Kazi ya Kiroho
MZEE ANDERSEN
Akina Ndugu na dada wapendwa,mojawapo ya baraka kuu za maisha yangu ni kuwa pamoja nanyi katika vigingi vyenu karibu kila wiki. Katika kila taifa na tamaduni, sisi, kama Viongozi Wakuu wenye Mamlaka, tuna fursa ya kuhisi wema wenu, na imani yenu katika Bwana, Yesu Kristo. Tunajua upendo Wake kwenu, na tunafurahia upendeleo wenu wa kumfuata Yeye na kuweka amri Zake. Tunawashukuru ninyi kama mabaraza ya vigingi na kata kwa kutunza Ufalme wa Mungu na kuwa vyombo katika mikono Yake katika kuwahudumia wanawe na mabinti Zake.
Tunapohudumu katika mabaraza na urais, sisi sote tunajikumbusha wenyewe kwamba yetu ni kazi ya kiroho. Tunapoketi chini katika mikutano ya baraza, kazi yetu huanza tukiwa kwenye magoti tunapotafuta mwongozo wa Bwana. Na ingawa wakati mwengine sisi huangalia kalenda, ni pale tunapoondoka kutoka kwa mikutano hii, kwenda kwenye kazi ya Bwana, ndipo mara nyingi tunatekeleza madhumuni yake yaliyo muhimu sana. Tunafanya kazi pamoja kwa imani na umoja. Kwa imani kwamba Bwana ataongoza hatua zetu na umoja na kila mmoja na pamoja na wamisonari, tukihamasishwa kwa upendo kwake Yeye na kwa kila mmoja na mwengine na kwa wale tunawahudumia.
Kanuni hizi za kiroho daima zimekuwa sehemu ya kazi ya Bwana. Mimi nina hakika kwamba zi dhahiri kabisa katika baraza la kata yako mnapohudumu pamoja.
Acha nishiriki hadithi tatu za kweli pamoja nanyi kutokana na shughuli niliyokuwa nayo wiki chache zilizopita katika Tampa, Florida. Mnapotazama matukio haya ya halisi ya kimaisha, fikiria juu ya mambo mazuri yanayotendeka katika baraza la kata yako.
Hadithi yetu ya kwanza inaanza katika Brooksville, baraza la kata ya Florida.
ASKOFU CICCARELLO
Tulipotazama orodha zetu, tuliona majina ambayo hatukutambua. Ilikuwa ni Dada Kane … Katika mabaraza yetu ya kata tunatoa shughuli mahususi ya kutembelea familia tofauti, na washiriki---nimeona mabadiliko ambapo wameingia ndani mara na hasa kujitolea---“ Askofu, mimi nitaenda.”
MZEE ANDERSEN
Hii iko katika kitovu cha kazi yetu takatifu---kuhisi msukumo wa kiroho na kuwa tayari kuufuata. Katika Kata ya Brooksville, ilikuwa ni Dada James ambaye alisonga mbele.
DADA KANE
Nilipata matembezi kutoka kwa Dada James na wamisionari fulani ambao walipitia. Na yeye alinialika katika shughuli fulani na mambo ambayo yalinifanya mimi kuwa na rafiki katika Kanisa, hasa. Na, unajua, ilileta tofauti yote, kama, kunifanya kuhisi kukaribishwa tena.
MZEE ANDERSEN
Tulipokuwa tunaendesha baraza la kata yetu kwa maombi, ufunuo ulikuja---Dada James alikuwa radhi, shughuli ikatolewa,na miujiza ikafuata. Punde, mumewe Dada Kane, ambaye hakuwa mshiriki wa Kanisa, pia akaanza kuhisi mvuto wa Bwana.
DADA KANE
Jumapili moja, bila kutarajiwa, aliamka na kusema, mimi nadhania nitaenda Kanisani pamoja nanyi leo.
