“34. Fedha na Ukaguzi wa Hesabu,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).
“34. Fedha na Ukaguzi wa Hesabu,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla
34.
Fedha na Ukaguzi wa Hesabu
34.0
Utangulizi
Zaka na Matoleo vinaruhusu kanisa kuendeleza kazi ya Bwana ya wokovu na kuinuliwa (ona 1.2). Fedha hizi ni takatifu. Zinawakilisha dhabihu na imani za waumini wa Kanisa (ona Marko 12:41–44).
34.2
Uongozi wa Masuala ya Kifedha katika Kata
34.2.1
Uaskofu
Askofu ana majukumu yafuatayo kwa ajili ya fedha za kata. Ananaibisha baadhi ya kazi hii kwa washauri na makarani wake.
Askofu:
-
Anafundisha na kuwahamasisha waumini kulipa zaka kamili na kutoa matoleo kwa ukarimu (ona 34.3.).
-
Anahakikisha kwamba fedha za kata zinatumika vizuri na kutolewa maelezo sahihi (ona 34.5).
-
Anarejea upya taarifa za kifedha kila mwezi na anahakikisha kwamba masuala yoyote yanatatuliwa mara moja.
-
Anahakikisha kwamba viongozi wa vikundi na makarani wanajifunza wajibu wao kwenye fedha takatifu za Kanisa.
-
Anatayarisha na kusimamia bajeti ya mwaka ya kata ( ona 34.6.).
-
Anakutana na waumini wa kata kila mwaka kupokea tamko lao la zaka.
34.2.2
Karani wa Kata
Askofu anamteua karani wa kata au karani msaidizi wa kata ili kusaidia utunzaji wa kumbukumbu za kifedha za kata. Makarani kwa uangalifu wanafuata sera zilizopo ili kulinda fedha za Kanisa na kuhakikisha kwamba kumbukumbu za Kanisa ni sahihi.
Karani ana majukumu yafuatayo:
-
Kurekodi mbukumbu na kuweka benki fedha zozote zilizopokelewa akiwa na mshiriki wa uaskofu.
-
Anarejea upya taarifa za kifedha kila mwezi na anahakikisha kwamba masuala yoyote yanatatuliwa mara moja.
-
Anausaidia uaskofu kutayarisha bajeti ya mwaka ya kata (ona 34.6.1 na 34.6.2).
-
Anahakikisha kwamba waumini wanaweza kuingia kwenye taarifa zao za michango na kusaidia kama itahitajika.
Makarani wanapaswa kuwa na Ukuhani wa Melkizedeki na wawe na kibali hai cha hekaluni.
34.3
Michango
34.3.1
Zaka
Zaka ni mchango wa asilimia kumi ya mapato ya mtu kwa Kanisa la Mungu (ona Mafundisho na Maagano 119:3–4.); faida inaeleweka kumaanisha mapato). Waumini wote wenye kipato wanapaswa kulipa zaka.
34.3.1.2
Tamko Juu ya Zaka
Askofu anakutana na kila muumini wakati wa miezi michache ya mwisho wa kila mwaka ili kupokea tamko lao la zaka.
Waumini wote wanaalikwa kukutana na askofu ili:
-
Kutamka kwa askofu hali yao kama walipa zaka.
-
Kuhakikisha kumbukumbu za michango yao ni sahihi.
Wakati wowote inanapowezekana, washiriki wote wa familia, ikijumuisha watoto, wanapaswa kuhudhuria pamoja.
34.3.2
Matoleo ya Mfungo
Viongozi wa Kanisa wanawahimiza waumini kuishi sheria ya mfungo. Hii inajumuisha kutoa kwa ukarimu matoleo ya mfungo (ona 22.2.2).
Miongozo kwa ajili ya matumizi ya matoleo ya mfungo imetolewa katika 22.5.2.
34.3.3
Fedha za Umisionari
Michango kwa ajili ya fedha za umisionari kimsingi ni kutimiza ahadi za michango ya wamisionari wa kudumu kutoka katika kata husika.
Michango kwenye Mfuko Mkuu wa Umisionari inatumiwa na Kanisa katika juhudu zake za jumla za umisionari.
34.3.7
Michango Haiwezi kurudishwa
Wakati zaka na matoleo mengine yanapotolewa kwa Kanisa, inakuwa ni mali ya Bwana. Imewekwa wakfu Kwake.
Marais wa vigingi na maaskofu wanawataarifu wale wanaochangia zaka na matoleo kwamba michango hii haiwezi kurudishwa.
