Msaada kwa ajili ya Watoto na Vijana
Wajibu


“Wajibu,” Watoto na Vijana wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho: Mwongozo wa Utambulisho kwa ajili ya Wazazi na Viongozi ( 2019)

“Wajibu”

Wajibu

Nyumbani na Wazazi

familia ikitembea nje

Jukumu langu ni lipi?

Kuwa mfano wa uadilifu kwa watoto wako. Wafundishe jinsi ya kukua katika nyanja zote za maisha yao. Tafuta njia za kuwasaidia kujifunza furaha ya kutunza maagano, kugundua vipaji vipya, na kufanya mambo magumu. Isaidie familia yako kuwa karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo na kuishi injili katika maisha ya kila siku.

Nifanye nini?

Waache watoto wako wajue jinsi gani unavyowapenda. Husika katika maisha yao. Kwa sala tambua mahitaji yao binafsi na panga mafunzo ya injili na shughuli ili kushughulikia mahitaji hayo. Mara kwa mara shiriki ushuhuda wako pamoja nao. Zungumza na viongozi kuhusu jinsi wanavyoweza kusaidia kuwakimu watoto wako.

Naanzia wapi?

Endelea kuzungumza na kuwasikiliza watoto wako. Omba kuhusu jinsi unavyoweza kuwasaidia. Wasaidie kugundua na anza kufanyia kazi maeneo ya kujifunza wanayoyapenda. Anza, au endeleza sala ya familia, mafunzo ya injili, fursa za huduma, na shughuli kuwasaidia watoto wako kukua.

Viongozi wa Msingi na Walimu

familia ikisali pamoja

Jukumu langu ni lipi?

Wapende na waimarishe watoto. Wasaidie wazazi katika kuwasaidia watoto kuhisi upendo wa Baba wa Mbinguni kwa ajili yao, kuelewe injili ya Yesu Kristo, kuhisi na kugundua ushawishi wa Roho Mtakatifu, na kujitayarisha kufanya na kutunza maagano matakatifu.

Nifanye nini?

Hakikisha kwamba madarasa ya Msingi na muda wa kuimba huwasaidia watoto kumhisi Roho, kuongezeka katika imani, na kuhisi shangwe ya injili ya Yesu Kristo katika maisha yao. Pamoja na nyanja za ukuaji ziliyopendekezwa katika Luka 2:52 kama mwongozo, panga huduma na shughuli za kufurahisha na zinazohusisha na shughuli ambazo zinajenga shuhuda, kuimarisha familia, na kukuza umoja na ukuaji binafsi.

Naanzia wapi?

Anza kuwajua watoto na familia zao, na hudumia mahitaji yao. Kama Urais wa Msingi, kwa sala uliza jinsi unavyoweza kuwasidia walimu wako, viongozi wa muziki, na viongozi wa shughuli kuwasaidia watoto kumfuata Mwokozi.

Viongozi wa Wasichana

wasichana wakiandika

Jukumu langu ni lipi?

Wasaidie wazazi na uaskofu katika kuwaelekeza na kuwatia moyo wasichana kuelewa utambulisho wao kama mabinti wa Mungu, kujiandaa kwa maagano ya hekaluni, na kutimiza malengo yao matakatifu. Ongoza urais wa madarasa pale wanapoelekeza, kuwahudumia, na kuwatumikia washiriki wa madarasa yao.

Nifanye nini?

Weka mfano kama mfuasi wa Yesu Kristo. Ongoza urais wa madarasa wanapopanga kwa sala na kusaidia kufundisha masomo kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Wasichana. Watie moyo kuongoza katika kupanga na kutekeleza huduma na shughuli ambazo zitawasaidia wasichana kukua katika nyanja zote za maisha yao. Toa msaada wa ziada kwa wasichana wanaouhitaji.

Naanzia wapi?

Wajue wasichana kibinafsi. Zungumza na wasichana, wazazi wao, na uaskofu kuhusu jinsi unavyoweza kusaidia ukuaji wa wasichana. Sali kujua jinsi unavyoweza kusaidia urais wa madarasa yako kufanikiwa katika miito yao.

Viongozi wa Ukuhani wa Haruni

Jukumu langu ni lipi?

