Yesu Kristo Ni Faraja
Dondoo
Kila mmoja wetu amebeba begi la mgongoni la kiistiari.
Begi hili la kiistiari ni ambamo ndani yake tunabeba mizigo ya kuishi katika ulimwengu ulioanguka. Mizigo yetu ni kama mawe kwenye begi.
Ninatamka kwa shangwe kwamba mizigo yetu ya kidunia, mawe haya kwenye mabegi yetu ya mgongoni ya kufikirika hayahitajiki kuhisiwa kuwa ni mazito.
Yesu Kristo anaweza kufanya mzigo wetu uwe mwepesi.
Yesu Kristo anaweza kuinua mizigo yetu.
Yesu Kristo anatupatia njia ya kutuondolea uzito wa dhambi.
Yesu Kristo ndiye faraja yetu. …
Basi kwa nini tunang’ang’ania kubeba mawe yetu peke yetu? …
Akina kaka na akina dada, siwezi kufanya peke yangu, na sihitaji iwe hivyo, na sitaki kufanya hivyo. …
Washika maagano wanabarikiwa kwa msaada wa Mwokozi. …
Toba, kupitia Upatanisho wa Yesu Kristo, ndiyo hutuondolea uzito wa mawe ya dhambi. …
Upatanisho wa Yesu Kristo pia hutuwezesha sisi kupokea nguvu ya kusamehe, ambayo huturuhusu kutua uzito tunaobeba kwa sababu ya kutendewa vibaya na wengine.
Basi Mwokozi hutuondolea vipi mizigo ya kuishi katika ulimwengu ulioanguka tukiwa wenye miili ya kidunia yenye kupata huzuni na maumivu?
Mara nyingi, Yeye hutoa aina hiyo ya faraja kupitia sisi! …
Baraka yetu ya agano ni kushirikiana pamoja na Yesu Kristo katika kutoa faraja, ya kimwili na wa kiroho, kwa watoto wote wa Mungu. …
Akina kaka na akina dada, Yesu Kristo ni faraja. Faraja ambayo Yeye hutupatia ni ya milele.