34.4
Usiri wa Zaka na Matoleo Mengine
Kiasi cha zaka na matoleo mengine yaliyolipwa na mtoa mchango ni siri. Ni askofu pekee na wale walioidhinishwa kushika au kuona michango hii ndiyo wanapaswa kuwa na uwezo wa kuingia kwenye taarifa hii.
34.5
Utunzaji wa Fedha za Kanisa
Rais wa kigingi na askofu wanahakikisha kwamba fedha yote ya Kanisa inatunzwa kwa usahihi. Uaskofu na makarani wanahimizwa kurejea video “ “Fedha Takatifu, Wajibu Mtakatifu” angalau mara moja kwa mwaka.
34.5.1
Kanuni za Mwenzi
Sera ya mwenzi inahitaji watu wawili —mshiriki wa uaskofu na karani, au washiriki wawili wa uaskofu—wawe wameshiriki kikamilifu wakati wa kurekodi na kusambaza fedha za Kanisa.
Viongozi wanapaswa kulinda na kamwe kutotoa nywila yao (ona 33.9.1.1.).
34.5.2
Kupokea Zaka na Matoleo Mengine
Bwana amewapa maaskofu uaminifu mtakatifu wa kupokea na kuwajibika kwa ajili ya zaka na matoleo mengine ya Watakatifu (ona Mafundisho na Maagano 42:30–33; 119). Ni Askofu na washauri wake pekee wanaweza kupokea zaka na matoleo mengine. Kwa vyovyote vile wake zao na washiriki wengine wa familia, makarani, au washiriki wengine wa kata hawapaswi kupokea michango hii.
34.5.3
Kuhakiki na Kurekodi Zaka na Matoleo Mengine
Michango inapaswa kuhakikiwa na kurekodiwa siku ya Jumapili michango hiyo inapopokelewa. Mshiriki wa uaskofu na karani au washiriki wawili wa uaskofu, wanafungua kila bahasha wakiwa pamoja. Wanathibitisha kwamba fedha zilizotiwa ndani ya bahasha ni sawa na kiasi kilichoandikwa katika fomu ya Zaka na matoleo mengine. Wanarekodi kila toleo vizuri. Kama fedha na kiasi kilichoandikwa vinatofautiana, wanawasiliana na mtoaji kwa haraka iwezekanavyo kutatua tofauti.
34.5.4
Kuweka Benki Zaka na Matoleo Mengine
Uwekaji benki unapaswa kutayarishwa baada ya kuhakikisha kiasi kilichorekodiwa kinafanana na fedha zilizopokelewa.
Mahali ambapo benki inapatikana kwa saa 24, mshiriki wa uaskofu na mtu mwingine mwenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweka fedha benki siku ile ile fedha inapofunguliwa na kuthibitishwa.
Mahali ambapo benki ya masaa 24 haipatikani na benki inafungwa siku ya Jumapili, askofu anamteua mwenye Ukuhani wa Melkizedeki kuziweka benki siku inayofuata ya kazi. Anapaswa:
-
Kuhakikisha kwamba fedha zinatuzwa sehemu salama mpaka zitakapowekwa benki.
-
Kupata risiti ya kuwekea fedha ikionesha tarehe na kiasi kilichowekwa.
34.5.5
Kulinda Fedha za Kanisa
Waumini wenye jukumu kwenye fedha ya Kanisa hawatakiwi kamwe kuiacha katika nyumba ya mikutano usiku kucha au kuiacha bila uangalizi wakati wowote kama vile wakati wa mikutano na shughuli.
34.5.7
Kusimamia Malipo ya Kigingi na Kata
Hakuna matumizi ya kigingi au kata yanayoweza kufanywa au kulipwa bila idhini ya afisa kiongozi.
Viongozi wawili walioidhinishwa lazima waidhinishe kila malipo. Mmojawapo lazima awe mshiriki wa urais wa kigingi au uaskofu. Ingawa washauri wanaweza kuidhinishwa kuruhusu malipo, rais wa kigingi au askofu lazima wapitie upya kila malipo. Viongozi hawapaswi kuidhinisha malipo kwao wenyewe.
Idhini ya maandishi ya rais wa kigingi inahitajika kabla ya askofu kutumia matoleo ya mfungo au kuidhinisha mipango ya askofu kwa ajili yake au familia yake. Idhini ya maandishi kutoka kwa mshiriki wa urais wa Eneo inahitajika kabla ya askofu kutumia matoleo ya mfungo au kuidhinisha mipango ya askofu kwa ajili ya rais wa kigingi au familia yake. Ona 22.5.1.2 kwa ajili ya miongozo.
