2020
Je, Maisha Yako ya Nyuma Yanakuzuia?
Aprili 2020


Je, Maisha Yako ya Nyuma Yanakuzuia?

Mwokozi tayari amelipa gharama. Shika mkono Wake na endelea kusonga mbele.

Muda mfupi uliopita, askofu wangu aliitaka kata yetu kufikiria baadhi ya unyonge au dhambi ambazo tungeweza kistiari kuziacha kwenye meza ya sakramenti ili Yesu Kristo aziondoe. Kuna dhambi nilizozibeba katika maisha yangu yote ya ujana wangu mkubwa ambazo nimejaribu kuzishinda lakini sikuweza kuzishinda kupitia sala au utashi wangu mwenyewe. Licha ya ukuaji wangu miaka yote, nilijua nilihitaji kuzishinda ili niendelee mbele.

Jumapili baada ya changamoto ya askofu, niliamua kwamba nitaiacha moja tu ya dhambi zangu kwenye meza ya sakramenti, ishara ya kimwili ya Mwokozi na dhabihu Yake ya upatanisho. Nilipokuwa najiandaa kushiriki sakramenti, nilikumbuka kamba kitambaa kinachoifunika kiliwakilisha sanda yake, na mkate na maji viliwakilisha mwili Wake na damu.

Kwa moyo safi na nia njema, nilirudia tena maagano yangu ya ubatizo na niliomba moyoni mwangu, nikimwomba Baba wa Mbinguni msaada na kufanya ahadi kuiacha nyuma yangu dhambi hii. Kisha kitu fulani kilitokea ambacho kamwe sikukitegemea: tamaa yangu ya kufanya dhambi iliondoka kabisa. Nilijaribu hii mara nyingine zaidi, na jambo lilelile lilitokea kwa dhambi zingine. Je, ilikuwa ni vyema zaidi kuwa mkweli?

Kufuganisha Mapenzi Yangu na Yake

Wiki iliyofuata, nilijua ni dhambi gani nilitaka kuiacha kwenye meza ya sakramenti, lakini sikujihisi tayari kuiacha. Nikiangalia nyuma, nilitambua kwamba moyo wangu haukuwa katika sehemu ambapo ulitakiwa uwe. Nilikuwa si mkweli vya kutosha kuamua kutofanya dhambi. Lakini nilitambua kiasi gani dhambi inamuumiza Baba wa Mbinguni. Nilijua nilihitaji kufuganisha mapenzi yangu na Yake na kulenga maisha yangu kumzunguka ili kuwa huru. Kwa hiyo nilifanya kwa uwezo wangu wote kufanya hiyo iwe uhalisia.

Niliepuka majaribu yoyote ambayo yangeweza kuongoza kwenye dhambi hii. Nilibadilisha jinsi nilivyosoma maandiko yangu kila siku na kwa kweli niliyatafakari na kuyatumia kwenye maisha yangu. Nililenga kwenye kuwa mkweli katika uamuzi wangu wa kubadilika, na nilitafuta kila siku kutafuta mapenzi ya Bwana juu yangu. Nilimweka Yeye wa kwanza, kwa sababu nilijua nisingeweza kuiacha dhambi hii nyuma yangu bila nguvu ya Upatanisho wa Mwokozi. Kwa kuendelea kumweka Yeye kwanza, niliweza kuiacha dhambi hii kwenye meza ya sakramenti. Hatimaye nilikuwa huru kutoka jambo fulani ambalo lilikua limenizuia kwa miaka mingi.

Kupitia mchakato huu, nilikua karibu zaidi na Baba wa Mbinguni na Mwokozi. Niliwafikiria wakinitazama kwa miaka yote hii kwa subira na upendo—wakijua, hatimaye, ningeacha dhambi ambazo kiroho zilizuia maendeleo yangu. Na wakati nilipokuwa tayari kuziacha, Yesu Kristo angekuwa pale kuniinua—kunishika mkono na kunipa msamahaa na nguvu. Tayari alitoa njia kwa ajili yangu kuwa huru kutoka kwenye dhambi zangu kupitia Upatanisho Wake. Alilipa gharama kwa ajili ya udhaifu, makosa, na dhambi zangu. Nilihitaji tu kumwamini Yeye.

Unaweza Kusonga Mbele

Wakati wa kipindi hiki, nilisoma baadhi ya maneno kutoka kwa Mzee Richard G. Scott (1928–2015) wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ambayo yalinipa mimi msukumo mdogo niliouhitaji: “Kama maisha yako katika mvurugano na unahisi kutokuwa na raha na kutokuwa na thamani … , usiwe na wasiwasi. Yeye tayari anajua kuhusu yote hayo. Anakungojea wewe upige magoti kwa unyenyekevu na kuchukua hatua chache za kwanza. Sali kwa ajili ya nguvu. … Sali kwamba upendo wa Mwokozi umiminwe ndani ya moyo wako.”1

Wakati tulipoimba “I Stand All Amazed” (wimbo wangu ninaoupenda) wiki iliyofuata, kila neno liliashiria ukweli; Kwa kweli nilishangazwa—kwa hofu kwamba mambo niliyopambana nayo kwa zaidi ya muongo mmoja yalikuwa yameondolewa. Kwa hofu kwamba kupitia nguvu ya Upatanisho wa Mwokozi, ningeweza kusonga mbele. Kwamba anaweza kuponya dhambi zote na majeraha na kutoacha alama yoyote nyuma. Kwamba sikuhitaji kuzuiwa na mambo yangu yaliyopita.

Bado nina mengi sana ya kujifunza na kuyashinda, lakini maisha yangu yako kwenye njia ya uhakika. Ninajihisi furaha zaidi na amani. Ninaonesha shukrani zaidi. Ninakaribia sana na kuimarisha ushuhuda wangu wa Baba wa Mbinguni na Mwokozi. Kila siku ambayo nachagua kujaribu tena, ninasogea hatua moja karibu zaidi na Wao na mtu Wanaejua ninaweza kuwa.

Muhtasari

  1. Richard G. Scott, “True Friends That Lift,” Ensign, Nov. 1988, 77.