“Maaskofu—Wachungaji juu ya Kundi la Bwana,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Ukuhani
Maaskofu—Wachungaji juu ya Kundi la Bwana
Dondoo
Askofu ana jukumu kubwa katika kuhudumu kama mchungaji kwa kukiongoza kizazi kinachoinukia, ikiwa ni pamoja na vijana wakubwa waseja, kwenda kwa Yesu Kristo. …
Unaweza kuuliza, “Kwa nini uaskofu umeelekezwa kutumia muda mwingi na vijana?” Bwana amepangilia Kanisa Lake kutimiza vipaumbele muhimu. Kwa hivyo, mpangilio wa Kanisa Lake una muundo ambamo ndani yake askofu ana jukumu la pande mbili. Ana jukumu la kimafundisho kwa kata kwa ujumla, lakini pia ana jukumu maalum la kimafundisho kwa akidi ya makuhani. …
Wengi wenu ninyi vijana wa thamani huenda msiwe na maono ya wazi ya wewe ni nani na unaweza kuwa nani. Walakini uko katika kilele cha kufanya maamuzi muhimu zaidi ambayo utafanya katika maisha yako. Tafadhali shauriana na wazazi wako na askofu wako juu ya chaguzi muhimu ambazo ziko mbele yako. Mruhusu askofu awe rafiki na mshauri wako.
Tunafahamu kuwa una majaribu na vishawishi vinavyokujia kutoka kila upande. Sisi sote tunahitaji kutubu kila siku kama Rais Nelson alivyofundisha. Tafadhali zungumza na askofu wako juu ya jambo lolote ambalo mwamuzi wa wote anaweza kukusaidia ili kufanya maisha yako yawe sawa na Bwana atakavyo katika kujiandaa kwa “kazi kubwa” aliyokupa katika kipindi hiki cha mwisho. Kama vile ambavyo Rais Nelson amekualika, tafadhali jistahilishe ili kuwa sehemu ya kikosi cha jeshi la vijana wa Bwana!