Muumini akiomba kurudishiwa malipo aliyoyafanya anatoa risiti au ankara iliyoandikwa kwa mkono au ya kielektroniki. Pia anajumuisha dhumuni, kiasi, na tarehe ya manunuzi.
Ikiwa fedha zilitolewa kabla ya matumizi, muumini anawasilisha fomu ya maombi ya malipo, akionesha madhumini, kiasi na tarehe. Baada ya matumizi kufanyika muumini kisha (1)anatoa risiti au ankara kwa ajili ya fedha zilizotumika na (2) anarudisha fedha zozote zilizobakia. Fedha zilizorudishwa zinapaswa kurudishwa benki.
34.5.9
Kutunza Kumbukumbu za Kifedha
Kila kigingi na kata vinapaswa kuweka kumbukumbu za fedha kwa wakati na kwa usahihi.
Kwa maelezo kuhusu matumizi na udhibiti wa kumbukumbu na ripoti, makarani wanapaswa kurejea kwenye maelekezo kutoka makao makuu ya Kanisa au ofisi ya eneo. Kumbukumbu za kifedha zinapaswa kutunzwa kwa angalau miaka mitatu jumlisha mwaka wa sasa.
34.6
Bajeti na Matumizi
Programu ya marupurupu ya bajeti inatoa fedha za jumla za Kanisa ili kulipia shughuli na programu za kigingi na kata.
Shughuli nyingi zinapaswa kuwa rahisi na zenye gharama ndogo au bila gharama.
34.6.1
Bajeti za Kigingi na Kata
Kila kigingi na kata kinatayarisha na kuendesha bajeti ya mwaka. Rais wa kigingi anasimamia bajeti ya kigingi, na askofu anasimamia bajeti ya kata.
Miongozo imeorodheshwa hapa chini:
-
Rejea upya viwango vilivyotumika wakati wa mwaka uliopita kuhakikisha kwamba matumizi yanayojirudia yanazingatiwa.
-
Viombe vikundi vikadirie mahitaji ya bajeti zao kwa kina.
-
Unganisha bajeti kwa kutumia desturi zilizoidhinishwa za utengenezaji wa bajeti.
34.6.2
Marupurupu ya Bajeti
34.6.2.1
Mgawanyo wa Bajeti
Fedha ya bajeti inagawiwa kila robo ya mwaka kwa kuzingatia mahudhurio katika makundi yafuatayo:
-
Mkutano wa Sakramenti
-
Wavulana
-
Wasichana
-
Watoto wa msingi umri miaka 7–10
-
Vijana wakubwa waseja
Ni muhimu kutoa taarifa ya mahudhurio kwa usahihi na kwa wakati (ona 33.5.1.1).
34.6.2.2
Matumizi Sahihi ya Bajeti
Marais wa vigingi na maaskofu wanahakikisha kwamba migao ya bajeti inafanyika kwa busara.
Fedha ya bajeti ya kata au kigingi inapaswa kutumika kulipia shughuli zote, programu, vitabu vya kiada, na vifaa vyote.
34.6.2.3
Bajeti Iliyozidi
Fedha zilizozidi za bajeti hazipaswi kutumika. Fedha zilizozidi za kata zinapaswa kurudishwa kwenye kigingi.
34.7
Ukaguzi wa Hesabu
34.7.1
Kamati ya Kigingi ya Ukaguzi wa Hesabu
Rais wa kigingi anateua kamati ya ukaguzi wa hesabu ya kigingi. Kamati hii inahakikisha kwamba fedha za kigingi na kata zinatumika kulingana na sera za Kanisa.
34.7.3
Ukaguzi wa Fedha
Wakaguzi wa hesabu za Kigingi wanakagua kumbukumbu za kifedha za kigingi, kata, na vituo vya Historia ya Familia mara mbili kwa mwaka.
Afisa kiongozi wa kitengo na karani aliyepangiwa jukumu la fedha wanapaswa kuwepo ili kujibu maswali wakati wa ukaguzi.
34.7.5
Upotevu, Wizi, Ubadhirifu, au Matumizi Yasiyofaa ya Fedha za Kanisa
Rais wa kigingi au mwenyekiti wa kamati ya ukaguzi ya kigingi wanapaswa kutaarifiwa mara moja ikiwa:
-
Fedha za Kanisa zimepotea au kuibwa.
-
Kiongozi amefanya ubadhirifu au ametumia isivyofaa fedha za Kanisa.