Kufundisha katika Kanisa
Nilipopokea jukumu la kuzungumzia Kanisa juu ya kufundisha, nilihisi kupungukiwa kabisa na kuomba kwa dhati juu ya jukumu hili. Takriban miaka 70 iliyopita, niliketi juu ya mwamba katika kisiwa kidogo kinachoonyeshwa kwenye stempu za kutuma barua kule mbali katika Pasifiki, mbali ya kisiwa cha Okinawa. Vita vilikuwa punde vimeisha na nilikuwa hai. Niliwaza kile ningefanya. Tulikuwa tunaongojea meli zije na zitupeleke nyumbani. Niliwaza kile ningefanya na maisha yangu. Je, nilitaka kufanya nini? Je, nilitaka kuwa nini? Hatimaye niliamua kwamba nilitaka kuwa mwalimu. Na hivyo basi, niko hapa, takriban miaka 70 baadaye, nikiwa na hamu ile ile, uamuzi ule ule, nikiwa nimejifunza mengi, lakini nina mengi bado kujifunza.
Kila kitu kingine, hatimaye kikichambuliwa, matokeo huwa ni kufundisha. Na sisi hujifunza ili kufundisha. Kunazo kanuni ambazo tunaweza kujifunza kuchambua na miongoni mwao, pengine ile ngumu kujifunza, ni kuishi ili kwamba tuweze kujiachilia wenyewe na tusisome kutoka kwa mswada, lakini tu kutegemea Roho
Laiti kungekuwa na njia ya kukuahidi kwamba ukisoma kwa bidii na kwa makini kwamba ungekuwa bora zaidi. Haitakuumiza. Lakini haitakufanya uwe bora, hata vyema zaidi kama vile ingekufanya kama ungeamini katika Bwana na kuamini katika Roho na kwenda mbele. Hiyo haitakuwa asili ya pili lakini wewe, kwa muda ufaao, unajifunza kuamini Roho, kwamba atakuwa hapo. Mara nyingi nimesimama ukumbini na kuwaza kile nitasema, nikiwa ni kama sina chochote akilini na nikijua kuwa kulikuwa na jukumu kuu, lakini daima huwa inakuja. Huja unapoanza. Unaanza na kisha ufunuo huanza kutiririka. Pongezi tunazofaa kutoka kwa hayo yote ni kidogo sana kwa ajili yetu wenyewe, kwa vile Roho ndiye chanzo cha uwezo huo.
Nimekuja kujua kwamba kila mtu ni mwalimu. Kanisani sisi huzungumzia kuhusu kuitwa kwa nyadhifa, kuwekwa wakfu ili kufundisha Shule ya Jumapili ama katika vitengo vingine vya ukuhani. Ukuhani wakati mwingine hujivunia kuwa na uwezo wa kutekeleza mafundisho. Hawakaribii uwezo uliopewa mama. Mafundisho makuu Kanisani hufanywa na akina mama.
Hivyo basi kwa wale wanaofundisha Kanisani, iwe unafanya hivyo kiustadi ama vinginevyo, unajua kwamba ni fundisho takatifu na kwamba kiasi chake kikubwa zaidi hutendeka nje ya darasa, hata nje ya matayarisho ambapo unasoma masomo, kujifunza, na kisha kutafakari kwa sababu ya maelezo katika maandiko---“neno la Bwana lilinijia akilini” Kwamba “neno” daima halishindiwi ukiendelea mbele na kuwa mtiifu. Utiifu kwa vijana ni kama neno la kuhuzunisha. Sisi huwa si watiifu mara moja. Wazazi, hasa akina mama, hufundisha watoto wao wadogo kuwa watiifu. Tunawajibika wenyewe tunapokuwa watu wazima na wakati mwingine sisi huwa na vita vya kindani na nafsi zetu. Kuna neno, tubu. Kwa kiinegreza “re” umaanisha nini? Inamaanisha kufanya tena---rudia, rudia. Kisha unafaa kurudi nyuma hadi ulipopotea njia na kuendelea mbele ukiwa huru kutokana na changamoto zilizokukumba hapo awali. Upatanisho ndio mponyaji mkuu, ---unalipia dhambi. Je, unafahamu uzuri wa ajabu wa jinsi kwamba unaweza kutumia Upatanisho? Bwana alitekeleza Upatanisho kwa ajili yetu. Na hakuna chochote ambacho hauwezi kutubu na ambacho hauwezi kuokolewa kutoka ikiwa utatubu na kuamua kufanya maamuzi. Kwa hivyo, ushauri wangu ni rahisi: amua tu kufanya vizuri, amua kuwa bora zaidi, amua kuamini katika maandiko na unapofanya hivyo, utakua na changamoto ulizonazo zitakuwa kwa faida yako.
Miaka hii 70 iliyopita imenifunza mengi. Bado nina mengi ya kujifunza. Sijui nitajifunza kwa muda gani lakini itakapokamilika nitaenda katika ufalme mpya na kuanza shule mpya. Basi ninatoa ushuhuda wangu kwenu kwamba Bwana anaishi, kwampa Urejesho ni wa kweli, kwamba uliongozwa na kuamuliwa kabla ya dunia kwa ajili yetu. Bwana yu hai. Ninajua Bwana anaishi na ninamjua Bwana. Katika jina la Yesu Kristo, amina.