“28. Ibada za Hekaluni kwa niaba ya Wafu,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“28. Ibada za Hekaluni kwa niaba ya Wafu,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla
28.
Ibada za Hekaluni kwa niaba ya Wafu
28.0
Utangulizi
Ibada zinazofanywa katika mahekalu zinafanya iwezekane kwa familia kuwa pamoja kwa milele yote na kupokea utimilifu wa furaha katika uwepo wa Mungu.
Ili watoto wa Baba wa Mbinguni waweze kurejea Kwake, kila mmoja wao lazima atubu, awe anastahili kupokea ibada za wokovu na kuinuliwa na aheshimu maagano yahusianayo na kila ibada.
Baba wa Mbinguni alijua kwamba wengi wa watoto wake hawatapokea ibada hizi wakati wa maisha yao ya duniani. Alitoa njia nyingine kwa wao kupokea ibada na kufanya Naye maagano. Ndani ya hekalu, ibada zinaweza kufanywa kwa niaba yao. Hii inamaanisha kwamba mtu aliye hai anapokea ibada kwa niaba ya mtu fulani ambaye amefariki. Katika ulimwengu wa roho, watu wanaweza kuchagua kukubali au kukataa ibada ambazo zimefanywa kwa niaba yao (ona Mafundisho na Maagano138:19, 32–34, 58–59).
Waumini wa Kanisa wanahimizwa kuwatambua jamaa zao walio fariki ambao hawajapokea ibada za wokovu na kuinuliwa. Waumini kisha wanafanya ibada hizo kwa niaba ya jamaa hao.
Kama waumini hawajatayarisha majina ya familia kwa ajili ya kazi ya hekaluni (ona 28.1.1), majina ya watu waliofariki wanaohitaji ibada yatatolewa hekaluni.
28.1
Maelekezo ya Jumla kwa ajili ya Kufanya Ibada kwa Niaba ya Wafu
Watu waliofariki wakiwa na umri wa miaka 8 au zaidi wakati wa vifo vyao, ibada zinaweza zikafanywa kwa niaba yao. Isipokuwa kama ilivyoelezwa katika 28.3, ibada kwa niaba ya wafu zinaweza kufanywa kwa ajili ya watu wote waliofariki alimradi siku 30 zimepita kutoka tarehe ya kifo chao kama mojawapo ya yafuatayo yatafanyika:
-
Jamaa wa karibu wa marehemu (mwenza ambaye hawakutalikiana, mtoto mtu mzima, mzazi au ndugu) atawasilisha jina kwa ajili ya ibada za hekaluni.
-
Ruhusa ya kufanya ibada inapokelewa kutoka kwa jamaa wa karibu wa marehemu (mwenza ambaye hawakutalikiana, mtoto mtu mzima, mzazi au ndugu).
Kama hakuna hata moja ya mambo yaliyotajwa hapo juu, ibada za hekaluni kwa niaba ya wafu zinaweza kufanywa miaka 110 baada ya marehemu kuzaliwa.
28.1.1
Kutayarisha Majina ya Watu Waliofariki kwa ajili ya Ibada za Hekaluni
Pale inapowezekana, taarifa zinazowatambulisha wanafamilia ambao ni marehemu zinapaswa kuingizwa kwenye FamilySearch.org kabla ibada za hekaluni hazijafanywa (ona 25.4.2).
28.1.1.1
Kuwasilisha Majina ya Wanafamilia
Wakati wa kuwasilisha majina kwa ajili ya ibada kwa niaba ya wafu hekaluni, waumini kwa kawaida wanapaswa kuwasilisha majina ya watu ambao ni jamaa zao pekee.
