2020
Kutumia Jina Kamili la Kanisa Ilikuwa Vigumu lakini Ilistahili
Aprili 2020


Kutumia Jina Kamili la Kanisa Ilikuwa Vigumu lakini Ilistahili

Kufuata maelekezo ya nabii kulionekana rahisi, lakini ilionekana kuchukua juhudi zaidi kuliko nilivyotarajia.

Wakati Rais Nelson alipozungumza kuhusu kutumia jina sahihi la Kanisa katika mkutano mkuu wa Oktoba 2018, ujumbe wake ulikuwa wazi kwangu: “ ni amri ya Bwana. …

“… Kuondoa jina la Bwana kutoka kwenye Kanisa la Bwana ni ushindi mkubwa kwa Shetani” (“Jina sahihi la Kanisa,” Liahona, Nov. 2018, 87, 88).

Nilitambua kwamba nilihitaji kufikiri upya jinsi ninavyofanya mazungumzo na wale wanaonizunguka, ikiwa ni pamoja na wateja fulani kazini kwangu ambao walikuwa wamezoea kuniita “Mmormoni” na muumini wa Kanisa la “Mormoni.”

Nikiwa nimeweka msimamo kutumia jina kamili la Kanisa, nilisubiri fursa iliyofuata ya kudai uumini wangu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Hakika vya kutosha, fursa hiyo ilikuja, tena katika mazingira ya biashara. “Nyie Wamormoni ni watu wakarimu sana,” mteja muhimu aliniambia. “Vema, asante,” nilijibu. “Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, tunaamini sisi sote ni kaka na dada.” Kisha mazungumzo yakaendelea na kila mmoja akizungumza kuhusu ukarimu wa “Wamormoni.”

Japokuwa nilikuwa nimefanya sehemu yangu kwa kusema jina kamili la Kanisa, bado nilihisi kuna jambo halikuwa sawa. Rafiki zangu na wafanyakazi wenzangu bado walinichukulia mimi kama sehemu ya “Kanisa la Mormoni” na si lazima kama mfuasi wa Kristo, achilia mbali kama muumini wa Kanisa la Kristo lililorejeshwa.

Je, Hilo Lilistahili kuwa Tatizo?

Kwa miingiliano kadhaa iliyofuata kuhusu imani yangu, nilijikuta nikilazimisha kwa sababu ya ugumu wa kusema jina kamili, refu la Kanisa mara nyingi katika mazungumzo yale yale. Kila niliyezungumza naye alionekana kunipa maelezo ya kupuuza. Na mazungumzo bado daima yalifokasi juu ya “Wamormoni.”

Nilijaribu kufanya miingiliano yangu kuwa kiasi yenye uasilia zaidi. Lakini hili liligeuka kuwa gumu zaidi kuliko nilivyotarajia, hasa na watu ambao sikutaka kuwaudhi. Sikutaka kuwa mpole au kuridhika kuhusu kuishi imani yangu, lakini sikutaka pia kuwa mkali, kwani wengi wa watu hawa kipindi cha nyuma waliniita “Mmormoni,” na mimi nilikubali. Nilisikia pia waumini wengi wa Kanisa bado wakijiita wao pamoja na wengine “Wamormoni” kwenye mikutano mbalimbali na katika mazingira mengine.

Nilijikuta nikijiuliza ikiwa kutumia jina kamili la Kanisa ilikuwa hasa muhimu hivyo katika utaratibu mkuu wa mambo. Alama ya “Mormoni”, hata hivyo, ni chanya katika akili za watu wengi—kuwa “Mmormoni” daima imekuwa rasilimali kwangu. Lakini katika kupitia tena mazungumzo ya Rais Nelson, nilivutiwa kwamba hili hasa lilikuwa muhimu, hata kama ilisababisha ugumu katika mazungumzo. Kwa hiyo nilijiwekea msimamo mpya.

Nafasi ya Kushuhudia juu ya Kristo

Wakati uliofuata nilipotakiwa kutumia jina kamili la Kanisa, nilikuwa nimemtembelea rafiki kwenye kanisa la imani nyingine. Mtu fulani aliniijia na kwa tabasamu angavu aliniuliza kama mimi ni Mmormoni. “Mimi ni muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, ndiyo” nilisema. Alianza kuniuliza maswali kadhaa, kila moja likianza na: “Je, Kanisa la Mormoni linaamini … ?” Na kila mara, nilianza jibu langu kwa kifungu: “Katika Kanisa la Kristo lililorejeshwa, tunaamini …”

Majibizano hayo yaliendelea mara nne au tano. Wakati alipogundua kwamba sikuwa nikikubali jina la “Mormoni,” aliniuliza kwa kuweka wazi, “Je wewe si Mmormoni?”

Hivyo nilimuuliza ikiwa alijua Mormoni alikuwa nani—hakujua. Nilimwambia kwamba Mormoni alikuwa nabii, mwanahistoria, mkuu wa jeshi, na mwanasiasa katika Amerika ya kale. Ninapata heshima kuhusishwa na mtu ambaye alikuwa amejitolea kwa kiasi kikubwa kwenye huduma ya Mungu na ya watu wengine.

“Lakini,” niliendelea, “Mormoni hakufa kwa ajili ya dhambi zangu. Mormoni hakumwaga damu yake kwa ajili yangu au kuteseka Gethsemane au kufa msalabani. Mormoni sio Mungu wangu. Yesu Kristo ni Mungu wangu na Mwokozi wangu. Yeye ni Mkombozi wangu. Na ni kwa jina Lake kwamba ninataka kujulikana siku ya mwisho, na ni kwa jina Lake kwamba ninatumaini kujulikana leo.”

Nilihisi hakikisho la Roho akinisaidia katika ushuhuda huu mfupi kwa mtu mgeni niliyekutana naye. Baada ya muda mfupi wa unyamavu, alisema, “Kwa hiyo wewe ni Mkristo?”

“Ndiyo, mimi ni Mkristo,” nilijibu, “na muumini wa Kanisa la Kristo lililorejeshwa.”

Kutafuta kufuata maelekezo ya nabii kulionekana rahisi, lakini ilionekana kuchukua juhudi zaidi kuliko nilivyotarajia. Bado si mkamilifu kwenye kufuata kila kitu ninachoagizwa kufanya. Lakini katika kila hali, sasa ninahakikisha kutumia jina kamili la Kanisa.

Nina shukrani kwa ajili ya Roho ambaye ninamsikia wakati ninaposhuhudia kwa wengine juu ya Mwokozi wangu na uumini wangu katika Kanisa Lake. Na sasa nina njia kuu ya uhalisia ya kushuhudia juu Yake na Kanisa Lake la Urejesho wakati wowote ninapoulizwa kuhusu kuwa “Mmormoni.”