Maktaba
Karibuni


Karibuni

Kina ndugu na dada, kwenye mabawa ya huo wimbo wa kifahari wa misionari, tunawakaribisha kwa haya matangazo ya uongozi duniani kote. Rais Thomas S. Monson, ambaye alikuwa nasi asubuhi ya leo na atashiriki baadaye katika matangazo haya, ameomba kwamba mimi, Mzee Holland, niendeshe mkutano huu.

Kwa wamisionari wote wa muda wanaoshiriki katika matangazo haya ulimwenguni, mimi nawambieni kwamba hamtawai tena katika maisha yenu yote kuwa sehemu ya mkutano wa eneo mkubwa kama huu! Hufurahieni na mjifunze kutoka kwake.

Kwa washiriki wengi wa Kanisa mliokusanyika katika maeneo yasiyohesabika, tunathibitisha kwamba mabaraza ya kata na vigingi hayawezi kusema tena kuhusu jeshi jipya kuu la wamissionari, “Waone wakienda.” Hapana, muda umetujia ambapo lazima sasa tuseme, “Waone wakija.” Sisi sote ni lazima tupangie na tutumie rasilmali hii iliyotumwa kutoka mbinguni kwa njia bora kabisa.

Kwa kuzingatia umoja huo wa mshiriki na mmisionari, tunashukuru kwaya yetu, inayojumuisha wamisionari kutoka Kituo cha Mafunzo cha Umisionari cha Provo na washiriki wa mabaraza ya kata na vigingi kutoka Kaunti ya Utah. Walifungua mkutano huu na ufasiri wa kupendeza wa “Hark All Ye Nations!” Wanaongozwa na Ndugu James Kasen na Ryan Eggett na Ndugu Seth Bott na Dada Ellen Amatangelo kwenye kinanda.

Maombi yetu ya kufungua yatatolewa na Mzee Christopher Ludlow, ambaye ameitwa kuhudumu katika Misheni ya Mexico Torreón

***

Asante, Mzee Ludlow.

Wakiwa wameketi nasi kwenye jukwa ni washiriki wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, Jamii ya Wale Sabini, Uaskofu Simamizi, na urais mkuu wa makundi saidizi. Wenzi wao wameketi katika uwanda wa mchezo hapa katika Kituo cha Marriot. Kwa njia fulani, hawa na sisi sote tuwakilisha wa mabaraza ya kata na vigingi vyenu na kazi ambayo tunayofanya sote pamoja. Hapa katika makao makuu ya Kanisa, sisi hushauriana kwa kina juu ya maamuzi yote makuu kuhusu kazi ya umisionari na kazi zote. Kwa mfano, tulipoangalia kushukishwa kwa umri wa huduma ya umisionari, tulishauriana na mabaraza yote simamizi na jamii za Kanisa, ikijumuisha urais wa Muungano wa Usaidizi wa Kina Mama, Wasichana, na Msingi. Ushauri wao na mawaidha yalikuwa muhimu katika uamuzi huo. Hivyo ndivyo tunatumahi ndivyo ilivyo katika mabaraza yenu ya kata na vigingi: kusikiliza kila mtu, akina ndugu na dada, katika kila swala la umuhimu, ikiwa ni pamoja na swala lililo nyeti kabisa juu ya kazi ya mshiriki mmisionari.

Hivyo basi katika roho ya haya yote, tunashukuru kukutana nanyi katika mkutano uliyo kama mkutano wa baraza la kigingi na kata la ulimwengu kote. Tunatumainia kuwapa maelekezo na mwongozo wetu bora kuhusu kazi ya wokovu katika kata na vigingi vyenu. Tuna shukrani hasa kwa kuwa nasi wale ambao kwenye mabega yao kiasi kikubwa cha kazi ya wokovu iko juu yao. Urais wa Eneo, Sabini wa Eneo, marais wa vigingi, maaskofu, washiriki wa baraza kuu waliopangiwa kazi ya umisionari, viongozi wa misheni wa kata, washiriki wa mabaraza ya vigingi na kata, na, bila shaka, wamisionari na marais wa misheni waliokusanyika duniani kote. Timu ya ajabu kweli, na tuna furaha kweli kushiriki nanyi katika matangazo kama haya ya kihistoria.

Tunawakaribisha wale ambao wameungana nasi kupitia setilaiti ama mtandao. Kwa mfano, tuko pamoja na Rais James Matsumori na wamisionari wake katika Misheni ya Washigton D.C. North. Rais Matsumori, hujambo?

RAIS MATSUMORI

Tunaendelea vyema, Mzee Holland

MZEE HOLLAND

Mnaonekana mnaendelea vyema, hasa Dada Matsumori.

DADA MATSUMORI

Asante

MZEE HOLLAND

Asante kwa kukutana nasi leo pamoja na baraza lako la uongozi wa misheni, ambao tunawaona katika scrini. Tunashukuru kwa ninyi kuwa pamoja nasi. Rais na Dada Matsumori, wapatie wamisionari wenu upendo wetu. Na Dada Matsumori, watoto wote wa Msingi wa Kanisa wanakuenzi. Wametuma upendo wao.

