“Ni Kipi Tunachojifunza na Kamwe Hatutakisahau,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Ukuhani
Ni Kipi Tunachojifunza na Kamwe Hatutakisahau
Dondoo
Mara ya mwisho kuwa na kikao cha ukuhani cha mkutano mkuu ilikuwa Aprili 2019. Mengi yametokea katika miaka hii miwili iliyopita! …
… Naomba nipendekeze masomo manne natumaini sote tumejifunza na kamwe hatuyatasahau.
Somo la 1: Nyumbani ni Kituo cha Imani na Kuabudu …
… Vizuizi vya sasa juu ya kukusanyika hatimaye vitafika mwisho. Hata hivyo, dhamira yako ya kutaka kuifanya nyumba yako kuwa mahali patakatifu pa kwanza pa imani haipaswi kamwe kwisha. …
Somo 2: Tunahitajiana Sisi kwa Sisi
… Tunaweza kukamilisha mengi zaidi kwa pamoja kuliko awezavyo kila mmoja pekee yake. Mpango wa furaha wa Mungu ungevurugika kama watoto Wake wangebaki wametengana. …
Kama unamjua yeyote aliye mpweke, mwendee—hata kama nawe unajihisi mpweke pia! …
Somo 3: Akidi Yenu ya Ukuhani Imenuiwa kuwa zaidi ya Kukutana tu
… Mikutano ni sehemu ndogo tu ya kile akidi inachonuiwa na kile inachoweza kufanya.
… Akidi zipo katika nafasi za kipekee kuongeza kasi ya kusanyiko la Israeli kwenye pande zote mbili za pazia.
Somo 4: Tunamsikia Yesu Kristo Vyema zaidi Wakati tupo Kimya
… Vurugu ulimwenguni itazidi kuongezeka. Kinyume chake, sauti ya Bwana ni … “sauti tulivu ya upole kamili, [kama] mnong’ono, na [inapenya] hata kwenye roho” [Helamani 5:30]. Ili kuweza kuisikia sauti hii tulivu, wewe pia lazima uwe umetulia! …
Ndugu zangu wapendwa, kuna mambo mengi Bwana anatutaka sisi kujifunza kutokana na matukio ya wakati huu wa janga la ulimwenguni kote. Nimeorodhesha manne tu. Ninawaalika kutengeneza orodha yenu wenyewe, kuitafakari kwa uangalifu, na kuishiriki na wale unao wapenda.