Minong’ono ya Roho
Dondoo
Bwana anatualika kutafuta kwa dhati karama zilizo bora, hata karama za roho. Yeye anatoa karama za roho ili kutubariki na ili tuzitumie katika kuwabariki wengine. …
Kutumia karama za roho kunahitaji mazoezi ya kiroho. …
Wenzi wa daima wa Roho Mtakatifu ni moja ya kipawa kikuu cha roho ambacho Watakatifu wa Siku za Mwisho wanakifurahia. …
Acha nitoe kanuni nne za mwongozo ambazo zinaweza kuwa za msaada kwako katika kumwalika na kutambua minong’ono ya Roho.
Ya kwanza ni kusimama mahali patakatifu. …
Pili, simama na watu watakatifu. …
Tatu, shuhudia juu ya kweli takatifu mara nyingi uwezavyo. …
Kanuni ya mwisho ni kumsikiliza Roho Mtakatifu. …
Unapozingatia kanuni hizi za kumwalika na kumtambua Roho, zingatia maneno yafuatayo ya mwongozo wa tahadhari.
Thibitisha misukumo yako ya kiroho. …
Kuwa na uhakika kwamba hisia unazopokea zinaoana na jukumu lako. …
Mambo ya kiroho hayalazimishwi. …
Tumia maamuzi yako mwenyewe yaliyo bora zaidi. …
Ninafunga kwa mwaliko mahususi kwa vijana wote! Wengi wenu mnaanza siku kwa kusimama mbele ya kioo. Kesho, wiki hii, mwaka huu, daima, tulia unapojitazama mwenyewe kwenye kioo. Fikiria, au sema kwa sauti kama unapenda, “Lo, hebu nitazame. Mimi ni wa kupendeza! Mimi ni mwana wa Mungu! Yeye ananijua! Yeye ananipenda! Nina kipawa—nina kipawa cha Roho Mtakatifu kama mwenzi wangu daima!”