Kujenga Ufalme katika New Caledonia
Vijana wakubwa katika New Caledonia na ulimwenguni kote wanaitikia wito wa kutumikia na kuwa viongozi katika Kanisa.
“Nafasi ya kutumikia ni moja ya baraka kubwa ya uumini katika Kanisa.”1 Kama kijana mkubwa, kutumikia Kanisani kunaweza kuwa fursa ya kusisimua kwa ajili ya ukuaji, uongozi na kuimarisha misuli yako ya kiroho. Lakini pamoja na majukumu mengine yote ujana mkubwa unayoleta, kutumikia wakati mwingine kunaweza kuwa na changamoto—hasa katika maeneo ambapo Kanisa bado ni changa. Kwa mfano, nini unafanya wakati unapoitwa kuwa rais wa Wasichana wa kigingi, unajaribu kujiandaa kutumikia misheni wakati pia ukihudhuria elimu ya juu na kusaidia kuratibu chuo na, ndiyo, una miaka 21 tu?
Kwa maeneo mengi ya Kanisa, hii sio hali ya kushangaza. Katika New Caledonia, himaya ndogo ya ng’ambo ya Ufaransa yenye waumini wa Kanisa takribani 2,400, vijana wakubwa waumini mara nyingi hupewa majukumu makubwa katika kujenga ufalme wa Bwana. Rais Russell M. Nelson aliwahi kusema kwa vijana wakubwa,: “Ninyi ni viongozi wa baadaye wa Kanisa la Bwana! Je, mko tayari kushika hatamu ya uongozi?”2 Kwa sababu ya uhitaji na kwa sababu ya upendo walionao wa Mwokozi, vijana wakubwa ulimwenguni kote wako tayari kutumikia na kuongoza katika Kanisa.
Katika Huduma Yake kwa Maisha
Kwa vijana wengi wakubwa wa New Caledonia, misheni zao zinasaidia kuwaandaa kwa maisha yote ya huduma ya Kanisa. Syoelanne (Syo) Ulivaka alipokea wito wa kutumikia kama mshauri wa pili katika uaskofu wiki moja tu baada ya kupumzishwa kutoka kwenye misheni yake ya muda wote. “Nilikuwa punde nimemaliza misheni yangu,” Syo anasema. “Nilikuwa nimechoka, na nilikuwa nimejiambia, sasa ninakwenda kupumzika.” lakini bado alikubali wito. “Nilitambua nitakwenda Bwana atakakotaka mimi niende. Niko katika huduma yake—si tu kwa miaka miwili, bali kwa maisha yote.”
Tangu alipotumikia katika uaskofu, Syo sasa ameoa, ana mtoto na amehamia kata nyingine. Lakini anaendelea kutumikia na kutimiza miito yake ya Kanisa.
Mzee Earl C. Tingey, Kiongozi Mkuu mstaafu Mwenye Mamlaka wa Sabini, aliwaambia vijana wakubwa: “Wito wa Kanisa ni moja ya baraka ya kupendeza zaidi unayoweza kufurahia katika hatua yako ya maisha. Una mengi ya kuchangia kwenye kata au tawi ambapo unaishi. Talanta na ujuzi wako ni muhimu kwa Kanisa linalokua.”3 Syo siye mvulana mkubwa pekee katika kisiwa ambaye ujuzi wake umewekwa kwenye matumizi ili kusaidia Kanisa linalokua—vijana wengine wakubwa wanatumikia katika karibia kila nafasi kwenye ngazi ya kata na kigingi. Syo anasema, “Tunajaribu kuleta mambo tuliyojifunza kwenye misheni zetu ili kuimarisha kigingi na kata zetu.” Vijana hawa wakubwa wanafanya dhabihu nyingi ili kuimarisha ufalme katika nchi yao ya asili, lakini kama Syo anavyosema, “kile tunachotoa dhabihu mara nyingi ni muda wetu.”
Baadhi ya vijana wakubwa wana miito miwili au hata mitatu. “Hiyo inaweza kuwa baraka kwao, lakini inaweza pia kuwa mzigo,” anasema Syo, pale wengi wanapopambana kuwekea usawa mahitaji ya ujana na majukumu yao ya Kanisa. “Ni vigumu kufanya kila kitu kwa wakati mmoja.” lakini Siyo alikuta kwamba anapomweka Bwana kwanza, yaliyosalia yalikuwa rahisi kuyakamilisha. Anasena, “Bwana amesaidia kwenye kila kitu kingine—shule, kupata mke—yote yalikuwa katika mikono ya Bwana.”
Wakati Ujao wa Kanisa
Manabii na mitume wana maoni yenye nguvu kuhusu uwezo na huduma ambayo vijana wakubwa wanaweza kutoa Kanisani: “Tunahitaji mioyo na nafsi zenu zote. Tunahitaji vijana wakubwa wachangamfu, wenye kufikiria, wenye ari ambao wanajua jinsi ya kusikiliza na kujibu minong’ono ya Roho Mtakatifu.”4
Vijana wakubwa katika New Caledonia na kote ulimwenguni wanaitikia wito huu wa kitume. Wanatambua kwamba wao ni wakati ujao wa Kanisa na wanachagua kutumikia katika njia yoyote wanayoweza. Wanahimizana wao kwa wao katika miito yao. Wanafanya kazi na wamisionari. Wanashiriki injili na kuwaalika rafiki zao kanisani. Wanatoa ushauri kwa vijana katika kata zao na kuwapa motisha kutumikia misheni. Wanasafiri umbali mrefu kuhudhuria hekaluni. Wanawafundisha wasio waumini katika familia zao. Na juhudi zote hizi zinajenga ufalme.
Syo anatambua kwamba, linapokuja suala la kumtumikia Bwana, “Sisi ni nyenzo Zake.” Katika nyakati hizi za ukuaji wa Kanisa, Bwana atawaita Watakatifu wa umri wote, kila mahali, kukubali majukumu ya kujenga na kuimarisha ufalme Wake. Je tuko tayari kuitikia wito huo?