Msaada kwa ajili ya Watoto na Vijana
Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza


“Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza,” Watoto na Vijana wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho: Mwongozo wa Utambulisho kwa ajili ya Wazazi na Viongozi ( 2019)

“Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza”

Ujumbe kutoka kwa Urais wa Kwanza

Wapendwa akina kaka na dada zetu,

Watoto na Vijana wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho ni wana na mabinti wapendwa wa Mungu. Wana uwezo wa kuwa na athari kubwa ulimwenguni.

Kanuni zilizofundishwa katika juhudi hii kwa ajili ya watoto na vijana zinatoa njia ya juu, iliyo tukufu kutia moyo kizazi kinachoinukia kumfuata Yesu Kristo na kutumia injili Yake katika maeneo yote ya maisha yao. Juhudi hii kubwa itajumuisha kujifunza injili, fursa ya huduma, maendeleo binafsi, na shughuli za kufurahisha. Juhudi hii inaanzia nyumbani. Wazazi wana jukumu takatifu la kuwafundisha watoto wao katika nuru na ukweli. Viongozi wa Kanisa wanatoa msaada wa thamani na mwongozo kwa watoto, vijana, na familia zao.

Tunawapenda. Tuna imani kubwa kwenu. Tunaahidi kwamba Baba yetu wa Mbinguni ataendelea kuwabariki na kuwaidhinisha mnapowaongoza na kuwaelekeza watoto Wake katika imani.

Urais wa Kwanza na Akidi ya Mitume Kumi na Wawili

Picha
Mwokozi

Chapisha