“Sivyo kama Ulimwengu Utoavyo,” Kwa Ajili ya Nguvu kwa Vijana, Mei 2021.
Kikao cha Jumamosi Alasiri
Sivyo kama Ulimwengu Utoavyo
Dondoo
Vurugu na migogoro vitakuwa alama za tabia za uhusiano katika siku za mwisho. …
Akina kaka naa dada, tunaona migogoro mingi sana, hasira, na kwa ujumla ukosefu wa ustarabu kati yetu.
… Pasaka hii acha tujaribu kudumisha amani katika njia ya binafsi, tukitumia mafuta ya neema na uponyaji ya Upatanisho wa Bwana Yesu Kristo kwetu sisi wenyewe na familia zetu pamoja na wale wote walio karibu yetu tunaoweza kuwafikia.
… Tunahitaji kile ambacho maandiko yanakiita “nguvu za mbinguni,” na ili kupata nguvu hizi ni lazima tuishi kwa kile maandiko hayo hayo yanachokiita “kanuni za haki” [Mafundisho na Maagano 121:36]. …
… Kanuni hizo za haki zilijumuisha sifa kama vile, uvumilivu, upole, unyenyekevu na upendo usio unafiki. Bila kanuni hizo, ilikuwa wazi kabisa tungeweza kuishi kwa mifarakano na uadui. …
… Kesho ni Pasaka, wakati wa kanuni za haki za injili ya Yesu Kristo na Upatanisho Wake “zitatimizwa”—kutuepusha na migogoro na ubishi, kutuepusha na dhiki na uvunjaji wa sheria, na hatimaye kushinda kifo. …
Licha ya kusalitiwa na uchungu, kutendewa vibaya na ukatili, na huku akibeba mrundikano wote wa dhambi za familia yote ya binadamu, Mwana wa Mungu Aliye Hai alitazama chini kwenye njia ya maisha ya duniani, akatuona sisi wikiendi hii na kusema: “Amani nawaachieni, amani yangu nawapa: niwapavyo mimi, sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.” (Yohana 14:27). Muwe na Pasaka yenye baraka, furaha na amani.