 128:18). Katika ulimwengu wa roho, watu binafsi waliofariki wanaweza kuchagua kukubali au kukataa ibada ambazo zimefanywa kwa niaba yao.
25.1.1
Jukumu Binafsi kwa ajili ya Kuhudhuria Hekaluni
Waumini wanaamua kwa ajili yao wenyewe lini na mara ngapi waabudu katika hekalu. Viongozi hawaweki idadi au utaratibu kwa ajili ya uhudhuriaji wa hekaluni.
25.2
Kupanga Kazi ya Hekaluni na Historia ya Familia katika Kata
25.2.1
Uaskofu
Uaskofu unaratibu kwa pamoja na urais wa akidi ya wazee na urais wa Muungano wa Usaidizi pale wanapoongoza juhudi za hekaluni na historia ya familia. Viongozi hawa wanashauriana pamoja mara kwa mara.
Uaskofu pia una madaraka yafuatayo kwa ajili ya kazi za hekaluni na historia ya familia katika kata:
-
Kuhakikisha kwamba mafundisho na baraka za kazi ya hekaluni na historia ya familia yanafundishwa kanisani.
-
Kuhakikisha kwamba kazi ya hekaluni na historia ya familia inaratibiwa katika baraza la kata na mikutano ya baraza la vijana la kata.
-
Kusimamia utaratibu wa kozi za matayarisho ya hekaluni (ona 25.2.8).
-
Kutoa vibali vya hekaluni ona sura ya 26).
25.2.2
Urais za Akidi ya Wazee na wa Muungano wa Usaidizi
Urais wa akidi ya wazee na wa Muungano wa Usaidizi wanaongoza juhudi za siku kwa siku za kazi ya hekaluni na historia ya familia katika kata (ona 8.2.4 na 9.2.4). Wanafanya kazi pamoja kuongoza juhudi hizi pamoja na baraza la kata, chini ya uratibu wa askofu.
Viongozi hawa wana majukumu yafuatayo:
-
Kuwasaidia waumini wajiandae kupokea ibada za hekaluni na kufanya maagano ya hekaluni.
-
Kuwahimiza waumini waabudu ndani ya hekalu mara nyingi kadiri hali zao zinavyoruhusu.
-
Kuwahimiza waumini wajifunze kuhusu mababu zao na wafanye ibada za hekaluni kwa niaba yao.
-
Kuongoza kazi ya kiongozi wa kazi za hekaluni na historia ya familia katika kata. Kama kiongozi huyu hajaitwa, mshiriki wa urais wa akidi ya wazee anachukua jukumu hili (ona 25.2.3).
Rais wa akidi ya wazee na rais wa muungano wa Usaidizi kila mmoja anamteua mshiriki wa urais ili asaidie kuongoza kazi ya hekaluni na historia ya familia katika kata. Washiriki hawa wawili wa urais wanafanya kazi pamoja. Wanahudhuria mikutano ya uratibu wa hekaluni na historia ya familia (ona 25.2.7).
25.2.3
Kiongozi wa kazi ya Hekaluni na Historia ya Familia katika Kata
Uaskofu unashauriana na rais wa kigingi kuamua ikiwa wamwite kiongozi wa kazi ya hekaluni na historia ya familia. Mtu huyu anapaswa kuwa mwenye Ukuhani wa Melkizedeki:
Kiongozi wa kazi za hekaluni na historia ya familia katika kata anausaidia urais wa akidi ya wazee na urais wa Muungano wa Usaidizi katika majukumu yao ya kazi za hekaluni na historia ya familia. Pia ana majukumu yafuatayo:
-
Anaongoza mikutano ya uratibu wa kazi za hekaluni na historia ya familia katika kata (ona 25.2.7).
-
Anawafundisha washauri elekezi wa kazi ya hekaluni na historia ya familia katika kata. Anaratibu juhudi zao za kuwasaidia waumini kwenye kazi ya hekaluni na historia ya familia.
-
Anafanya kazi na kiongozi wa kazi ya umisionari katika kata na wamisionari ili kuwasaidia wale wanaojifunza injili, waumini wapya, na wanaorudi kujiingiza katika kazi ya hekaluni na historia ya familia.
25.2.4
Washauri Elekezi wa Hekalu na Historia ya Familia katika Kata
Washauri elekezi wa Hekalu na historia ya familia wanahudumu chini ya maelekezo ya kiongozi wa kazi za hekaluni na historia ya familia wa kata au mshiriki wa urais wa akidi ya wazee mwenye wajibu huu. Uaskofu simamizi unawaita waumini hawa kuhudumia. Watu wazima na vijana wanaweza kuitwa.
Washauri elekezi wana majukumu yafuatayo:
-
Kuwasaidia waumini wapate uzoefu wa baraka za kuwagundua mababu zao na kufanya ibada za hekaluni kwa niaba yao.
