Vitabu vya Maelekezo na Miito
35. Utunzaji na Matumizi ya Nyumba za Mikutano


“35. Utunzaji na Matumizi ya Nyumba za Mikutano,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“35. Utunzaji na Matumizi ya Nyumba za Mikutano,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

watu wakisafisha madirisha na kutoa vumbi

35.

Utunzaji na Matumizi ya Nyumba za Mikutano

35.1

Dhumuni

Kanisa hutoa nyumba za mikutano ili kwamba wote wanaoingia waweze:

35.2

Wajibu na Majukumu

35.2.2

Maneja wa Vifaa vya Kanisa

Maneja wa vifaa aliyeajiriwa na Kanisa anasaidia kila kigingi kuendesha nyumba za mikutano. Yeye anapanga ukarabati mkubwa, usafi wa kina, na matengenezo ya kawaida ya jengo.

Kadiri inavyohitajika, maneja wa vifaa anasaidia kuwaelekeza wawakilishi wa majengo ya kigingi na kata juu ya jinsi ya kusafisha jengo na kufanya kazi zingine za eneo husika. Yeye anatoa maelekezo, nyenzo na vifaa.

Yeye anaweza pia kurejea upya gharama za jengo akiwa pamoja na uaskofu.

35.2.7

Uaskofu

Uaskofu (au mwakilishi wa jengo katika kata) anawafundisha waumini jinsi ya kutumia, kutunza, na kulilinda jengo. Uaskofu pia unagawa funguo za jengo kwa viongozi wa kata.

Wanahakikisha kwamba shughuli katika jengo na kwenye viwanja zinaendeshwa kwa usalama (ona 20.7).

Wanawasiliana na meneja wa vifaa wa Kanisa kuhusu matengenezo na mahitaji ya kiuendeshaji. Wanaweza pia kurejelea upya matumizi yanayohusika akiwa na meneja wa vifaa.

35.2.9

Mwakilishi wa Jengo la Kata

Uaskofu ndiyo unaamua ikiwa wanahitaji kumwita mwakilishi wa jengo la kata. Kama wanaamua kutoa wito huu, uaskofu unaweza kumwita mtu mzima nwanamume au mwanamke ambaye ni muumini. Kama mwakilishi wa jengo la kata haitwi, askofu anaweza kutoa wajibu huu kwa mmoja wa washauri wake, karani wa kata au karani msaidizi wa kata, au katibu mtendaji.

Mwakilishi wa jengo wa Kata anawasimamia waumini na watu wanaojitolea kulisafisha na kulitunza jengo. Yeye anawafundisha jinsi ya kufanya kila kazi kwa vifaa na nyenzo zilizopo.

35.3

Kutoa Nyumba za Mikutano

Nyumba za mikutano zinatofautiana kwa ukubwa, na aina kutokana na mahitaji na hali ya mahali husika. Nyumba ya mikutano inaweza kuwa imejengwa na Kanisa au nafasi iliyonunuliwa, nyumba ya muumini, shule ya eneo husika au kituo cha kijamii, nafasi iliyokodiwa, au uchaguzi mwingine ulioidhinishwa.

Viongozi wa eneo na viongozi wenyeji wanajitahidi kutumia kikamilifu nyumba za mikutano zilizopo na kuwa wenye hekima katika kupendekeza eneo la ziada.

35.4

Matunzo ya Nyumba za Mikutano

35.4.1

Kuzisafisha na Kuzitunza Nyumba za Mikutano

Viongozi wenyeji na waumini, ikijumuisha vijana, wanao wajibu wa kusaidia kuweka kila jengo liwe safi na katika hali nzuri.

Ratiba ya kusafisha haipaswi kuwa mzigo kwa waumini. Kwa mfano, kama kusafiri kwenda kwenye jengo ni changamoto, waumini wanaweza kulisafisha kama sehenu ya matukio ya wiki wakati wawapo tayari kwenye jengo.

35.4.2

Kuomba Ukarabati

Waumini wa baraza la kata na kigingi wanaweza kutoa taarifa ya mahitaji kwa ajili ya ukarabati wa jengo. Hii inaweza kufanywa kwa kutumia nyenzo ya Utoaji Taarifa juu ya Suala la Kifaa (FIR).

35.4.5

Usalama na ulinzi

Viongozi na waumini wanapaswa:

  • Kuacha wazi njia za kumbi, ngazi, milango ya kutokea, na vyumba vyenye vifaa vinavyotumika kwa ajili ya usalama wa kuingia na kutoka.

  • Kutotumia au kutunza vifaa hatarishi au vinavyoweza kuwaka moto katika majengo.

