Hadithi Kuu ya Pasaka Iliyowahi Kusimuliwa
Dondoo
Tunapangilia vipi mafundisho na sherehe ya Ufufuko wa Yesu Kristo, hadithi ya Pasaka, kwa uwiano sawa, utimilifu, na mapokeo mengi ya kidini juu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, hadithi ya Krismasi? …
… Kama nyongeza ya mistari muhimu kuhusu Pasaka katika Agano Jipya, sisi kama Watakatifu wa Siku za Mwisho tumejaliwa zawadi kuu ya Pasaka! … Ndiyo ninarejelea kwenye Kitabu cha Mormoni, na hususani zaidi, kwenye masimulizi ya Yesu Kristo akiwatokea wakaazi kwenye Ulimwengu Mpya, akiwa kwenye utukufu Wake wa ufufuko. …
… Tunatumainia kufanya sura hizi kwenye 3 Nefi kama sehemu muhimu ya desturi yetu ya Pasaka kama Luka 2 ilivyo utamaduni wetu wa Krismasi. Kiukweli, Kitabu cha Mormoni hushiriki hadithi kuu ya Pasaka ambayo imewahi kusimuliwa. Na isiwe hadithi kuu ya Pasaka ambayo haikuwahi kusimuliwa.
Lakini ninawaalika kukitazama Kitabu cha Mormoni kwa nuru mpya na kutafakari ushahidi wake wenye nguvu unaotolewa wa uhalisia wa Kristo aliyefufuka pamoja na wingi na kina juu ya mafundisho ya Kristo. …
Matembezi Yake kama Mwokozi aliyefufuka, yaliyotambulishwa na Mungu Baba, ni ujumbe mtukufu na wa kishujaa wa Pasaka. Utawasaidia wanafamilia wetu kupata ushuhuda binafsi juu ya Yesu Kristo kama Mwokozi na Mkombozi wetu, aliyevunja vifungo vya mauti.