ASKOFU CICCARELLO
Ndugu Kane alihudhuria na punde baada ya mkutano wa sakramenti akaondoka. Nilimuona Dada Kane na kumuuliza yeye pale mmewe alikuwa, naye alisema, “Yuko nje katika uwanda wa kuegesha magari. Alikuwa tayari kwenda zake.” Na mimi nikauliza kama yeye hakuwa na pingamizi mimi nikijitambulisha kwake. Kwa hivyo nilifanya hivyo.
MZEE ANDERSEN
Baraza la kata, wamisionari, Dada James, askofu unaweza kuona umoja walionao? Askofu basi alipata maongozi kuwaalika Ndugu na Dada Kane kukutana na rais wa kigingi.
NDUGU KANE
Alisema, “Unajua mimi ningependa wewe uje na kujiunga na Kanisa. Unafikiria nini kuhusu hayo?” Na nilifikira, “eeh, hivyo si ni vyema, kuwa na mtu anayenithamini, na kunipenda mimi kikweli. Ni vyema kupendwa, unajua hivyo?
MZEE ANDERSEN
Kile Ndugu Kane alihisi akiwa na rais wa kigingi kilikuwa kitu kile kile yeye alikuwa anahisi siku zote. Yeye alihisi upendo wa Bwana kwake na upendo huo ulipotiririka kutoka kwa viongozi, washiriki, na wamisionari wakifanya kazi kwa umoja.
ASKOFU CICCARELLO
Kutoka hapo, tulianza kumwalika yeye kwenye mikutano ya sakramenti. Makaribisho ambayo alipokea kutoka kwa kata na kisha Roho ambayo alihisi kupitia upendo wetu, hasa ndipo yeye alianza kubadilika.
MZEE ANDERSEN
Nilipotembelea baraza la kata katika Brooksville, Askofu Aaron Ciccarello aliongea kile kilichokuwa katika moyo wa kila mtu.
ASKOFU CICCARELLO
Kumekuwa na mabadiliko makubwa katika jinsi tunavyowapenda watu hawa. Sisi sote tuko katika mambo haya pamoja na sisi tu kundi la viongozi wasio wakamilifu. Na tofauti kubwa ni kwamba sisi tunajua ni kazi Yake na Yeye hatakubali tushindwe kama tutafanya bidii tunavyoweza.
MZEE ANDERSEN
Hii ni muhimu sana: tunapofanya bidii tunavyoweza, Yeye hatakubali tushindwe. Sisi sote tunahisi mapungufu. Lakini kama vile Rais Monson anavyosema, “Tunapokuwa katika kazi ya Bwana, tuna haki ya usaidizi wa Bwana.” Sisi tunamngojea Bwana, tukijua kwamba miujiza itafuatia imani yetu.
Nefi alisema kwamba yeye kuwa “aliongozwa na Roho, wala hakujua kimbele vitu ambavyo [yeye] angefanya” (1 Nefi 4:6). Hii ndiyo njia ya uanafunzi. Hatujui daima kile kilicho mbele, lakini Bwana anajua, na kama tutamwamini Yeye, Yeye atatuongoza sisi kwa mkono Wake, na miujiza Yake itafuata. Mimi nalipenda tamko thabiti la Bwana wakati Yeye alisema: “Mimi ni Mungu wa miujiza; na kwamba mimi sitendi lolote miongoni mwa watoto wa watu ila tu kulingana na imani yao” (2 Nefi 27:23).
Kanuni hii kweli katika kila taifa, kila tamaduni, na katika kila lugha. Mwezi mmoja tu uliopita katika Hong Kong, nilitumia kamera ndogo ya video niliokuja nayo kutoka nyumbani ili kunasa mawazo mafupi na hisia za baadhi ya viongozi wa Kanisa wa sehemu hii.
MZEE ANDERSEN
Askofu Chek, umeshatambua familia tatu au nne ambazo wamisionari wanaweza kukusaidia wewe katika kujaribu kuwaleta tena katika kushiriki kikamilifu?
