Vitabu vya Maelekezo na Miito
37. Vigingi, Kata, na Matawi Yaliyowekwa Maalumu


“37. Vigingi, Kata, na Matawi Yaliyowekwa Maalumu,” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla (2023).

“37. Vigingi, Kata, na Matawi Yaliyowekwa Maalumu” Kurasa Zilizochaguliwa kutoka kwenye Kitabu cha Maelezo ya Jumla

Picha
watu wakila nje

37.

Vigingi, Kata, na Matawi Yaliyowekwa Maalumu

37.0

Utangulizi

Rais wa Kigingi anaweza kupendekeza kutengenezwa kwa vigingi maalumu, kata, na matawi ili kuhudumia waumini.

37.1

Kata na Matawi ya Lugha

Rais wa kigingi anaweza kupendekeza kuanzishwa kwa kata au tawi la lugha fulani kwa ajili ya waumini wa kigingi (1) ambao hawazungumzi lugha ya asili ya wenyeji wa pale au (2) wanaotumia lugha ya ishara.

37.7

Vikundi katika Vigingi, Misheni, na Maeneo

Vikundi ni mikusanyiko midogo iliyoidhinishwa ya waumini wanaosimamiwa na askofu, rais wa tawi, au rais wa misheni. Rais wa kigingi au misheni anaweza kupendekeza kuanzishwa kwa kikundi katika hali zifuatazo:

  • Usafiri kwa ajili ya wanaoweza kuwa waumini ili kukutana na kata au tawi ni mgumu.

  • Idadi ndogo ya waunimi wanazungumza lugha ambayo ni tofauti na wale walio katika kata au tawi.

  • Waumini katika jeshi wanahudumiwa vizuri zaidi kwa kuwa katika kikundi.

Kikundi lazima kiwe na angalau waumini wawili. Mmoja lazima awe kuhani anayestahili katika ukuhani wa Haruni au anayeshikilia Ukuhani wa Melkizedeki mwenye kustahili.

Katika kigingi, rais wa kigingi anamteua askofu au rais wa tawi kuanzisha na kusimamia kikundi. Katika misioni, rais wa misioni anamteua rais wa tawi kukianzisha na kukisimamia.

Rais wa kigingi, rais wa misheni, askofu, au rais wa tawi anamwita kiongozi wa kikundi na kumsimika. Kiongozi wa kikundi anapanga na kuongoza mikutano ya kikundi ambayo inajumuisha usimamiaji wa sakramenti.

Kiongozi wa kikundi hashikilii funguo za ukuhani, na haruhusiwi kufanya yafuatayo:

  • Kupokea zaka na matoleo.

  • Kumshauri muumini kuhusu dhambi kubwa.

  • Kutoa vizuizi rasmi au visivyo rasmi kwa muumini.

  • Kufanya kazi zingine ambazo zinahitaji funguo za ukuhani.

Kwa kufanana hasa, makundi yanatumia Programu ya Msingi ya Vikundi.

Kumbukumbu za uumini za washiriki wa vikundi zinawekwa katika kata au tawi ambalo linakisimamia kikundi hicho.

Makao makuu ya Kanisa hayatoi namba ya kitengo kwa vikundi.

Chapisha