Stahimili Siku katika Kristo
Dondoo
Nimejifunza kutokana na uzoefu binafsi kwamba maandalizi ya kiroho kwa ajili ya ujio wa Bwana si tu muhimu bali ndiyo njia pekee ya kupata amani na furaha.
Ilikuwa siku baridi ya majira ya majani kupuputika niliposikia kwa mara ya kwanza maneno “Wewe una saratani.” …
Kwa sababu ya Yesu Kristo na injili Yake iliyorejeshwa, kama ningekufa, familia yangu ingefarijiwa, ingeimarishwa na siku moja kurejeshwa. Kama ningeishi, ningepata nguvu kuu sana hapa duniani ili kusaidia kunifariji, kunihimili na kuniponya. Mwisho, kwa sababu ya Yesu Kristo, kila kitu kinaweza kuwa SAWA. …
Yesu Kristo hufanya iwezekane kwa ajili yetu “kustahimilli siku.” Kustahimili siku haimaanishi kuongezea kwenye orodha inayoongezeka ya vitu vya kufanya. Fikiria kuhusu lenzi ya kukuzia. Dhumuni lake hasa si tu kufanya vitu vionekane kuwa vikubwa. Pia inaweza kukusanya mwanga na kuufanya kuwa na nguvu zaidi. Tunahitaji tu, kufokasi juhudi zetu na kuwa wakusanyaji wa Nuru ya Yesu Kristo. Tunahitaji uzoefu mtakatifu zaidi na wa ufunuo. …
Uzima wa milele ni shangwe ya milele. Shangwe katika maisha haya, sasa hivi—si kwa sababu ya changamoto za siku yetu bali kwa sababu ya msaada wa Bwana ili kujifunza kutoka kwazo na hatimaye kuzishinda—na shangwe isiyo na kifani katika maisha yajayo. Machozi yatakauka, mioyo iliyovunjika itaponywa, kile kilichopotea kitapatikana, wasiwasi utaondolewa, familia zitarejeshwa tena na vyote vile Baba alivyonavyo vitakuwa vyetu.