Leo, Rais Matsumori anawakilisha marais wa misheni 405 wote kote duniani. Tuna shukrani kwa marais hao wote wa misheni na wake zao ambao hivi sasa wanahudumu, kwa wale wanaokamilisha misheni zao katika siku chache zijazo (huu ni wakati ororo kwao), na wale waliokusanyika hapa usiku wa leo katika mwanzo wa huduma yao katika semina ya marais wetu wa misheni.

Tunaye pamoja nasi Rais Marco De Loayza Guillen wa Kigingi cha Lima Peru Magdalena. Habari ya jioni, rais. Tunashukuru kuwepo kwako hivi leo.

RAIS DE LOAYZA

Ni fursa kuu kwetu kuwa nawe, Mzee Holland. Asante sana.

MZEE HOLLAND

Ni siku ya ajabu jinsi gani ambayo tunatangaza kutoka Peru hadi Provo. Kuna kitu cha kimashairi kuihusu.

Asante, Rais, kwa kuchukua nafasi ya kukutana nasi hivi leo. Tunatuma upendo wetu kwa Dada De Loayza na washiriki wote wa kigingi chako.

Anawakilisha, kama rais wa kigingi, marais wa vigingi wengi wema waliokusanyika duniani kote pamoja na mabaraza yao ya vigingi. Tunashukuru sana huduma ya uaminifu ya ndugu na kina dada hawa.

Pia akiwa pamoja nasi leo ni Askofu Ofeina K. Unga wa Kata ya Hauula Fourth, ya Kigingi cha Laie Hawaii, na baraza lake la kata. Habari, Askofu! Hali ya anga iko vipi Hawaii?

ASKOFU UNGA

Ni nzuri. Tuna mvua, tuna jua, na tuna upepo.

MZEE HOLLAND

Karibuni Hawaii---ni maridadi na tuna mvua. Tunakupenda, Askofu. Asanteni, wewe na maaskofu wengine waaminifu na mabaraza ya kata yanayoshiriki pamoja nasi hivi leo. Tunashukuru una baraza lako la kata hapa.

Bwana anavyofunua mapenzi Yake kwetu sisi, kutakuwa na maboresho ya kuendelea ya jinsi tunavyotekeleza kazi ya umisionari. Tumekutana jioni hii ya leo ili kushiriki baadhi ya maboresho hayo nanyi. Maelezo zaidi na ushauri utawajia kupitia washiriki wa Jamii za Wale Sabini, ambao wana majukumu yaliyobainishwa wazi ya kazi ya umisionari.

Kristo alipojenga Kanisa Lake kwa mara ya kwanza, “aliweka na wengine, sabini, na kuwatuma wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe” (Luka 10:1). Katika wakati wetu, Bwana aliwaamuru Wale Kumi na Wawili “kuwaita hawa Sabini ... badala ya mwingine yeyote” na kuhimiza kwamba “Sabini pia wameitwa kuhubiri injili, na kuwa mashahidi maalum kwa Wayunani na ulimwenguni kote” (M&M 107:38, 25). Kazi ya umisionari daima imekuwa msingi kwa wito wa Wale Sabini. Kwa njia moja ama ingine, kila mtu hapa huripoti kwa Urais wa Kwanza na Jamii ya wale Kumi na Wawili kupitia Wale Sabini.

Watazamie kwa ajili ya maelekezo na mwongozo. Watazamie kwa ajili ya mfano wa jinsi kazi ya wokovu inastahili kutekelezwa.

Kwa kila mmoja wenu, Sabini mmoja muhimu kabisa ni yule Sabini wa Eneo ambaye anasimamia baraza la uratibu mahali unapoishi. Maelekeo na mwongozo kuhusu kazi ya wokovu utakujia kupitia Sabini wa Eneo wako katika baraza hilo, ambapo marais wa vigingi na misheni hushuriana kuhusu kazi ya mshiriki mmisionari. Hatimaye, wakati mabaraza ya uratibu yalipotekelezwa kwa mara ya kwanza, yalikuwa yanaitwa, “Member-Missionary Coordinating Councils.” Hiki ni kipengele muhimu cha historia cha kukumbukwa. Tafadhali hakikisheni kwamba kila baraza linashikilia sisitizo kwenye sehemu hii muhimu ya kazi ya wokovu.

Ninaomba kwamba sote tuweze kuguswa na kufundishwa na jumbe ambazo zitashirikishwa leo. Ninatoa ushahidi kwamba hii ni kazi ya Baba yetu wa Mbinguni, na kwamba anaijali kabisa kibinafsi. Ninashuhudia kwamba mnapotekeleza maelekezo yatakayotolewa hapa hivi leo, mtakuja kujua pia jinsi Yeye anahusika kindani katika jukumu hili. Mtamhisi Yeye akiwaongoza na akiwainua na kuwaelekeza kufanya kile ambacho, sisi wenyewe, kinashinda uwezo wetu kabisa, lakini kwamba pamoja Naye daima kinawezekana. Kwa haya ninashuhudia katika jina la Mwanawe Mpendwa, hata Yesu Kristo, amina.

