“Tumaini katika Kristo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Jumamosi Alasiri
Tumaini katika Kristo
Dondoo
Akina kaka na akina dada, katika wakati huu wa Pasaka tunaangazia katika Ufufuko mtukufu wa Bwana na Mwokozi wetu Yesu Kristo. Tunakumbuka mwaliko wake wa upendo wa “Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
“Jitieni nira yangu, mjifunze kwangu; kwa kuwa mimi ni mpole na mnyenyekevu wa moyo; nanyi mtapata raha nafsini mwenu.
“Kwa maana nira yangu ni laini, na mzigo wangu ni mwepesi” (Mathayo 11:28–30).
Mwaliko wa Mwokozi wa kumfuata Yeye ni mwaliko kwa wote ambao si tu mwaliko wa kumfuata Yeye bali pia wa kuwa wa Kanisa Lake. …
Yesu anatutaka tufahamu kuwa Mungu ndiye Baba wa Mbinguni mwenye upendo.
Kufahamu kuwa tunapendwa na Baba yetu wa Mbinguni kutatusaidia kufahamu sisi ni nani na kufahamu kuwa sisi ni wa familia Yake kubwa ya milele. …
… Licha ya changamoto tunazokabiliwa nazo maishani, tunaweza, kama asubuhi ile ya Pasaka ya kwanza, kuamka katika maisha mapya katika Kristo tukiwa na uwezekano bora na mpya na uhalisi mpya pale tunapomgeukia Bwana kwa ajili ya tumaini na kuwa sehemu ya. …
Sizungumzii juu ya matumaini katika Kristo kama mawazo ya kutamanika. Badala yake, nazungumza juu ya matumaini kama matarajio ambayo yatatimizwa. Tumaini kama hilo ni muhimu katika kushinda dhiki, kukuza uthabiti wa kiroho na nguvu, na kupata kujua kwamba tunapendwa na Baba yetu wa Milele na kwamba sisi ni watoto Wake ambao tunastahili kuwa wa familia Yake.
Kamwe usisahau kwamba wewe ni mtoto wa Mungu, Baba yetu wa Milele, sasa na hata milele. Anakupenda, na Kanisa linakutaka na kukuhitaji. Ndiyo tunakuhitaji wewe! Tunahitaji sauti zako, talanta, ustadi, wema, na uadilifu wako.