ASKOFU CHEK
Ndio, sisi hasa tuna hadithi ya mafanikio. Familia ya Wong imekuwa haishiriki kwa miaka 5–6. Wamisionari walitembelea familia hiyo. Washiriki walifunga na kuombea familia hiyo. Na walipokuwa tayari, tuliwarudisha.
DADA MOK
Usaidizi upo daima tunapokuwa na imani.
MZEE ANDERSEN
Tunapotenda kwa imani, kila mara tunapata kwamba baraka kutoka kwa Bwana ni tofauti kuliko matarajio yetu, lakini bora zaidi ya vile tulifikiria. Hadithi yetu ya pili inaonyesha kanuni hii. Inaanza na Rais Victor Patrick wa Kigingi cha Tampa Florida. Yeye na familia yake mwenyewe walitafuta mwongozo wa Bwana, na walipata maongozi kuwaalika marafiki zao na majirani kwa ubatizo wa binti yao uliokuwa unawadia.
RAIS PATRICK
Idadi ya watu ilikuja. Hamna yeyote wao alioonyesha hamu yoyote kwa Kanisa. Na hivyo, katika mkutano wa kigingi nilielezea, “Hapa kuna mpango wa Patrick, hivi ndivyo tulivyofanya, na ilikuwa vyema. Tulikuwa na watu wengi waliokuja kwenye ubatizo, lakini kufika hapo hakuna chochote kilichotendeka.” Dada Palmer alikuwa katika mkutano huo.
MELISSA PALMER
Mwaka uliopita nilimsikia Rais Patrick akitoa hotuba na kutaja tu kwa kupitia kwamba mke wake amefanya mwaliko katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya kila mmoja wa mabinti zake, pia akiwaalika katika ubatizo. Kwa hivyo, niliweka kijibarua kidogo cha mwandiko wa mkono na kuwaalika wote kwenye ubatizo. Lakini bahati mbaya …
YOTE
Hakuna aliyekuja. [Kicheko]
BRAD PALMER
Na hatukujua chochote wakati huo lakini mmojawapo wa majirani wetu alikuwa anatayarishwa.
MZEE ANDERSEN
Bwana alikuwa amewavuvia wote Rais Patrick na Dada Palmer, lakini kwa muijiza ambao wao hawakutarajia. Sisi daima hatuwezi kuona mwisho kutoka mwanzoni. Sisi tunamwamini Bwana na kumngojea Yeye, tukijua kwamba katika wakati Wake na kwa njia Yake, Yeye atafanya miujiza Yake. Wakati alipokuwa anawapatia mvuvio Rais Patrick na Dada Palmer, Yeye pia alikuwa anamtayarisha Dada Valerie Adams, mshiriki asiyeshiri kikikamilifu ambaye alikuwa hajaja Kanisani kwa zaidi ya muongo mmoja. Mwanawe Dada Adams, Braden na Rhet Palmer walikuwa tayari marafiki shuleni.
MZEE ANDERSEN
Tuambie kidogo zaidi jinsi haya yalitokea kwa familia yako.
DADA ADAMS
Kwanza, nilikuwa nimepata ndoto kuhusu Kanisa. Na haikuwa kitu chochote maalum. Karibu wiki mbili baadaye, mlango uligongwa na alikuwa ni huyu mvulana mdogo maridadi ambaye alikuwa mlangoni na alikuwa na mwaliko wa siku ya kuzaliwa naye akanipatia. Na ndani ya mwaliko huu kulikuwa na mwaliko mwengine. Na hasa nimekuja na huo mwaliko.
MZEE ANDERSEN
Oh, ningependa kuuona.
DADA ADAMS
Ndio, niliuhifadhi kwa sababu ni muhimu sana.
DADA ADAMS
Kwa hivyo nilipousoma nilitazama kote kama, “Oh, kumbe.’
MZEE ANDERSEN
Kwa sababu mtu alikuwa anakutunza wewe.