28.1.2
Nani Anaweza Kushiriki katika Ibada kwa niaba ya Wafu
Waumini wote ambao wana kibali hai cha hekaluni wanaweza kushiriki katika ubatizo na kuthibitishwa kwa niaba ya wafu. Waumini wenye endaumenti pamoja na kibali hai cha hekaluni wanaweza kushiriki katika ibada zote kwa ajili ya wafu. Ona 26.3
28.1.4
Kupanga Ratiba
Waumini wanaweza kuhitaji kufanya miadi kabla ya kufanya ibada kwa niaba ya wafu. Ona temples.ChurchofJesusChrist.org kwa ajili ya taarifa ya mawasiliano ya kila hekalu na vigezo vya kuweka ratiba.
28.2
Kufanya Ibada za Hekaluni kwa niaba ya Watu Waliofariki
Wakati wa kufanya ibada kwa niaba ya wafu, muumini anaweza kufanya hivyo kwa ajili ya mtu aliyefariki ambaye ni wa jinsia sawa katika kuzaliwa na jinsia ya muumini.
28.2.1
Ubatizo na Uthibitisho kwa niaba ya Wafu
Muumini yeyote ambaye ana kibali hai cha hekaluni anaweza kualikwa kuhudumu katika majukumu ya ubatizo. Baadhi ya majukumu yanaweza kujumuisha:
-
Kubatizwa na kuthibitishwa kwa niaba ya marehemu.
-
Kuwa kama shahidi kwa ajili ya ubatizo.
-
Kuwasaidia wanaobatizwa.
Wale wenye Ukuhani wa Melkizedeki na makuhani katika Ukuhani wa Haruni wanaweza kualikwa kufanya ubatizo kwa niaba ya wafu. Wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweza pia kualikwa kufanya uthibitisho kwa niaba ya wafu.
Wanaume wenye endaumenti pekee wanaweza kualikwa:
-
Kuhudumu kama mtunza kumbukumbu wakati wa ubatizo.
-
Kuhudumu kama mtunza kumbukumbu za uthibitisho.
28.2.2
Endaumenti (Pamoja na ibada ya Utangulizi)
Wakati wa kufanya endaumenti kwa niaba ya wafu sehemu ya ibada ya utangulizi ya endaumenti hufanywa na kurekodiwa tofauti (ona 27.2). Muumini yeyote aliyepokea endaumenti yake na mwenye kibali hai cha hekaluni anaweza kusimama kwa niaba ya marehemu ili apokee ibada hizi.
28.2.3
Kuunganishwa kwa Wenza na Kuwaunganisha Watoto kwa Wazazi Wao
Ndani ya hekalu, watu waliofariki wanaweza kuunganishwa kwa wenza wao ambao walikuwa wameoana wakati wakiwa hai. Watu waliofariki wanaweza pia kuunganishwa na watoto wao walio hai au waliofariki. Muumini yeyote aliyepokea endaumenti na aliye na kibali hai cha hekaluni anaweza kusimama kwa niaba ya marehemu kwa ajili ya ibada ya kuunganishwa.
28.3
Hali Maalumu
Sehemu hii inaelezea hali ambayo baadhi ya miongozo katika 28.1 inaweza isitumike.
28.3.1
Watoto Ambao Walikufa kabla ya Kuzaliwa (Ikijumuisha Kuharibika kwa Mimba)
Ibada za Hekaluni hazihitajiki kufanywa kwa niaba ya watoto wanaokufa kabla ya kuzaliwa. Kwa maelezo zaidi, ona 38.7.3.
28.3.2
Watoto Ambao Walikufa kabla ya Umri wa Miaka Minane
Watoto wadogo wamekombolewa kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo na “wameokolewa katika ufalme wa selestia wa mbinguni” (Mafundisho na Maagano 137:10). Kwa sababu hii, hakuna ubatizo au endaumenti inayofanywa kwa niaba ya mtoto aliyekufa kabla ya umri wa miaka 8. Hata hivyo, kuunganishwa kwa watoto na wazazi kunaweza kufanywa kwa watoto ambao hawakuzaliwa katika agano au hawakupokea ibada hiyo wakiwa hai (ona 18.1).