Msaada kwa ajili ya Watoto na Vijana
Utangulizi


“Utangulizi,” Watoto na Vijana wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho: Mwongozo wa Utambulisho kwa ajili ya Wazazi na Viongozi (2019)

“Utangulizi”

Utangulizi

Wakifanya kazi pamoja, wazazi na viongozi husaidia watoto na vijana kuzidisha uongofu wao, kuwa wafuasi wanaostahili wa Bwana Yesu Kristo, na kuwa wanaume na wanawake waadilifu kupitia:

  • Kujifunza injili ambako kunatia msukumo kujitolea binafsi.

  • Huduma na shughuli ambazo zinaadilisha mwili na nafsi.

  • Maendeleo binafsi ambayo yanaleta ukuaji unaotosheleza.

Kanuni zinazoongoza na majukumu ya jumla yaliyofupishwa katika kijitabu hiki yanatoholeka. Hakuna njia moja tu sahihi ya kuzitumia. Baadhi ya mawazo na mifano inapatikana katika mtandao kwenye ChildrenandYouth.ChurchofJesusChrist.org. Tafuta msukumo kujua kile kinachofaa zaidi kwa kila mtu binafsi (ona “Adjust and Adapt”).

Kizazi Kinachoinukia

Picha
vijana wakitabasamu

Manabii wamesema kwamba kizazi hiki cha watoto na vijana ni miongoni mwa walio wema mno Bwana aliowaleta duniani (ona Russell M. Nelson, “Tumaini la Israeli,” ibada ya vijana ulimwenguni kote, Juni 3, 2018, 16). Wana uwezo wa kuwa na athari kubwa ulimwenguni. Wamealikwa kusaidia kukusanya Israeli pande zote za pazia. Mtazamo wa juu zaidi, mtakatifu unahitajika kuwajali na kuwahudumia. Mtazamo huu utawasaidia watoto na vijana:

  • Kufahamu utambulisho na lengo lao la milele.

  • Kuongeza uongofu wao kwa Yesu Kristo, kufanikisha kuweka injili Yake katika mioyo yao na kuwatia moyo kuchagua kumfuata Yeye.

  • Kutimiza Wajibu wa Ukuhani wa Haruni.

  • Kushiriki kwa pamoja katika kazi ya Wokovu.

  • Kujiendeleza kibinafsi kwa msaada wa wazazi na viongozi wakisaidia pale inapohitajika.

  • Kuwa wenye kustahili kuhudhuria hekaluni na kuwa na furaha ya kudumu kwenye njia ya agano.

Pale watoto na vijana wanapopokea ufunuo kwa ajili ya maisha yao, wanapojenga mahusiano yenye kiini cha injili, na kutumia uhuru wa kuchagua wanapokua, watafanikiwa katika kukamilisha malengo haya.

Jitahidi Kumfuata Mwokozi

Katika ujana wake, Yesu alihitaji kujifunza utambulisho Wake mtakatifu na kazi Yake maalumu, kama vile ambavyo kila mtoto wa Mungu lazima afanye. “Aliendelea katika hekima na kimo, akimpendeza Mungu na wanadamu” (Luka 2:52). Alikua katika njia iliyo na usawa, na ndivyo watoto wote na vijana wanaweza kukua.

Wasaidie watoto na vijana kumleta Mwokozi katika vipengele vyote vya maisha yao—si tu siku ya Sabato. Wanapojitahidi kumfanya Yesu Kristo kiini cha maisha yao, Anaahidi kumtuma Roho Mtakatifu kuwa mfariji wao na kiongozi wao.

Kiukamillifu, kumfuata Mwokozi kunaanzia nyumbani. Viongozi wa Kanisa wanaweza kutoa msaada muhimu kwa ajili ya watu binafsi na familia.

Inayolenga Nyumbani

Picha
familia imekaa kwenye benchi

Wazazi wanapanga uzoefu wa familia na mazungumzo kufundisha injili ya Yesu Kristo na kukidhi mahitaji ya kipekee ya kila mtoto. Hii inatokea wakati familia zinapofanya kazi na kucheza pamoja katika njia ambazo zinafundisha ujuzi muhimu, kuimarisha tabia, na kutoa fursa za kukua.

Himiza ukuaji.

  • Sali kwa ajili ya mwongozo. Baba wa Mbunguni anawajua watoto wako na atakusaidia kuwafundisha.

