Maktaba
Mazungumzo na Dada Neill F. Marriott


Mazungumzo na Dada Neill F. Marriott

MZEE NELSON

Dada Marriott, mimi nimeshapata nafasi ya mahusiano ya mapema na wewe na mume wako mpendwa, David. Lakini wengi wa washiriki wa Kanisa hawakujui vyema kama ninavyokujua. Je! U tayari kutuambia kidogo kuhusu kuongoka kwako katika Kanisa?

DADA MARRIOTT

Asante sana. Mzee Nelson. Nilipokuwa na umri wa miaka 22 nilihamia Boston, Massachusetts kwa ajili ya kazi. Na huko nilikutana na washiriki wawili wa Kanisa na mmoja wao alisema, “Mimi ni Mmormoni.” Wenzi wangu wa chumba nami tulisema, “Mmormoni ni nini?”

Basi mmoja wao akasema, “Vyema, ungependa sisi tuwalete marafiki kadha katika flati yako ili waweze kukuambia zaidi kuhusu imani yetu?” Basi, karibu juma moja baadaye walileta marafiki wawili na hii ilikuwa mara ya kwanza kuwaona wamisionari Wamormoni. Na acha niseme nilikuwa na maswali mengi, mengi sana.

Lakini, waliendelea kuja na mwishowe walifikia mpango wa wokovu. Na bado nakumbuka usiku huo vyema kabisa. Wao walisema, “Kabla ya kuja hapa, wewe uliishi katika ulimwengu wa roho na Baba yako wa Mbinguni. Wewe ni binti Yake wa kiroho.” Mzee Nelson, mimi nilitambua maneno hayo. Yalikuwa yanafahamika kwangu. Nilikuwa sijayasikia katika maisha haya lakini najua nilishayasikia mapema mahali fulani.

Mwishoni mwa mkutano huu mmoja wa washiriki alisema na kunena, ningependa kuuliza swali moja la mwisho” Aliniangalia na kusema, “Neill, unahisi vipi kuhusu Kitabu cha Mormoni?” Na maneno yaliyotoka mdomoni mwangu yalikuwa, “Nafikiria ni cha kweli.” Nilishangaa sana kusikia maneno haya yakielea hewani hapo. “Nafikiria ni cha kweli.” Na yeye, kwa hekima sana, hakunirukia, alisema tu, “Vyema, basi, kwa ufahamu huu, utafanya nini?” Na mimi nilimwahidi kwamba usiku huo nitaomba kwa uaminifu. Nilipiga magoti chini katika chumba changu cha kulala, na kusema tu, “Baba wa Mbinguni, ikiwa hili ndilo Kanisa la Mwokozi la pekee na la kweli ulimwenguni, mimi nitabatizwa. Nilikuwa nahitaji tu kujua ni kweli.” Na mara moja sauti ikaja katika kichwa changu, au katika moyo wangu ikisema: Ni kweli. Hivyo tu. Na nikasimama na kusema, “Ni kweli!” kwa kushangazwa kabisa na hili jibu la ajabu. Kisha nilimpigia simu rais wa misheni asubuhi iliyofuata na kusema, “Halo, mimi nahitaji kubatizwa.”

MZEE NELSON

Ee, bila shaka alifurahia kusikia kutoka kwako. Je! Una hisia zozote kuhusu wahenga wako?

DADA MARRIOTT

Vyema, inashangaza umeniuliza hivyo kwa sababu, wito wangu wa kwanza katika Kanisa ulikuwa umeongozwa sana. Askofu aliniita mimi, na akaniuliza ikiwa ningekuwa mshiriki wa kamati ya nasaba.

Niliwaandikia bibi zangu wawili ambao walikuwa katika umri wa miaka 80. Nakumbuka ikiwa wiki kadhaa, lakini barua zilikuja na kulikuwa na sanduku la viatu limejaa picha na majina nyuma yake na maandishi katika vijikaratasi vidogo. Kwa hivyo, nilikaa chini kwenye sakafu katika chumba changu cha kulala na nikaanza kuweka mabunda ya familia, familia ya Dade, familia ya Hill, familia ya Ray, familia ya Fielding. Na nilipokuwa nikizichagua, ghafula nilitazama juu … sikuona chochote, lakini chumba kilijaa. Nilihisi kilikuwa kimejaa watu ambao walikuwa wanapendeza na wenye furaha. Na ningeweza kuhisi uwepo wao kwa jinsi fulani.

Nafikiria, katika miaka miwili au mitatu ya kuwa mshiriki, nilishughulikia karibu majina 70, nilipata karibu majina 70 kufanyiwa endaumenti katika hekalu. Niliyatuma kwa jamii ya David, mume wangu. Nitaongea kuhusu David katika muda usio mrefu.

MZEE NELSON

Ee, tafadhali. Tuambie David ni nani.

DADA MARRIOTT

David ni mtu maalumu. Yeye alikuwa mmoja wa washiriki ambao waliniuliza ikiwa ninataka kujua zaidi kuhusu Kanisa. Na tulioana katika Hekalu la Salt Lake miezi 13 tu baada ya ubatizo wangu.

MZEE NELSON

Ala! Si hayo ni marupurupu mazuri ya kuwa mshiriki mmisionari?

DADA MARRIOTT

Ndio. Mimi napendekeza.

MZEE NELSON

Vyema, wewe na David mna familia nzuri sasa. Tuambie kuhusu familia yako.

DADA MARRIOTT

Vyema, sisi tuna watoto 11 na wakati tulioana tulitaka kuwa na familia, kuanzisha familia, na watoto walikuja tu. Wao walikuwa roho teule.

MZEE NELSON

Una ushauri wowote kwa akina dada zetu wa ajabu ambao wanajaribu kushughulika kama mke, mama na mtumishi mwaminifu wa Bwana, mfuasi wa Bwana?

DADA MARRIOTT

Vyema, naipenda mikutano ya Kanisa---najua kwamba hii inaonekana kuwa kitu kigeni---lakini moyo wangu halisi upo katika nyumba yangu. Na kwa hivyo kwa kila wito, na ilionekana kujenga mmoja juu ya mwingine, nilitunza nyumba yangu kwanza. Mikutano fulani nilikosa kuhudhuria lakini haikuwa muingiliano katika maisha ya familia. Bila shaka, ilinifunza kuwa mama bora.

MZEE NELSON

Wewe ni mama bora kwa sababu umekita nanga katika injili.

DADA MARRIOTT

Hiyo ni kweli kabisa.

MZEE NELSON

Vyema, sisi tuna shukrani kwa sababu yako, kwa huduma ambayo wewe umetoa na ambayo bado utatoa.

DADA MARRIOTT

Asante.