  • Kuanzisha na kufuata utaratibu wa kufunga na kufungua jengo.

  • Kuweka salama vifaa vinavyomilikiwa na Kanisa ili visiibiwe.

  • Kujua jinsi gani ya kufunga vitu kama vile bomba la maji, kuzima taa za umeme, gesi au mafuta.

Kadiri inavyohitajika, meneja wa vifaa anaweza kutoa ramani inayoonesha vifaa vya kuzima moto, vyombo vya huduma ya kwanza, na sehemu za kuzima vifaa. Taarifa za ziada kuhusu usalama zinapatikana katika “Taratibu za Usalama na za Ufungaji wa Milango” katika “Kutunza Nyumba za Mikutano” (Mwongozo wa Vifaa vya Nyumba ya Mikutano). Ona pia 20.7.

35.5

Sera juu ya Kutumia Mali za Kanisa

35.5.1

Kazi ya Sanaa

Nyumba za mikutano zinapaswa kuonesha jinsi ya kuwa na staha kwa Yesu Kristo na kushuhudia imani ya waumini Kwake. Sanaa inayomwonesha Yesu Kristo inapaswa kuwekwa katika eneo la ukumbi wa nyumba ya mkutano ili kusaidia kueleza kiini hiki cha imani.

35.5.2

Matumizi ya Jengo Ambayo Hayaruhusiwi

35.5.2.1

Matumizi ya Kibiashara

Mali za Kanisa haziwezi kutumika kwa madhumuni ya kibiashara. Kwa mfano, haiweza kutumika kuunga mkono aina yoyote ya biashara. Matumizi kama hayo hayafungamani na madhumuni ya mali za Kanisa. Inaweza pia kuleta mgongano na sheria za mahali husika au za taifa ambazo zinaweza kuruhusu msamaha wa kodi kwa mali za Kanisa.

Kuwakaribisha wazungumzaji au walimu ambao watawaajiri washiriki, kuwaomba wanunuzi au wateja watoe pesa au wanalipwa ada wakati wakitoa semina, masomo, (isipokuwa kwa ajili ya maelekezo binafsi ya piano au kinanda ; ona 19.7.2), Madarasa ya mazoezi, na shughuli zingine haziruhusiwa.

35.5.2.2

Madhumuni ya Kisiasa

Mali za Kanisa haiwezi kutumika kwa ajili ya madhumuni ya kisiasa. Matumizi haya hujumuisha kufanya mikutano au kampeni za kisiasa. Kanisa kisiasa halipendelei upande wowote (ona 38.8.30)

35.5.2.3

Matumizi Mengine

Matumizi mengine ya mali ya Kanisa ambayo hayaruhusiwi yanajumuisha:

  • Kufanya mazoezi ya riadha yaliyopangwa au matukio mengine ambayo hayafadhiliwi na Kanisa. Kwaya za jamii na ndoa za kiraia zinaweza kuwa na upekee (ona 38.3.4 kuhusu ndoa za kiraia).

  • Kuruhusu pawe kimbilio usiku kucha; (isipokuwa katika wakati wa dharura; ona 35.5.4).

  • Kuweka kambi au shughuli zingine ambazo zinajumuisha kulala usiku kucha.

Matumizi yafuatayo kwa kawaida hayaidhinishwi. Viongozi wenyeji wanawasiliana na meneja wa vifaa kama wanahisi jambo lenye upekee linahitajika.

  • Kupangisha au kukodisha majengo na mali za Kanisa

  • Kutumia mali kwa ajili ya kuandikisha wapiga kura wa kisiasa au sehemu za kupigia kura; jambo la upekee linaweza kufanywa kwa maombi ya maafisa wa serikali wakati kunapokuwa hakuna mbadala na tukio halitaleta madhara ya taswira au msimamo wa Kanisa usiopendelea upande wowote (ona 38.8.30)

35.5.4

Dharura

Wakati wa dharura rais wa kigingi anaamua ikiwa inafaa kufanya mikutano ya kata na ya kigingi. Anaweza pia kuruhusu majengo na mali za Kanisa kutumiwa na mashirika ya misaada ya maafa kwa ajili ya juhudi shirikishi.

35.5.10

Picha na Kurekodi Video Wakati wa Mkutano wa Sakramenti

Mikutano ya Sakramenti ni mikutano mitakatifu. Kwa sababu hii, hairuhusiwi kupiga picha au kurekodi mkutano wa sakramenti.

Kwa maelezo kuhusu kutangaza au kutiririsha mikutano ya sakramenti na mikutano mingine, ona 29.7.