  • Wasaidie watoto wako kutafuta na kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu.

  • Onesha upendo na mara kwa mara wasifie watoto wako katika juhudi zao kufanya yaliyo mema na kwa ajili ya tabia kama za Kristo unazoziona ndani yao.

  • Tafuta fursa za kuwatumikia wengine kama familia.

Toa Mwongozo

  • Wasaidie watoto wako kuona jinsi gani wanaweza kutumia injili katika nyanja zote za maisha yao.

  • Waongoze watoto wako na wahimize kuweka malengo na mipango yao wenyewe.

  • Wasaidie kupata suluhisho lao wenyewe la matatizo.

  • Toa tegemeo, msaada, na tia moyo kadiri mnavyoendelea.

Zungumza na Viongozi

Wasiliana na walimu na viongozi kuamua jinsi wanavyoweza kuwasaidia vyema watoto wako. Kuwa mwangalifu kutovunja ujasiri wa watoto wako au kuwaaibisha.

Inayosaidiwa-na Kanisa

Inayolenga-Nyumbani (Familia)

Picha
ikoni ya kujifunza injili
Picha
ikoni ya huduma na shughuli
Picha
ikoni ya maendeleo binafsi

Inayosaidiwa-na Kanisa (Viongozi)

Wajibu wa Kanisa unajumuisha kufundisha injili ya Yesu Kristo, kutoa ibada, na kusaidia nyumbani. Viongozi na walimu wanawasaidia wazazi kwa kuanzisha mahusiano yenye nguvu, yenye malezi kwa watoto na vijana wanaowahudumia.

Zungumza na Wazazi

  • Wasiliana na wazazi katika njia isiyo rasmi kugundua jinsi ya kuwasaidia watoto wao. Shiriki uwezo unaouona.

  • Waulize kile wanachotegemea watoto wao watapitia na kujifunza katika akidi za Ukuhani wa Haruni, katika madarasa ya Wasichana, na kwenye shughuli.

Wakati wazazi ni waumini wasioshiriki kikamilifu Kanisani:

  • Eleza kwa wazazi juhudi hii ya kusaidia watoto na vijana, na waulize kama na kwa jinsi gani wangependa watoto wao wahusishwe.

  • Waulize watoto au vijana aina gani ya msaada wangependa.

  • Ongea na baraza la kata kuhusu jinsi ya kujumuisha wazazi mara nyingi kadiri inavyowezekana.

Wasaidie Watoto na Vijana

  • Wasaidie watoto na vijana kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu.

  • Waulize kile wanachotaka kujifunza na kupata uzoefu katika darasa na kwenye shughuli.

  • Wahimize kuchukua nafasi ya mbele katika kupanga na kuongoza shughuli.

  • Wasaidie wenye Ukuhani wa Haruni katika kutimiza majukumu ya akidi.

Kujifunza Injili

Picha
familia ikijifunza pamoja

Nyumbani

Kujifunza maandiko na kuomba kibinafsi na kifamilia kutasaidia watoto na vijana kuhisi na kutambua ushawishi wa Roho Mtakatifu na kujifunza kumpenda Mwokozi. Watu binafsi na familia wanahimizwa kutumia Njoo Unifuate—Kwa Ajili ya Watu Binafsi na Familia na maneno ya manabii wanaoishi ili kujifunza injili ya Yesu Kristo.

Kanisani

Watoto na Vijana wanakutana pamoja kujifunza injili ya Yesu Kristo. Watoto wanajifunza injili kupitia maelekezo ya darasani na wakati wa kuimba wa Msingi. Vijana wanajifunza mafundisho katika madarasa na akidi. Watoto na Vijana wanaalikwa kushiriki kile wanachojifunza nyumbani na kutumia injili katika maisha yao.

Huduma na Shughuli

Picha
Wanaojitolea kwenye Mikono ya Usaidizi ya Mormoni

Nyumbani

Huduma na shughuli vinaanzisha tabia za kiadilifu za kila siku, kujenga mahusiano ya kifamilia, kufundisha ujuzi wa maisha, kuendeleza sifa kama za Kristo, na kusaidia watoto na vijana kukua. Huduma na shughuli za familia zinaweza kulenga kwenye mahitaji ya mtu binafsi na familia na kutoa fursa za kutumia kanuni za injili katika uzoefu wa kila siku.

