“Mioyo Imeunganishwa Pamoja,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao
Mioyo Imeunganishwa Pamoja
Dondoo
Alipoulizwa, “Mwalimu, ni amri ipi iliyo kuu?” Mwokozi alijibu “kumpenda Bwana, Mungu wako, kwa moyo wako wote,” ikifuatiwa na, “Mpende jirani yako kama nafsi yako” [Mathayo 22: 36–39] Jibu la Mwokozi linaimarisha wajibu wetu wa kimbingu. Nabii wa kale aliamuru “kwamba pasiwe na ubishi kati yetu, lakini kwamba [tutazame] kwa jicho moja … mioyo [yetu] ikiwa imeunganishwa pamoja kwa umoja na kwa kupendana sisi kwa sisi” [Mosia 18:21, msisitizo umeongezwa]. …
Sasa, kwa vijana wa kiume na wa kike, mnapoendelea kukua, kuwadhihaki wengine kunaweza kuwa ni hatari sana. Wasiwasi, msongo wa mawazo, na mbaya zaidi mara nyingi ni matokeo ya uonevu. …
Kwa wazi, adui anatumia hii kukiumiza kizazi chenu. Kusiwe na swala hili katika mtandao wako, vitongoji, shule, akidi au madarasa. Tafadhali fanya yote uwezayo kufanya maeneo haya kuwa ya ukarimu na salama zaidi. …
… Unapojitanua kwa ukarimu, kujali, na huruma, hata kidijitali, ninaahidi kwamba utainyosha mikono iliyolegea na utaiponya mioyo. …
Hebu kila mmoja wetu, bila kujali umri wetu, tujitahidi kuwa bora.
Unapojitahidi kukua katika upendo, heshima na ukarimu, bila shaka utaumizwa au kuathiriwa vibaya na uchaguzi mbaya wa wengine. Tunafanya nini basi? Tunafuata ushauri wa Bwana “wapendeni adui zenu … na waombeeni wale wanaowachukia ninyi.” [Luka 6:27 –28].
Wakati dhiki na mateso vinapoletwa kwetu kwa matendo ya kukosoa, hasi au ya roho mbaya, tunaweza kuchagua kumtumaini Kristo. Tumaini hili linatokana na mwaliko Wake na ahadi ya “changamkeni, kwa kuwa nitawaongoza” [Mafundisho na Maagano 78:18] na kwamba Yeye ataweka wakfu mateso yenu kwa faida yenu [ona 2 Nefi 2:2]