DADA ADAMS
Hasa, hii ni ishara. Kwa hivyo mimi nilienda kwenye karamu ya siku ya kuzaliwa.Nilipoingia na kusema tu “Ee, Mimi ni Valerie na nilibatizwa katika Kanisa.”
MZEE ANDERSEN
Mara moja Valerie na familia yake walizungukwa na upendo na urafiki wa kundi la ajabu la washiriki na wamisionari. Wamisionari wakawa walimu. Punde, Valerie akarudi Kanisani. Derek, mumewe , akabatizwa, na yeye akambatiza Braden.
Je! Unaweza kuona jinsi Bwana hutimiza kazi Yake? Baba yetu wa Mbinguni anajua watoto Wake. Yeye anasikia maombi yao. Yeye anajua nani anayemtafuta Yeye, na Yeye atatuongoza kwao. Kama Amoni anavyosema katika Kitabu cha Mormoni: “Wao wako katika mikono ya Bwana wa mavuno, na wao ni wake.” (Alma 26:7).
Kuna kanuni muhimu ya imani ambayo imeongoza maisha ya nabii wetu, Rais Thomas S. Monson. Yeye husema, “Kutamani hakutatufanya kuwa. Bwana anatarajia … matendo yetu.” Hadithi yetu ya tatu inasisitiza mafundisho haya vyema. Inaanza na Askofu Rodney Kelly ambaye alihisi haja ya kusaidia kata yake kuchukua hatua.
ASKOFU KELLY
Tulikuwa tumekuwa na wakati mgumu, kupata ubatizo katika kata yetu. Ulikuwa ni wa chini sana, na, tukatambua kwamba Bwana hatatubariki sisi na waongofu wapya mpaka tutakapowatunza wale watu tulionao tayari katika kata yetu.
MZEE ANDERSEN
Askofu na baraza la kata walikuwa wanatambua kwamba kuzungumza na watu hakukutosha. Walihitaji kutenda.
ASKOFU KELLY
Kwa hivyo sisi kama vile uaskofu tulipoanza mwanzo, na tulienda na, tukachukua majina kadhaa ambayo kamwe hatukuyajua, na tukawatafuta. Tulialika Kamati Tendaji ya Ukuhani ili kuunagana nasi na kisha baadaye, tukapanua hivyo hata kwa jamii yote ya ukuhani na hata kwa kundi la makuhani wakuu. Na tuliwauliza wao kutenga usiku wa Jumanne au Alhamisi moja katika mwezi.
MZEE ANDERSEN
Viongozi wa kata na wamisionari walipoanza kuwashughulikia na kubariki wengine, mabadiliko makubwa yalitokea katika kata. Roho wa Bwana alienea. Wamisionari wa muda waliona tofuati iliyotokea.
MZEE LYONS
Tulikuwa na kiongozi wa misheni wa kata ambaye alikuwa anatupigia simu kila siku, si hivyo tu, askofu alikuwa anatupigia siku bila kukoma na kisha washiriki---washiriki wote ambao tulikuwa tunafanya kazi nao pia walikuwa wanatupigia simu karibu kila siku au kututumia ujumbe mfupi au wakajaribu kujihusisha katika kila njia ambayo wengeweza.
MZEE ANDERSEN
Viongozi na wamisionari kutoka Kata ya Tampa 4 walishiriki uzoefu wao pamoja nami wakati nilitembelea mkutano wao wa baraza la kata.
NDUGU BARNHILL
Najua kwamba nilipokuja kwanza, na nikaanza kuzungumza kuhusu kufanya matembezi ya kila wiki, mimi niko hivyo, “Huo ni wakati mwingi.” Lakini nilipata kwamba nilipokuwa nikienda na kutembelea watu na kufuata maelekezo ya askofu na mwongozo ambao yeye alikuwa anatoa, ilishangaza sana.
RAIS WA MUUNGANO WA USAIDIZI WA KINA MAMA
Nimeona mabadiliko katika kina dada kwa haya, ambapo walikuwa tayari kwenda hatua ingine zaidi na kufanya kazi wanayohitaji kufanya na kumfanya kila mtu kuhisi kupendwa na kukaribishwa.