Kanisani

Huduma—ikijumuisha wenye Ukuhani wa Haruni kuhudumu katika ibada ya sakramenti—na shughuli za mara kwa mara hutoa fursa ya kukusanyika, kujifunza ujuzi mpya, kukamilisha jukumu zito, na kujenga mahusiano yenye kiini katika injili na makundi rika pamoja na viongozi. Shughuli hizi huwasaidia watoto na vijana kukua kiroho, kijamii, kimwili, na kiakili na kutoa huduma yenye maana kwa wengine. HudumiaTu (JustServe.org) ni nyenzo yenye thamani kwa ajili ya fursa za huduma ya jamii.

Shughuli zinazofanyika kwa siku kadhaa kwa ajili ya vijana zinajumuisha mikutano Kwa ajili ya Nguvu ya Vijana (KNV), kambi, na mikusanyiko mingine. Shughuli hizi zinaweza kusaidia vijana kuzidisha hamu yao ya kumfuata Mwokozi, kuwatoa kwenye utaratibu wao wa kawaida, na kuwasaidia kuona kwamba wao ni sehemu ya kundi kubwa la vijana wanaoshiriki malengo ya haki.

Picha
KNV Brazili 2016

Maendeleo Binafsi

Nyumbani

Watoto na vijana wanachagua kile wanachoweza kufanya ili kukua na kujifunza kumfuata Mwokozi. Wazazi wanaweza kuwasaidia kutambua jinsi ambavyo tayari wanakua na wapi wanaweza kuhitaji kujiboresha. Shughuli zote, ikijumuisha kanisa, shule, urafiki, michezo, sanaa, kazi, na vivutio vingine binafsi vinaweza kusaidia watoto na vijana kumfuata Yesu Kristo.

Kanisani

Viongozi wanampenda na kumhudumia kila mtoto na kijana na kufahamu mahitaji yao na mambo wanayoyapenda. Kupitia mahusiano ya upendo, viongozi wanaweza kutoa ushawishi wa kipekee na wenye nguvu kusaidia na kuhimiza watoto na vijana katika huduma yao na ukuaji wao binafsi.

Rekebisha na Tohoa

Picha
wasichana wawili wakitabasamu

Kila mtu binafsi, familia, na mkutano ni wa kipekee. Kinachofanya kazi vizuri kwa mmoja kinaweza kisifanya hivyo kwa mwingine. Fanya kile kinachofanya kazi kwa ajili ya familia, darasa, akidi, au kata yako. Zungumza kuhusu fursa zako na wasiwasi, na tafuta ufunuo wa jinsi ya kurekebisha juhudi hii ili kusaidia watoto na vijana kibinafsi kufikia uwezo wao mtakatifu.

Kwa mfano, watoto na vijana watatofautiana katika jinsi wanavyokaribia ukuaji binafsi: aina, nambari, na marudio ya malengo, vilevile kiasi gani cha msaada wanahitaji, vinapaswa kuamuliwa kibinafsi. Madarasa na akidi pia yanabadilika kukidhi mahitaji. Kwa nyongeza, aina na marudio ya shughuli inaweza kubadilika kulingana na hali ya mahali pale.

Fanya iwe rahisi. Fanya kile kinachowezekana.

Motisha na Utambuzi

Picha
mvulana mdogo amesimama darasani

Motisha

Watoto na vijana kwa kawaida watakuwa na motisha wanapohisi kupendwa, kukua, kuboreka, na kumhisi Roho Mtakatifu katika maisha yao. Wakati mabadiliko na ukuaji vinakuwa vitu vigumu kwao, watie moyo kutafuta njia za kushinda changamoto au kubadili mipango yao. Mahusiano yenye nguvu na kuaminiana na wazazi, viongozi, na makundi rika yanaweza kuwapa nguvu kuendelea kujaribu.

Utambuzi

Pale watoto na vijana wanapoendelea, sifia juhudi zao na watie moyo. Wape fursa kushiriki kile wanachojifunza, na sherehekea ukuaji wao. Kwa nyongeza, watoto wote na vijana wanaweza kupokea vitu kama pete au medali kuwakumbusha kwamba wao ni sehemu ya kundi la ulimwenguni kote linalojitahidi kumfuata Yesu Kristo. Pale watoto na vijana wanapotimiza malengo ya kiroho, kijamii, kimwili, na kiakili, wanaweza kupokea nembo za ziada.

Chapisha