Kikao cha Jumapili Asubuhi
Akili Yangu Ilifikiria Wazo Hili juu ya Yesu Kristo
Dondoo
Hadithi maridadi katika Kitabu cha Mormoni hutwambia kuhusu kijana mdogo, kutoka katika familia maarufu, aitwaye Alma, ambaye maandiko yalimwelezea kama kafiri mwabudu sanamu. …
Katika kukata kwake tamaa, alikumbuka kufundishwa ujanani mwake kuhusu “kuja kwa mtu mmoja aitwaye Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, kulipia dhambi za ulimwengu”[Alma 36:17]. … Alipokata rufaa kuomba nguvu za kiungu za Mwokozi, kitu cha kimuujiza kilitokea. … Ghafla alihisi amani na nuru. …
Alma “alifikiria” ukweli juu ya Yesu Kristo. …
… Akitenda kwa imani kwenye ukweli huo, na kwa nguvu na rehema ya Mungu, aliokolewa kutokana na kuangamizwa na akajawa na tumaini.
… Akili zetu pia “zimefikiria wazo hili” juu ya Yesu Kristo na dhabihu Yake ya rehema, na roho zetu zimehisi nuru na shangwe ambayo huja.
… Upendo wetu kwake Yeye hautukingi dhidi ya huzuni na majonzi kwenye maisha haya ya duniani, bali unaturuhusu kutembea kupita changamoto hizo tukiwa na nguvu zaidi ya uwezo wetu wenyewe. …
Kwa kufokasi umakini wetu kwa Yesu Kristo, vyote vinavyotuzunguka—tukiwa bado hai—huonekana kupitia upendo wetu kwake Yeye. … Kwa umakini unapoendelea kufikiria wazo hili juu ya Yesu Kristo, kumwamini Yeye na kushika amri Zake, sikuahidi tu mwongozo wa kimbingu bali pia uwezo wa kimbingu —uwezo uletao nguvu kwenye maagano yako, amani kwenye magumu yako na shangwe kwenye baraka zako.