Wasaidie wazazi na uaskofu katika kuwaandaa wavulana kwa ajili ya kutawazwa kwenye ofisi za ukuhani, maagano ya hekaluni, misheni, na majukumu matakatifu. Watie moyo kuelewa lengo lao na utambulisho wao kama wana wa Mungu. Ongoza urais wa akidi wanapoelekeza, kutumikia, na kuhudumia washiriki wa akidi zao na wanapohudumu katika ibada ya sakramenti.

Nifanye nini?

Weka mfano kama mfuasi wa Yesu Kristo. Ongoza urais wa akidi pale wanapotumia funguo zao, wanapohudumu katika ibada ya sakramenti, na kwa sala panga na saidia kufundisha masomo kutoka Njoo, Unifuate—Kwa Ajili ya Wavulana. Wasaidie kupanga na kutekeleza huduma na shughuli ambazo zitawasaidia wavulana kukua katika maeneo yote ya maisha yao. Waache waongoze. Toa msaada wa ziada kwa wavulana wanaouhitaji.

Naanzia wapi?

Tumia muda pamoja na wavulana. Wajue na wapende kibinafsi. Zungumza na uaskofu, wavulana, na wazazi wao kuamua jinsi unavyoweza kuwasaidia wanapokua na kuwa zaidi kama Mwokozi. Sali kujua jinsi unavyoweza kuwasaidia urais wa akidi yako kutumia funguo zao na kufanikiwa katika miito yao.

Walimu wa Shule ya Jumapili

vijana wakisoma maandiko

Jukumu langu ni lipi?

Jitahidi kuwasaidia vijana kuja kwa Kristo kwa kujifunza na kufuata mafundisho Yake. Fundisha vijana kuelewa, kushiriki, na kuishi injili ya Yesu Kristo.

Nifanye nini?

Weka mfano kama mfuasi wa Yesu Kristo, na wasaidie vijana kujenga imani yao. Watie moyo kujifunza maandiko nyumbani—kibinafsi na pamoja na familia zao. Wasaidie kuandaa na kufundisha kanuni za injili. Waalike kutumia kile wanachojifunza kwenye maendeleo yao binafsi.

Naanzia wapi?

Jitahidi kufundisha kama Mwokozi alivyofundisha. Wajue vijana kibinafsi. Sali kujua jinsi unavyoweza kuwasaidia kukua ili wawe zaidi kama Mwokozi. Waimarishe washiriki wa darasa na wazazi wao katika juhudi za kujifunza na kufundisha injili kanisani na majumbani mwao.

Uaskofu, na Urais wa Darasa na Akidi

mtu akisalimiana na mvulana kwa mikono

Jukumu lao ni nini?

Uaskofu ni urais wa Ukuhani wa Haruni katika kata na unawajibika na wasichana na wavulana. Urais wa akidi za Ukuhani wa Haruni unafanya kazi kwa funguo zilizotunukiwa wakati marais wa akidi wanaposimikwa. Urais wa darasa la Wasichana hufanya kazi chini ya mamlaka ya ukuhani baada ya wao kusimikwa na mshiriki wa uaskofu.

Wanafanya nini?

Marais wanapaswa kujitahidi kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo pale wanapomsaidia kila mshiriki wa darasa au akidi kuhisi kupendwa na kugundua shangwe ya kuishi injili. Chini ya maelekezo ya uaskofu, urais wa akidi huongoza wenye Ukuhani wa Haruni pale wanapohudumu katika ibada ya sakramenti. Urais wa akidi na darasa huongoza katika kukusanya Israeli katika pande zote za pazia na kuwatunza wale wenye uhitaji.

Wanaanzia wapi?

Marais wanajifunza majukumu yao kutoka kwa Bwana na kutoka kwa viongozi wao. Wanasali kwa ajili ya akidi au washiriki wa darasa na kuweza kujua mahitaji yao. Wanawasaidia katika kuwa wafuasi wa Yesu Kristo. Wanashauriana pamoja kuhusu masomo gani, shughuli, na huduma ambazo zitabariki na kuiwamarisha vijana na kuleta umoja kwenye madarasa yao au akidi zao.