-
Kuwasaidia waumini wajiandae kupokea ibada za hekaluni na kufanya maagano ya hekaluni.
-
Kushiriki katika mikutano ya uratibu ya hekaluni na historia ya familia (ona 25.2.7).
25.2.7
Mikutano ya Uratibu wa Kazi za Hekaluni na Historia ya Familia ya Kata
Mikutano mifupi ya uratibu isiyo rasmi katika kata ya hekalu na historia ya familia inafanyika mara kwa mara. Kama kiongozi wa hekalu na historia ya familia wa kata ameitwa yeye ndiye anaendesha mikutano hii. Ama sivyo, mshiriki wa urais wa akidi ya wazee ndiye anachukua jukumu hili la kuendesha.
Wengine ambao wanaalikwa ni pamoja na:
-
Washiriki wa urais wa Muungano wa Usaidizi na urais wa Akidi ya Wazee.
-
Msaidizi katika akidi ya makuhani.
-
Mshiriki wa urais wa darasa la wasichana wakubwa.
-
Washauri elekezi wa hekalu na historia ya familia.
Madhumuni ya mikutano hii ni:
-
Kupanga jinsi ya kuwasaidia washiriki maalumu wa kata kwenye kazi yao ya hekaluni na historia ya familia kama ilivyoombwa.
Mikutano hii inaweza kufanyika ana kwa ana au kwa kila mmoja kuwa mbali. Uratibu unaweza pia kutokea katika njia zingine, ikijumuisha kwa njia ya simu, ujumbe wa maandishi, na barua pepe.
25.2.8
Kozi ya Maandalizi ya Kwenda Hekaluni
Chini ya maelekezo ya askofu kozi ya maandalizi ya kwenda hekaluni inaweza kuandaliwa ili kuwasaidia waumini wajitayarishe kufanya maagano wakati watakapopokea ibada za hekaluni. Kozi hizi zinafanyika kando na mikutano ya kawaida ya Jumapili katika wakati unaofaa kwa waumini. Inaweza kufanyika kwenye nyumba ya mikutano au nyumba ya muumini.
Masomo na maelekezo kwa ajili ya kuanzisha kozi yapo kwenye Endowed from on High: Temple Preparation Seminar Teacher’s Manual. Washiriki wanapewa nakala za Preparing to Enter the Holy Temple. Kwa ajili ya kujifunza binafsi na Nyenzo za Masomo, ona temples.ChurchofJesusChrist.org.
25.4
Nyenzo za Historia ya Familia
25.4.1
Familia Yangu: Hadithi Ambazo Zinatuleta Pamoja
Familia yangu: Hadithi Ambazo Zinatuleta Pamoja huwasaidia watu wawagundue jamaa na mababu na kukusanya hadithi zao. Kijitabu hiki kinaweza pia kuwasaidia waumini waanze kutayarisha majina ya familia kwa ajili ya ibada za hekaluni.
Kijitabu kinaweza kupakuliwa kwenye ChurchofJesusChrist.org. Nakala halisi zinaweza kuagizwa kwenye Store.ChurchofJesusChrist.org.
25.4.2
FamilySearch.org na app ya FamilySearch
FamilySearch.org ni tovuti ya Kanisa kwa ajili ya kazi ya hekaluni na historia ya familia. Inaweza kuwasaidia watumiaji:
-
Kujenga muunganiko na mahusiano ya mti wa familia.
-
Kuwagundua mababu na hadithi zao.
-
Kushiriki na kuhifadhi hadithi za familia, picha, na historia.
-
Kutayarisha majina ya familia kwa ajili ya ibada za hekaluni.
app ya FamilySearch Tree na app ya FamilySearch Memories inawawezesha watu washiriki katika kazi ya hekaluni na historia ya familia kutoka kwenye vifaa vya mkononi.
25.5
Kupendekeza na Kuwaita Wafanyakazi wa Hekaluni
25.5.1
Kupendekeza Wafanyakazi wa Hekaluni
Wafanyakazi watarajiwa wa hekaluni wanatambuliwa katika njia zifuatazo:
-
Waumini waliotambuliwa na askofu au kiongozi mwingine wa kata
-
Waumini ambao wanamwendea askofu kuhusu kuhudumu
-
Waumini waliopendekezwa na rais wa hekalu, matroni, au kiongozi mwingine wa hekalu
-
Waumini wanaojitayarisha kwa ajili ya misheni au waliorudi hivi karibuni kutoka kwenye huduma ya umisionari (ona sura ya 24)
Majina ya wafanyakazi watarajiwa wa hekaluni kama yalivyotumwa kwa kutumia kifaa cha Kupendekeza Mfanyakazi wa hekaluni. Kifaa kinapatikana kwa maaskofu, marais wa vigingi, na urais wa hekalu.