Maktaba
Kiongozi wa Misheni wa Kata katika Kazi ya Wokovu


Kiongozi wa Misheni wa Kata katika Kazi ya Wokovu

CHRIS EUBANKS

Sisi tulikuwa katika miongoni mwa mojawapo wa ukame mbaya tuliyowahi kupata katika miaka 50.

Kukiwa pamoja na ukame hamna maendeleo mengi yanayofanyika katika juhudi za umisionari katika kigingi chetu. Najua katika kata yetu, sisi hatujakuwa na ubatizo wa mwongofu katika miaka mitatu.

RAIS BOWMAN

Tulikuwa na hofu kama urais kuhusu kile kilichokuwa kinatendeka, na tulishauriana pamoja. Kwa hivyo tulituma barua, tukiwauliza washiriki kuungana pamoja katika mfungo kwa kazi ya umisionari na kwa ajili ya ukame.

CHRIS EUBANKS

Tulipokea barua hii na kigingi chote na vigingi vingine jirani vilifunga na kazi ya umisionari mara ikaanza kuongezeka.

Milango ya gharika kwa njia fulani ilifunguka na kila mtu alikuwa akijihusisha.

Mzee Bowen wa wale Sabini alikuja katika eneo hili na kutoa mafunzo ya umisionari. Mojawapo ya matamshi ya kwanza ambayo alitoa yalikuwa “wamisionari wa muda wote katika kata yenu au katika tawi lenu wako hapo tu kuwasadia ninyi katika kazi ya umisionari.”

Ni kazi yetu kama washiriki wa Kanisa kuwa hai katika kujishughulisha katika kazi na kuwaalika marafiki zetu na familia kanisani.

RAIS BOWMAN

Haiwezi kutendeka bila wamisionari wa muda au washiriki wakiwa wamejishughulisha nayo. Hilo ndilo lengo letu, kuwawezesha hao viongozi wa misheni wa Kata na Baraza la Kata kuwa wao ndio wanaosukuma hiyo kazi, na wala si wamisionari wa muda wote.

ASKOFU

Kazi ya kiongozi misheni wa kata ni kukutana na askofu pamoja na baraza la kata na kuweka Mpango wa Misheni wa Kata kisha kujaribu na kuendesha huu mpango ambao ni kuwasaidia washiriki kupata na kufanya urafiki na watu kwa wamisionari wa muda ili kuwafunza.

CHRIS EUBANKS

Kitu kimoja ninachojaribu kufanya, pamoja na msaidizi wa kiongozi wa misheni wa kata na wamisionari ni kujaribu kujaza kikamilifu kalenda ya wamisionari. Kwa sababu juhudi yote ya umisionari imesonga mbele katika miaka iliyopita, tulitoka kwa wastani wa kufunza masomo mawili, matatu, manne pamoja na washiriki wakiwepo kila wki, hadi kumi hata kumi na mbili. Miezi michache iliyopita tulikuwa na wastani wa 14 hadi 16 na sasa lengo letu ni masomo 20 kufunzwa kila wiki pamoja na mshiriki akiwepo.

Ninapokaa na kutazama mabadiliko haya katika kata yetu na katika kigingi chetu, ni rahisi sana kuona mambo mawili muhimu ambayo yanaongoza juhudi za umisionari kupanuka na hivi ni washiriki wakijihusisha katika juhudi za umisionari na kisha kutoa mwaliko wa kuhudhuria kanisa au kukutana na wamisionari. Kwa hivyo mimi ninaisaidia familia yangu na kila familia nyingine katika kata kupata nafasi za kushiriki injili na watu wengine.

TRISH GAUVIN

Mimi ni Trish Gauvin, huyu ni Mark Gauvin.

MARK GAUVIN

Tulibatizwa mnamo Januari 26, 2013.

CHRIS EUBANKS

Ilikuwa ni hadithi kamilifu ya kazi ya mshiriki mmisionari. Tulikuwa na familia moja ambayo ilifanya urafiki na wao, walijulishwa kwa familia nyingine. Watoto wao walikutana na watoto wengine katika kata yetu na kuwa marafiki.

TRISH GAUVIN

Naamini kwamba Mungu aliwaweka washiriki wengi wa Kanisa katika maisha yetu kwa madhumuni fulani.

CHRIS EUBANKS

Na hiyo ilipelekea hata kwenye mazungumzo ya dhati zaidi na wamisionari na walianza kuhudhuria kanisa zaidi kila mara.

TRISH GAUVIN

Niliona jinsi injili inafanya kazi katika maisha yao na jinsi walivyo nuru.

CHRIS EUBANKS

Ni muhimu kwa washiriki wetu kupata kujua wamisionari wetu na wamisionari wetu kujuana na washiriki wetu. Lakini hata cha muhimu zaidi, ni muhimu kwa washiriki wetu kujuana na wachunguzi wetu na kuanzisha urafiki na wao.

MARK GAUVIN

Inakuwa rahisi unapojifunza na kukutana na watu kama hao kwa sababu unaweza kuhisi huru kuuliza. Unaweza kuhisi huru kugundua na kujifunza kitu fulani ambacho hujui. Hamna hukumu.

TRISH GAUVIN

Kwangu mimi nilihisi sana kama Joseph Smith nilipokwenda kutoka kanisa baada ya kanisa. Haikuoneka kamwe kama kuna chochote kikubwa kinachokosekana na kamwe sikukipata. Hii inalingana: inalingana na familia yangu, inalingana na maisha yangu.

CHRIS EUBANKS

Ukame huu au kipindi cha mdororo wa kazi ya umisionari katika eneo hili kwa kweli kilikuwa kimeisha na inaendelea kupata kasi siku baada ya siku. Na sioni ikififia wakati wowote karibuni.

Hii ni kazi kuu katika siku za mwisho. Hii ndiyo sababu sisi tuko hapa, kukusanya Israeli. Na kwangu mimi na kwa washiriki wote wa Kanisa, ni jukumu letu kushiriki injili na watu wengi tuwezavyo.