Sasa, ndugu na dada, itakuwa furaha yetu kuu kusililiza kutoka kwa Mzee L. Tom Perry wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, akifuatiwa na wimbo, “I’ll Go Where You Want Me to Go.”

Mzee Perry.

***

Shukrani zetu zimwendee Mzee Perry na kwa sehemu hii ya video kwa kutukumbusha sisi hasa kuhusu jukumu letu kama washiriki, tofauti kabisa na wamisionari, kualika wengine kumjia Kristo na kupokea injili.

Hili ni jukumu ambalo sisi saa zingine huliepuka kwa sababu tunaogopa kwamba mwaliko wa kukutana na wamisionari ama kuhudhuria kanisa linaweza kuhudhi jirani ama rafiki, ama hata mwanafamilia wa familia yetu wenyewe, kama ilivyoonyeshwa katika video hii. Hata hivyo, mwaliko uliotolewa kwa upendo wetu kwa ajili ya wengine na Bwana Yesu Kristo na hamu yetu kwa ajili ya furaha hii kwa marafiki hawa na wanafamilia hautaonekana kamwe kama kuwa wa kuhudhi ama kuhukumu.

Agizo la mwisho la Bwana aliyefufuka kwa wafuasi Wake lilikuwa kufundisha na kubatiza. Ubatizo ndiyo agano la kwanza la muhimu kwenye safari ya wokovu. Maandiko yanatueleza juu ya furaha ya Bwana tunapobatiza watu waliotubu na kustahili. Tunapaswa tuwe na hamu ya kufanya hivyo na kumletea furaha hiyo. Jambo nzuri kuhusu haya ni furaha inayokuja kwetu sisi pia.

Itakuwa fursa yetu sasa kujifunza kutoka kwa Mzee Neil L. Andersen wa Jamii ya Kumi na Wawili. Baada ya Mzee Andersen kutufundisha, tutafurahia wimbo mseto wa nyimbo za umisionari.

Mzee Andersen.

***

Asante, Mzee Andersen, na asanteni kwa kizazi chipukizi, 70,000 ambao tayari wako katika wito katika uwanda wa misheni.

Hatua ya kwanza katika kujenga Kanisa ni kuleta mtu ndani yake kupitia maji ya ubatizo. Jumbe tulizokuwa na fursa ya kuzisikiliza hivi leo zimetufundisha jinsi ya kusaidia kujenga Kanisa, ama kulijenga tena, katika nyumba za marafiki zetu na majirani na familia ambazo bado hazijapata nafasi kulikubali ama wameondoka kutoka kanisani kwa muda.

Itakuwa fursa yetu kuu sasa kusikiliza kutoka kwa Mzee Russell M. Nelson, ambaye, pamoja na majukumu yake mengine katika Jamii ya Kumi na Wawili, anahudumu kama Mwenyekiti wa Baraza Tendaji la Umisionari. Ninafurahia kuhudumu kama mwenzi mdogo wa Mzee Nelson kwenye baraza hilo.

Kufuatia Mzee Nelson tutazungumuziwa kupitia video na mmoja wa walimu wakuu wa siku zetu, Rais Boyd K. Packer, Rais wa Jamii ya Mitume Kumi na Wawili, atakayetufunza jinsi ya kufundisha.

Mzee Nelson, kisha video ya Rais Packer.

***

Asante, Mzee Nelson kwa mafunzo yako na Rais Packer, kwa mafunzo yako kuhusu mafunzo.

Kama tulivyofundishwa leo, ndugu na dada, Bwana anatuita kama washiriki binafsi wa Kanisa, na kama washiriki wa mabaraza katika Kanisa, kufanya mengi zaidi ili kutekeleza malengo Yake na kupeleka kazi Yake mbele.

Itakuwa ni fursa yetu na baraka sasa kusikiliza kutoka kwa nabii wetu, Rais Thomas S. Monson, anayeamini vivyo hivyo. Ataongezea ushahidi wake na kutufundisha umuhimu wa imani katika kazi yetu ya kazi ya mshiriki mmisionari. Ni furaha kweli kuwa na Rais Monson kuwa nasi. Licha ya kupoteza mkewe mpendwa hivi majuzi, Frances, Rais Monson alinuia kuongeza sauti yake na ushuhuda wake kwa kile kinachotendeka hapa jioni hii. Tuna shukrani kiasi gani kwa ajili ya nabii wa kutuongoza katika wakati wetu. Ninawahimiza msikilize kwa makini ushauri wa Rais Monson, mhisi ushawishi wa ujumbe wake, na mkubali ushahidi anaotoa wa kazi hii.

Kufuatia hotuba ya Rais Monson kwetu, kwanya itaimba wimbo wa umisionari unaoenziwa sana, “ Called to Serve,” baadaye maombi ya kufunga yatatolewa na Dada Ruth Astorga anayehudumu kama Rais wa Muungano wa Uasidizi wa Kina Mama katika Kata ya Bonneville 7 ya Kigingi cha Provo Utah Bonneville.

Rais Monson.