ASKOFU KELLY
Matukio haya ya kiroho yalipotokea, ilikuwa ni mahali nilipostahili kuwa. Watu katika kata ambao walikuwa wanahudhuria kikamilifu walikuwa wanataka kuwa na matukio haya ya kiroho.
DADA BOWE
Usiku wangu wa kwanza kwenda nje, walikuwa wanafanya migao ya kata. Na ilikuwa kitu cha mvuvio kwangu, kujua kwamba mimi niko nje kufunza watu na kuwaleta tena katika zizi na kusaidia kata.
MZEE ANDERSEN
Katika ziara hiyo hiyo hadi Asia wiki nne zilizopita, nilitembelea India. Viongozi huko walielewa kweli hizo hizo za kiroho. Walishiriki umaizi wao kwenye ile kamera ndogo nilikuja nayo.
RAIS BENGANPA
Sisi huenda nyumbani mwao. Ndio, sisi tunaenda nyumbani kwao. Na sisi tunajaribu kushiriki ushuhuda wetu na kuwapenda wao na kujaribu kuwarudisha kanisani tena.
DADA MASSEY
Tunaposikia ushuhuda wetu, kwa kweli tunaalika Roho katika chumba hicho, na mchunguzi au washiriki wasioshiriki kikamilifu, wanaweza kuhisi Roho. Na wanaamua kurudi tena kwa sababu wanajua hiki ni kitu muhimu ambacho wanakosa hasa katika maisha yao.
MZEE ANDERSEN
Ili kutusaidia sote, kuna sehemu mpya kwenye LDS.org inayoitwa “Hastening the Work of Salvation.” Hapo utapata hadithi zaidi na mifano na nyenzo za kukufaidi kutoka kwa viongozi, washiriki, na wamisionari kote duniani ambao, kama wewe, wanafanya kazi pamoja kwa imani na upendo kuharakisha kazi ya Bwana.
Tunapofanya vyema tunavyoweza, Bwana atakuwa pamoja nasi. Maandiko yanasema, “[Kama] watumishi walienda na kufanya kazi kwa [nguvu] zao; Bwana … pia alifanya kazi pamoja nao.” (Yakobo 5:72).
Nilipokuwa nimekaa katika jukwaa katika Mkutano Mkuu wa Kigingi cha Tampa Florida wiki chache zilizopita, nilishangaa kuona ndugu 32 wakikubaliwa kupokea Ukuhani wa Melkizedeki. Walikuja kutoka kata na matawi yaliyo sawa kabisa na yale ya sehemu mnayoishi na kuhudumu.
Kila mwanaume aliposimama, nilifikiria juu ya muijiza ambao ulikuwa umetokea katika maisha yake na katika maisha ya wanawake na watoto waliokaribu naye. Nilifikiria juu ya viongozi, washiriki, na wamisionari ambao walifanya kazi kwa umoja, na upendo na huduma yao ya kama Kristo. Nilifikira mwongozo mtakatifu wa Bwana walipotenda kwa imani. Nilifikiria maneno ya Moroni: “Je, miujiza imekoma? ... Au malaika wamekoma kuonekana kwa watoto wa watu? Au amesimamisha uwezo wa Roho Mtakatifu kutoka kwao? (Moroni 7:27, 36).
“Tazama ninawaambia, La; kwani ni kwa imani kwamba miujiza hufanyika.” (Moroni 7:37).
Mimi nashiriki nanyi ushuhuda wangu halisi kwamba Yesu ndiye Kristo, kwamba Yeye ni Mwokozi wetu na Mkombozi wetu. Hii ni kazi Yake takatifu. Mimi nawaahidi kwamba Yeye atawaongoza na kuwa pamoja nanyi mnapojinyenyekeza kutafuta usaidizi Wake kwa imani. Katika jina la Yesu Kristo, amina.